Adam Nindi, Songea.
Dereva wa Shirika la Umeme
TANESCO Tawi la Songea, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha ajali
katika Msafara wa Waziri wa Maendeleo Mifugo na
Uvuvi Dr David Mathayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma Deusdedit Nsmeki aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari kuhusu Ajali ilyotokea kutoka Mbambabay – Songea na kusababisha watu 5
kujeruhiwa ambao walilazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
Akimtaja Dereva
anayeshikiliwa na Polisi amemtaja ni Ahamadi Hamisi 33 ambaye alikuwa akiendesha
Gari lenye lenye No. za Usajili SU 37788
TOYOTAHilax iliyo igonga gari no stk 9906 mali ya RAS Mkoa
wa Ruvuma Akiwataja waandishi wa habari walio pata ajali na kulazwa ni Joseph Mwambije, Lauf Mohamed, Lauf Mohamed,
Cresensia Kapinga na Joicy Joliga na
mwingine ni Abiria mmoja aliyekuwa kwenye Gari la TANESCO.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit
Nsmeki ameelezea Madereva wa Shirika la TANESCO Mkoani Ruvuma pamoja na kupewa onyo wamekuwa
wakiendelea kwanda kwa mwendo kasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Madereva wa Shirika la TANESCO ambao huendesha
kwa kasi gari zao, mara nyingi wapitapo mitaani wamekuwa wakizomewa na Wananchi
ikiwa ni ishara ya kupinga mwendo mkali
lakini hata hivyo wao huishia kuongeza mwendo
. Dereva Ahamad Hamis anayeshikiliwa na
Polisi anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa Mahakamani.
Waziri wa Maendeleo, uvuvi na Mifugo Dr. David Mathayo alikuwa Ziarani Mkoani
Ruvuma kwa kutoa Majibu ya Utafiti juu Samaki waliokuwa wanakufa Ovyo katika
Ziwa Nyasa Wilayani Nyasa na kugundua ilitokana na Uchafuzi wa Hali ya Hewa na
siyo Sumu.
No comments:
Post a Comment