KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, October 29, 2013

VIVUTIO VILIVYOKO KATIKA MWAMBAO MWA ZIWA NYASA VYA THIBITISHWA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO SOFIA SIMBA

 Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sofia Simba akifurahia ubaridi wa maji ya ziwa nyasa wilaya Nyasa Mkoani Ruvuma
 Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sofia Simba akinawa maji ya Ziwa Nyasa kuongeza Baraka kama ilivyo Desituri ya Wanyasa
 Kama alivyo fanya Nabii Issa au Yesu Kristo Katika Mto Yorodani ndivyo ilivyo mtokea Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto kuzama katika ziwa nyasa kuongeza baraka za kuhiji katika Ziwa nyasa
 Picha ya Pamoja katika ufukwe wa Ziwa Nyasa kati ya Watoto na Mheshimiwa Waziri Sofia Simba
 Watoto wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wakifurahia ujio  wa waziri wao Mh Sofia Simba
 Juma Nyumayo  Mwandishi Mwandamizi wa Radio Uhuru akitoa heshima kwa Mizimu iliyiko katika Ziwa Nyasa Unamwona alivyo kakamaa
 Nani kama mama Mheshimiwa Sofia Simba katika ziara yake Mkoani Ruvuma alikuwa kioo cha watoto walipenda kuwa naye Muda Wote alipo kuwa hapa Ruvuma
 Unapo ambiwa utalii ni pamoja na vifaa vya jadi vinavyo tumika kuwekea nafaka hicho ni kikapu naungo akipewa Mheshimiwa Waziri Sofia Simba
 Siyo lazima kukaa kwenye kochi ndivyo walivyo mwambia mheshimiwa Waziri Sofia Simba ana weza kujipumzisha kwa kukaa kwenye utefu
 Watu wa Mwambao wa Ziwa Nyasa niwakalimu hakutosha kumpa vitu vya kiutalii bali wali mpa pia kitoweo Mbuzi jike
 Furushi unaliona mbele yako ni Dagaa wa Ziwa Nyasa wananoga kupita kiasi, Kingine hicho ni jamanda ni marufu kwa wangoni kupelekea zawadi kwa ndugu pale wanapo kuwa na Saherehe
 Pamoja na utalii mbalimbali uliopo mkoa wa Ruvuma pia kuna ngoma ya mganda jezi lake ni nguo nyepe tu kama unavyo ona
 Watu wana penda cha unaona wanavyo apa katika kujiunga na CCM Tujiulize kosa liko wapi kwa CCM
 Utulivu wawatoto kusikiliza Waziriwao wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto ni moja ya kuonyesha kukubaliana na Mheshimiwa Sofia Simba
 Hapo siyo wana salimia bali hicho ni kiapo cha kujiunga na chama cha CCM Wilayani Nyasa
 Mkuu wa wilaya ya Nyasa Erenest Kahindi akiwa ana tafakari jinsi ya kuweza kuleta maendeleo katika Wilaya yake
 Mwandisha Chipukizi Juduth Lugoye akiwa na viongozi waandamizi wa Cham,a cha Mapinduzi katika ziara Wilayani Nyasa
 Unasikia Dagaa Nyasa ni hao unao waona katika usanjo ,Dagaa wengi hutumbukizwa ziwani kutokana na vifaa walivyo navyo wavuvi kuwa havina uwezo wa kubeba tani nyingi za samaki au dagaa wanao vuliwa
 Waandishi wa Vyombo mbali mbali wakiwa kazini kuelimisha jamii kile kinacho tendeka
Afisa Utumishi akiwa katika Tafakari kijiuliza jee haya anayo ya fanya Mhesmiwa Waziri na Nitayafikia.

Monday, October 21, 2013



Adam Nindi, Songea.



Dereva wa Shirika la Umeme TANESCO Tawi la Songea, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha ajali katika Msafara wa Waziri wa Maendeleo Mifugo na  Uvuvi Dr David Mathayo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ajali ilyotokea kutoka Mbambabay – Songea na kusababisha watu 5 kujeruhiwa ambao walilazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.



