Mbunge Gaudence Kayombo akijibu hoja kuhusu matumizi ya mfuko wa jimbo ,amesema mfuko huo una wajumbe 7 hiyo uko kisheria hakuna fedha ambayo ina weza kutumika bila wajumbe kufahamu.Ameahidi kuitisha mkutano ambao uta husisha viongozi wa serekari pamoja na wananchi ili kujibu hoja zilizo tolewa kwenye Mdahalo
Mwakilishi kutoka The Foundation Ciliv Societry akitoa maelekezo kuhusiana na kujaza dodoso
Mwana sheria Komba akiwakilisha mada kuhusu mindo mbinu ya Barabara ,kuwa barabara zetu hazikamiliki kila mwaka zina kuwa mbaya kwa nini tusifuate mfano wa Mwanza wa kujenga barabara kutumia mawe, mawe tunayo kipi kinacho zuia alihoji ?
Mbunge wa Jimbo la Mashariki Mh. Gaudence Kayombo aliye Kulia akisikiliza kwa makini uwakilisho wawananchi kuhusu kero zao kwa Serekari
Mwakilishi wa Radio Maria Jofrey Nilahi akito Live Mdahalo wa Uajibikaji wa Viongozi kwa wananchi na jinsi wananchi wanavyo takiwa kuajibika kwa viongozi wao, watu wasio pungua 3,000,000 waliweza kupata ujumbe kupitia Radio Maria
Washiriki wa Mdahalo wa Uajibikaji viongozi kwa wananchi waliendelea kushangaa pale walipo ambiwa kuwa Tenda za wilaya hiyo hutolewa bila kushirikisha mawazo ya wananchi, wamedai utendaji watenda zinazo tolewa wilayani hapo hazi zingatii utalamu bali zina zingatia zaidi kujuana.
Wananchi walio hudhulia katika mdahalo wa uajibikaji walishangaa kusikia mfanyakazi wa Halimashauri ya Mbinga kusikia katika miaka 19 aliyo fanyia halimashauri hiyo bado ana pata mshahara wa shilingi 30,000/= huku wilaya ya mbinga ikidai kuongoza katika mapato.
washiki katika mdahalo wa uajibikaji wa viongozi wa katika wilaya ya mbinga walihoji vipi katika mdahalo kama huo ulio kusanya watu zaidi ya 250 ukose wawakilishi kutoka serekarini jee huo ndio mshikamano wa viongozi wa serekari na Wananchi ?
Mdahalo ulio fanyika katika wilaya ya Mbinga kuhusu Uajibikaji wa Viongozi kwa wananchi na wananchi wanavyo weza kuajibika kwa viongozi wao ,lakini hilo limeonyesha utengano ulivyo kati ya viongozi na wananchi Viongozi katika kuamua maamuzi ya utekelezaji wa mambo ya maendeleo hawawashirikishi wananchi
No comments:
Post a Comment