KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, November 19, 2013

TMF KUJENGA UWEZO WA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO (BLOGGERS) KUTOKA MIKOANI NAMNA YA KURIPOTI HABARI ZA UCHUNGUZI

 Kutoka kulia Meza ya mbele ni Leader Mentor wa Mafunzo Mahiri na ya aina yake Bw. Beda Msimbe anayefuatia ni Bw. Japhet Sanga kutoka TMF wanaoendesha Mafunzo ya kujengea uwezo wa waandishi wa Habari wa Blogu kutoka Pembezoni na wa tatu ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bw. Saimon Mkina wakifafanua kwa waandishi wa Mafunzo yanayoendelea Dodoma Hotel Ukumbi wa Mvumi kuwapika waandishi kujikita na Maadili katika kazi yao.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wanaoendelea na Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi Mitandaoni (Blogging) wakifuatilia kwa makini mbinu na namna ya kupambana na changamoto za kiuandishi kwa kuzingatia misingi ya uandishi.
 Aliyesimama ni mwandishi wa Iringa Fransince Godwin akishirikisha uzoefu wa kazi ya uandishi wa Blog na faida zake na matatizo yanayopatikana katika uandishi. Akisistiza kuwa cha muhimu ili kuwa mwandishi bora ufahamu namna ya kukwepa matatizo kwa kutumia ushahidi na uhakika katika habari yako kabla ya kuituma
 Afisa wa TMF Bw. Japhet Sanga akiwatoa hofu waandishi na kuwasisitiza fursa zipo nyingi TMF ni juu ya Waandishi kuzingatia matakwa ya uandishi kwa kufanya kazi kadiri ya Matakwa yao na kuwa milango iko wazi kwa Ufadhili wanaoupata ajili ya kuwajengea uwezo waandishi jinsi ya kuripoti habari zinazosaidia Jamii na kutatua Matatizo yanayowakabili ili ifikea wakati waandishi waachane na habari za uchochezi au zinazoleta migogoro na kutothamini utu na haki za binadamu.
 Waandishi wa Blog wakifuatilia kwa makini Mafunzo baada ya kugundua yanawagusa na yana umuhimu mkubwa katika kazi yao katika kujiweka salama na ulinzi wa kazi wanazozifanya, aliyesimama ni Mwandishi wa Blog kutoka Ruvuma akichangia mada juu ya changamoto zinazowapata waandishi unapofuatilia habari za uchunguzi hasa zinazogusa kuonyesha uhalisia na hali ukieleza uhalisia unakiuka maadili ya kutomtendea haki mlengwa.
Mwandishi kutoka Dodoma akichangia katika Mafunzo ambayo kiukweli yana umuhimu na kuamsha hamasa kubwa ya waandishi kuhitaji kujifunza zaidi kwa umuhimu wake kutokana na namna wanavyowezesha wakufunzi mahiri waliobobea Bw. Beda Msimbe na Saimon Mkina.

No comments:

Post a Comment