Akimtaja Dereva anayeshikiliwa na Polisi amemtaja ni Ahamadi Hamisi 33 ambaye alikuwa akiendesha Gari lenye lenye No. za Usajili SU 37788  TOYOTAHilax iliyo  igonga gari no stk 9906 mali ya RAS Mkoa wa Ruvuma Akiwataja waandishi wa habari walio pata ajali na kulazwa ni   Joseph Mwambije, Lauf Mohamed, Lauf Mohamed, Cresensia Kapinga na Joicy Joliga na mwingine ni Abiria mmoja aliyekuwa kwenye Gari la TANESCO.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki ameelezea  Madereva wa Shirika la TANESCO  Mkoani Ruvuma pamoja na kupewa onyo wamekuwa wakiendelea kwanda kwa  mwendo kasi.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Madereva wa Shirika la TANESCO ambao huendesha kwa kasi gari zao, mara nyingi wapitapo mitaani wamekuwa wakizomewa na Wananchi ikiwa ni ishara ya kupinga mwendo mkali



 lakini hata hivyo wao huishia kuongeza mwendo .  Dereva Ahamad Hamis anayeshikiliwa na Polisi anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa Mahakamani.  



Waziri wa Maendeleo, uvuvi na Mifugo Dr. David Mathayo alikuwa Ziarani Mkoani Ruvuma kwa kutoa Majibu ya Utafiti juu Samaki waliokuwa wanakufa Ovyo katika Ziwa Nyasa Wilayani Nyasa na kugundua ilitokana na Uchafuzi wa Hali ya Hewa na siyo Sumu.

Thursday, October 17, 2013

MKULIMA APATA MAENDELEO KUTOKANA NA KILIMO RUVUMA


Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa inayotegemewa kwa upande wa Kilimo. Mkoa wa Ruvuma ambao una wakaazi 1,400,000,  ambao wakaazi wake hutemea Kilimo kwa asilimia 80%. Maendeleo ya Kilimo katika Mkoa huu yalianzishwa Mwaka 1977 wakati Agizo la Mlale lilipoanzishwa kwa madhumuni ya kumfanya kila mwana Ruvuma kushiriki katika Kilimo.

Miongoni mwa Wananchi waliounga mkono suala hilo ni Mzee Aizack Mwilamba ambaye alizaliwa 9.10.1966 amekuwa Mkulima toka Mwaka  1977 ambapo shughuli zake za Kilimo alianzia Kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano Peramiho Songea Vijijini kwa kulima Ekari 150 ambazo kila mwaka hutoa kiasi cha Tani 250 na kuendelea.
 Mwilamba katika uwekezaji wake ameweza kusaidia kutoa ajirakwa vijana kama anavyo onekana dada huyo hapo juu ni mfanyakazi wake ambaye anamlipa kwa kazi ya kuuza pembejeo miongoni mwa biashara zake.
 Mwilamba amekuwa Mtaalamu wa Mbolea ambazo haziwezi kumwangusha Mkulima, Pia amekuwa wakala wa Mbolea kwa mda mrefu ambapo yeye Pembejeo za Kilimo huweza kumpelekea moja kwa moja Mkulima Shambani.
 Mke wa Izacki Mwilamba akiwa katika duka la vifaa vya ujenzi (hard ware) Duka lililotokana na mtaji wa Kilimo linapatikana  mtaa wa Sokoine barabara kuu ya lami iendayo Songea - Mbambabay.
 Mwilamba ameweza kuwa wezesha ndugu zake na kuwawezesha na wao kumiliki Miradi ya Maduka ya Pembejeo katika mtaa wa Zanzibar Manspaa ya Songea huyi ni mdogo wake akiwa katika Duka lake.
 Mkulima Stadi Izack Mwilamba amesema Kilimo ukikizingatia kinakutoa katika Umaskini. Hivi sasa kutokana na Kilimo ameweza Kujenga Hoteli kubwa ya Kisasa yenye Ghorofa tatu ambayo iko Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani Stendi hiyo inajulikana kwa jina la UGABE

 
 Huyo hapo juu ni mdogo wake Mkulima Izack Mwilamba akiwa katika moja ya Maduka ya Kaka yake ambalo lipo Stendi Kuu Mjini Songea.
 Izack Mwilamba ni Mkulima na wakala ambaye amekuwa na maduka 4 ya kuuzia Pembejeo za Kilimo Mkoani Ruvuma, Pia ni wakala wa Pembejeo katika Maeneo ya Peramiho ambapo Uwakala wake umeungwa mkono na Viongozi wa Serikali Mkoa wa Ruvuma akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti. Hata hivyo amewashukuru wasambazaji wa Mbegu za Mahindi aina ya PAN kuwa mbegu zao ni Bora na zina Tija