KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, April 29, 2015

TTCL YAWA MKOMBOZI KWA WANANCHI WA WILAYA YA MBINGA KUPATA MAWASILIANO KUPITIA MNARA WENYE GHARAMA YA SH. MILIONI 51 NA LAKI TATU KUJENGWA KATA YA KIHUNGU.


Umati wa Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukioa la kihistoria kwao la kupata Mawasiliano kujionea Uzinduzi wa Mnara. Hao ni wakazi wa Kijiji cha Kihungu Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akizindua Mawasiliano ya Simu Mtandao wa TTCL Katika Ghafula ya Uzinduzi wa Mnara wa TTCL wenye urefu wa Mita 50 toka juu katika Kijiji cha Kihungu Kata ya Kihungu Wilani Mbinga Mkoani Ruvuma. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Mh Gaudens Kayombo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akikata Utepe kuashiria Kiu ya Muda mrefu ya kukosa Mawasiliano kwa wakazi wa Vijiji vya Kihungu, Mipeta, Mwangaza, Ruhehe, Kizuka na Ruvuma chini sasa imepatiwa ufumbuzi kupitia Shirika la Simu la TTCL.
 Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini  Juvenal Utafu  Akitoa Maelekezo kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga juu ya mradi ulivyotekelezwa  chini ya Shirika la simu la TTCL.
 Kikundi cha Ngoma maarufu kwa jina la Kihoda kutoka Kijiji cha Kihungu Kata ya Kihungu Wilayani Mbinga kikitumbuiza kufurahia kuletewa huduma ya Mawasiliano ambayo ilikuwa ni kitendawili kwao kwa kuwa awali iliwalazimu kupanda juu ya miti au milima kutafuta mawasiliano, lakini kwa sasa suluhisho limepatikana kupitia Mtandao wa Kimataifa wa TTCL.
 Akuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akihutubia Wananchi wa Kata ya Kihungu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Mara Baada ya uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL ambao utawafikia wakazi zaidi ya lakimoja. Amewataka Wananchi kutunza na kulinda Mnara huo ili watumie kwa muda mrefu. Pia amewakumbusha wananchi kutumia Vizuri mawasiliano kwa lengo la kuleta maendeleo wasitumie kwa jili ya kutuma meseji au mawasilikano yenye kuashiria uvunjifu wa amani.
 Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa akitoa Ufafanuzi kwa wananchi wa Kata ya Kihungu waiohudhuria shughuli ya Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano ya Simu wa TTCL uliojengwa chini ya Mpango wa Serikali wa Kusambaza Mawasiliano V ijijini kazi kubwa ya wananchi ni kujitokeza kuitumia huduma kwa umakini.
 Wananchi wa Kata ya Kihungu na Vijiji jirani vinavyoizunguka kata hiyo wakiwa na Nyuso za furaha baada ya kupata Mawasiliano na kujiona na wao wako kwenye ulimwengu wa utandawazi kupitia Mawasiliano ya TTCL.
 Meneja wa TTCL Nyanda za juu Kusini Juvenal Utafu amesema Wananchi wategemee kupata mawasiliano mazuri kutokana na kuboreka kwa huduma za TTCL. Lengo likiwa kufikisha huduma kwa Wananchi walio Pembezoni. Mnara uliozinduliwa umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 51 na Laki Tatu.
 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki ambako Mradi Umetekelezwa Mh. Gaudensi Kayombo amewataka Viongozi TTCL kuboresha huduma zaidi kwa kupeleka huduma katika maeneo mengi zaidi ambako mawasilino ni tatizo.
 Wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL Kijiji cha Kihungu Kata ya Kihungu wakifuatilia tukio la uzinduzi kwa karibu mahali ambapo mnara umejengwa.
 Meneja wa TTCL Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akiongoza Msafara wa Mgeni Rasmi kuelekea kwenye eneo la uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa TTCL Kijijini Kihungu Kata ya kihungu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
 Mgeni Rasmi katika ghafla ya Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano ya Simu wa TTCL Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akifanya Mawasiliano kuthibitisha kama Mawasiliano yako vizuri ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Mawasiliano hayo yaliyowezeshwa na Shirika la TTCL kupitia Mpango wa kusambaza huduma za Mawasiliano Vijijini.


 Shambra shambra na Nderemo unazolziona ni furaha kubwa ya Wakazi wa Kijiji cha Kihungu kwa kufikiwa na huduma ya Mawasiliano katika Kata ya Kihungu ambayo itawarahisishia kuharakisha shughuli za Maendeleo kupitia Mawasilikano ya Simu ambayo haikuwa rahisi kuwafikia hapo awali. Hiki ni Kikundi cha Ngoma aina ya Kihoda ikisherehesha wakati wa uzinduzi wa Mnara.
 Maafisa wa TTCL wakisimamia na kuongoza Zoezi la Kutoa zawadi ya Simu kwa Viongozi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi, kutoka kulia mwenye maiki ni Meneja wa Biashara TTCL Mkoa wa Ruvuma Victor Njila, anayefuatia ni fundi Umeme wa Kampuni ya Simu ya TTCL Abrahamu Msangi, anayefuatia ni Afisa Mauzo Bw. Domisian  Kumburu na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Nyanda za kusini Juvenal Utafu akifuatilia kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kihungu akipokea zawadi ya simu kwa Mgeni Rasmi kwa ajili ya mawasilikano katika Shule ili kurahisisha utoaji wa tgaarifa na shughuli mbalimbali za shuleni hapo.

