Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Amiri Jeshi
Mkuu wa Majenshi Nchini Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Familia ya
Marehehu Rodney Ndunguru na Watanzania wote kuwa na Moyo wa Subira kwa kifo cha
Praiveti Rodney Ndunguru kilicho mpata huko Durfer Sudani 13/7/2013 baada
ya kuvamiwa na waasi
Mheshimiwa Amiri
Jeshi mkuu Jakayaya Mrisho Kikwete ameya sema hayo wakati akitoa salamu za
Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru salalamu zilizo somwa na
mwakilishi wa Briged ya 401 Tembo brged kanaliGeorge
Tomasi Msongole
Jeneza la Rodney Ndunguru muda mfupi kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mjimwema Songea.
Afisa Tawala Wilaya ya Songea Joseph John Kapinga katikati akiwa na Maafisa wa Jeshi katika Maombolezo ya Msiba wa Rodney Ndunguru Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma.
Jeshila la Wananchi (JWTZ) lina taratibu zake katika kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao anapofariki, hapo ni wanajeshi wakitimiza taratibu za heshima za mwisho katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema Songea ikiwa ni ishara ya kumuenzi Shujaa Rodney Ndunguru aliyefariki tar 13/07/2013 huko Darful Sudani akitekeleza Jukumu la Kimataifa la kulinda Amani.
Jeneza lililohifadhi Mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likiwa limetolewa Bendera ya Taifa na Mavazi aliyokuwa akiyatumia tayari kwa kuingizwa kwenye Makao ya milele.
Wanajeshi wakiwa katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Rodney Ndunguru kadiri ya taratibu za ki Jeshi.
Katika mazishi hayo yaliyo fanyika katika
makabuli ya Mjimwema manspaa ya Songea ya liweza kuhudhuliwa na viongozi wa
serekari wa kiwakilishwa na katibu tawala Joseph John Kapinga ,jeshi la
wananchi wa Tnzania ambapo heshima zote za kijeshi zilitolewa
Wanajeshi walioshiriki msiba wa Mwenzao Rodney Ndunguru wakitafakari changamoto zinazowakabili katika kulinda amani.
Mamia ya waombolezaji Wanajeshi wakiwa na huzuni katika kumsikitikia mwenzao aliyekufa kishujaa katika kutekeleza Majukumu ya Kitaifa wakiwa nyumbani kwa Marehemu Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma kabla ya Mazishi.
Padre Noi Duwe akiendesha misa amesema swala la uvunjifu wa
amani una tokana na kuto tii sheria zinazo tolewa serekari badala yake
kuendeleza migomo na maandamano amewataka waumini waache kukashifu serekari
Msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amewaomba wa Tanzania kudumisha amani katika nchi yao bila ya amani ya
kudumisha amani yata tupata yanayo tokea Sudani hivi sasa hatunge weza
kumpoteza ndugu yetu Rodney Ndunguru lakini ni kutokana na kukosekana kwa Amani
Maafisa wa Jeshi wakitoa vifaa vya kazi (kofia, Sare, Mkanda na viatu) alivyokuwa akivitumia Marehemu Rodney Ndunguru wakati wa uhai wake tayari kwa Mazishi
Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakitoa heshima zao za mwisho kwa Shujaa Rodney Ndunguru kwa kupiga Risasi hewani mara baada ya mazishi yake katika Makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea
Captaini Patrick Kitosi kutoka kikosi cha 92 akisoma wasifu
wa marehemu Rodney Ndunguru amesema Rodney Ndunguru alizaliwa 9/7/1985 Mjimwema
mkoani Ruvuma alikuwa kijana shupavu, aliweza kufuzu mafunzo ya ukomandoo dalaja
la pili na dalaja la tatu. Alisha wahi kwenda Dur fur mara mbili katika jitihada
za kulinda amani Umoja wa Mataifa wa Nchi za Afirika alipata nishani akiwa Durfur
Sudani
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete amesema Marehemu
Rodney Ndunguru alipwatwa na mauti hayo wakati akitekeleza jukumu la umoja wa
mataifa wa Africa la ulinziwa amanikatika
eneowalilo shambuliwa ghafula ambapo yeye na wenzake 6 waliweza kupoteza
maisha.
Kanali Goerge Thomas Msongole akisoma salamu hizo kwa niaba ya Amiri
jeshi mkuu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema msiba huu ni wa wa Tanzania wote
na Taifa lote hivyo ni wajibu wetu watanzania wote kushiriki katika maombolezo
na maombi ya kumwombea ndugu yetu Rodney Ndunguru
Jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likitolewa ndani nyumbani kwake Mjimwema Songea tayari kwa kuelekea Makaburini kwenye Makao ya Milele.