Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa inayotegemewa kwa upande wa Kilimo. Mkoa wa Ruvuma ambao una wakaazi 1,400,000, ambao wakaazi wake hutemea Kilimo kwa asilimia 80%. Maendeleo ya Kilimo katika Mkoa huu yalianzishwa Mwaka 1977 wakati Agizo la Mlale lilipoanzishwa kwa madhumuni ya kumfanya kila mwana Ruvuma kushiriki katika Kilimo.
Miongoni mwa Wananchi waliounga mkono suala hilo ni Mzee Aizack Mwilamba ambaye alizaliwa 9.10.1966 amekuwa Mkulima toka Mwaka 1977 ambapo shughuli zake za Kilimo alianzia Kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano Peramiho Songea Vijijini kwa kulima Ekari 150 ambazo kila mwaka hutoa kiasi cha Tani 250 na kuendelea.
Mwilamba katika uwekezaji wake ameweza kusaidia kutoa ajirakwa vijana kama anavyo onekana dada huyo hapo juu ni mfanyakazi wake ambaye anamlipa kwa kazi ya kuuza pembejeo miongoni mwa biashara zake.
Mwilamba amekuwa Mtaalamu wa Mbolea ambazo haziwezi kumwangusha Mkulima, Pia amekuwa wakala wa Mbolea kwa mda mrefu ambapo yeye Pembejeo za Kilimo huweza kumpelekea moja kwa moja Mkulima Shambani.
Mke wa Izacki Mwilamba akiwa katika duka la vifaa vya ujenzi (hard ware) Duka lililotokana na mtaji wa Kilimo linapatikana mtaa wa Sokoine barabara kuu ya lami iendayo Songea - Mbambabay.
Mwilamba ameweza kuwa wezesha ndugu zake na kuwawezesha na wao kumiliki Miradi ya Maduka ya Pembejeo katika mtaa wa Zanzibar Manspaa ya Songea huyi ni mdogo wake akiwa katika Duka lake.
Mkulima Stadi Izack Mwilamba amesema Kilimo ukikizingatia kinakutoa katika Umaskini. Hivi sasa kutokana na Kilimo ameweza Kujenga Hoteli kubwa ya Kisasa yenye Ghorofa tatu ambayo iko Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani Stendi hiyo inajulikana kwa jina la UGABE
Izack Mwilamba ni Mkulima na wakala ambaye amekuwa na maduka 4 ya kuuzia Pembejeo za Kilimo Mkoani Ruvuma, Pia ni wakala wa Pembejeo katika Maeneo ya Peramiho ambapo Uwakala wake umeungwa mkono na Viongozi wa Serikali Mkoa wa Ruvuma akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti. Hata hivyo amewashukuru wasambazaji wa Mbegu za Mahindi aina ya PAN kuwa mbegu zao ni Bora na zina Tija
No comments:
Post a Comment