 Mkurugenzi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akionyesha Mfano wa Mawasilikano kupitia simu zinazouzwa na Kampuni ya TTCL zinazotoa Mawasilikano kupitia ,mnara uliozinduliwa Kijijini Kihungu Wilayani Mbinga. Amewataka wananchi kununua simu hizo na kufurahia mawasilino hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akiuthibitishia Umma uliopo katika sherehe za Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL kwa kutumia simu hiyo kufanya mawasiliano mbele ya wananchi. Simu unayoiona hapo ni nzuri inanunuliwa kwa gharama ya chini kiasi cha Tsh. 45,000 na unawekewa muda wa hewani wa sh 50,000.
 Mkurugenzi wa TTCL Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akimpa mkono Diwani wa Kata ya Kihungu Bonifance mpepo mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya simu kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Kata.
 Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudensi Kayombo anayefuatia ni Mkuu wa wilaya ya Mbinga na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanda za juu kusini wakielekea kwenye eneo la uziknduzi wa Mnara.
 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki akihutubia Wananchi wa Kata ya Kihungu wakati wa Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL.
 Eneo ambapo Mnara umejengwa kama unavyoonekana pichani limetolewa Bure na Wananchi wa Kijiji cha Kihungu ili kunusuru madhara waliyokuwa wakiyapata kwa kukosa mawasilikano kutokana na kuwaletea ugumu wa kufikisha mawasiliano.
 Wakazi wa Kijiji cha Kihungu wakiwa foleni ya kuhakikisha wanapata huduma ya kununua simu na watoa huduma wakiendelea kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa.
 wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi katika ghafula ya uzinduzi wa Mnara.
 Huo ni mwonekano wa Jengo ambapo Mnara umejengwa kijijini  Kihungu.
 Hapo ni eneo amb apo uzinduzi umefanywa.
 Watoa Huduma kwa  wateja kutoka kampuni ya TTCL Mkoa wa Ruvuma wakiendelea na huduma ya kuuza simu na kutoa elimu ya matumizi ya simu hizo kwa wateja Kijijini Kihungu siku ya Uzinduzi wa Mnara wa Simu, kutoka kulia ni Gothad Gama na anayefuatia ni Sikudhani ponera


 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL
 Mkurugenzi wa Nyanda za Juu kusini Juvenal Utafu akimpokea Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga.
 Mgeni Rasimi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akisalimiana na Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa kwenye eneo la Uzinduzi.
 Mkurugenzi wa Nyanda za Juu Kusini akibadilishana Mawazo na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga jinsi ya Kuboresha huduma zaidi ili kuwafikia wananchi wengi.
 Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa kushoto akiwa na Afisa Biashara wa TTCL Victor Njilwa katika Viwanja vya Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL Kijijini Kihungu.
 Mganga wa Zahanati ya Kihungu akipokea Zawadi ya Simu kwa ajili ya Mawasiliano ya Zahanati
 Diwani wa Kata ya Kihungu akifurahia zawadi ya Simu ya TTCL kwa kuwa itarahisisha mawasiliano katika utendaji wake wa kazi.


 Wakala Mkubwa wa TTCL Kata ya Kihungu Mwalimu Ndunguru akijipatia zawadi ya Simu kwa ajili ya matumizi ya shughuli za uwakala katika kuongeza ufanisi wa kazi zake kwa wateja.


Sunday, April 26, 2015

BENKI YA NMB SONGEA YA TOA SARE ZA HALAIKI ZENYE THAMAN YA SHILINGI MILIONI 31



Benk ya NMB Tanzania  kwa mwaka 2015 imetenga kiasi cha shilingi Bilioni Moja  kwa ajili ya majanga mbalimbali ikiwa na pomoja na maswala yanayo husu Elimu ,Afya, ikiwa na pamoja na sherehe za kitaifa kama sherehe za mwenge.




Meneja wa Benk ya NMB Tawi la Songea Rehema Nasibu ameya sema hayo wakati akikabidhi sale za hallaiki ya Mwenge  katika ikulu ndogo songea zikiwa na thamani ya shilingi milioni 31.



Meneja wa Benki ya  NMB Tawi la songea Rehema Nassibu amesema msaada unao tolewa na Benk ya NMB  kwa wananchi ni moja ya kuonyesha kuwa faida inayo patikana ina rudi kwa wananchi ili ifanye kazi za maendeleo

Meneja wa Benki ya NMB Bibi Rehema Nassib akimwonyesha sample ya sare za TRUCKSUT zitakazotumiwa na chipkizi wa Halaiki katika Sherehe za Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru 2015.
Mkururenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma said Thabit Mwambungu wakikagua Sare za Vijana wa Halaiki itakayotumbuiza katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwenye Uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Said Thabit Mwambungu akifurahi kuona Benki ya NMB inavto wajali wananchi wake kwa kuthubutu kushiriki katika kufanikisha Shughuli mbalimbali za Maendeleo zinazofanyika Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kulia Mh. Said Thabit Mwambungu akipokea zawadi ya Trucksut za Halaiki kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Bibi Rehema Nassib.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma said Thabit Mwambungu Mwenye Suti katikati  akiwa na Viongozi waandamizi wa Benki ya NMB na viongozi wa Manispaa ya Songea, kulia ni Afisa Biashara wa Mkoa wa Ruvuma Nehemia James na anayefuatia  ni Kaim RAS Joel Mbewa.
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Benki ya NMB Tawi la Songea na Mstahiki Meya wa Maniospaa ya Songea Charles Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa wakiwa na wakufunzi  wa Halaiki baada ya kukabidhiwa zawadi ya Sare za Halaiki
Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB Kushoto na Afisa Masoko wa Benki ya NMB wakibadilishana Mawazo namna ya kufanikisha zoezi la kukabidhi zawadi ya Sare za halaiki kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu, muda mfupi kabla ya kukabidhi Ikulu Ndogo Songea.
Stafu wa Benki ya NMB Tawi la Songea wakiwa tayari kwa kukabidhi TRUCKSUT 1000 kwa ajili ya Halaiki ya Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu kitaifa mbio zake zinazinduliwa Songea Mkoani Ruvuma tar. 29/04/2015 katika Uwanja wa Majimaji.
Maafisa Kutoka Bnki ya NMB Tawi la Songea wakifurahia kufanikisha lengo la kurudisha faida kwa wananchi kupitia kushiriki katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii, hapo ni muda mfupi kabla ya kukabidhi Sare aina ya Trucksut kwa ajili ya watoto wa Halaiki ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Ruvuma. Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Rehema Nassib, Kushoto ni Afisa Mahusiano Bw. Shaban na kulia ni Afisa Masoko.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Rehema Nassib akifafanua dhima ya Benki ya NMB kuamu kusaidia Shughuli za jamii ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana katika Benki hiyo kwa Wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama aliyesimama Katikati akifurahia Msaada wa jezi za Rtucksut zilizotolewa na NMB kwa ajili ya Halaiki ya Sherehe za Mwenge Mwaka huu Mkoani Ruvuma. Kulia Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Joeli Mbewa
Kushoto ni Mkufunzi Mkuu wa Halaiki ya chipkizi wa Mkoa wa Ruvuma wanaotarajia kusheherehesha siku ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge 29/04/2015 kitaifa Mkoani Ruvuma Manispaa ya Songea.
Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa na Wakufunzi wa Halaiki, Ikulu Ndogo Songea Mkoani Ruvuma
Maafisa wa Benki ya NMB wakiwa na Viongozi mbalimbali kushuhudia tukio la Kupokea Sare ya Vijana wa Halaiki aina ya Rtucksut 1000 zilizotolewa kwa ufadhili wa Benki ya NMB.
Wakufunzi wa Halaiki na Viongozi waandamizi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakisubiri kupokea mavazi ya Vijana wa Halaiki ya Mwenge.
Wakufunzi wa Halaiki ambao wanawanoa Vijana Chipukizi watakaosherehesha katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge mwaka Huu Kitaifa Mkoani Ruvuma.
Waandishi wa Habari wakiwa katika kazi Ikulu ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Pichani ni Mwakilishi wa Redio Free Afrika na Star Tv Bi Judith Lugoye na anayeonekana kwa mbele ni Mwakilishi wa TBC Songea Hamza Mashole.
Meneja wa Benk ya NMB Songea Rehema Nasibu akiwa na Afisa Biashara Nemia wakati wakiwa Ikulu ndogo katika Manspaa ya Songea wakati wa kukabidhi Sare za Halaiki kwa Mkuu waMkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu
Wadau m balimbali wa Maendeleo waliojitokeza kupokea Msaada wa Sare za Halaiki kwa ajili ya Sherehe za Mwenge wa uhuru wakisubiri kwa hamu kupokea zawadi hiyo katika Ukumbi wa Ikulu ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mjini Songea
wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB Tawi la Songea Bw Shaban akihakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika kufanikisha zoezi la kukabidhi pea 1000 za Truck sut zikiwa na thamani ya Shilingi milioni 31 kwa ajili ya vijana wa Halaiki ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru, anayefuatia ni Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Songea, anayefuata ni Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Afisa Biashara wa Mkoa Bw. Nehemia James.