Umati wa Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukioa la kihistoria kwao la kupata Mawasiliano kujionea Uzinduzi wa Mnara. Hao ni wakazi wa Kijiji cha Kihungu Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma. |
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akikata Utepe kuashiria Kiu ya Muda mrefu ya kukosa Mawasiliano kwa wakazi wa Vijiji vya Kihungu, Mipeta, Mwangaza, Ruhehe, Kizuka na Ruvuma chini sasa imepatiwa ufumbuzi kupitia Shirika la Simu la TTCL.
Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini Juvenal Utafu Akitoa Maelekezo kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga juu ya mradi ulivyotekelezwa chini ya Shirika la simu la TTCL.
Kikundi cha Ngoma maarufu kwa jina la Kihoda kutoka Kijiji cha Kihungu Kata ya Kihungu Wilayani Mbinga kikitumbuiza kufurahia kuletewa huduma ya Mawasiliano ambayo ilikuwa ni kitendawili kwao kwa kuwa awali iliwalazimu kupanda juu ya miti au milima kutafuta mawasiliano, lakini kwa sasa suluhisho limepatikana kupitia Mtandao wa Kimataifa wa TTCL.
Akuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akihutubia Wananchi wa Kata ya Kihungu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Mara Baada ya uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL ambao utawafikia wakazi zaidi ya lakimoja. Amewataka Wananchi kutunza na kulinda Mnara huo ili watumie kwa muda mrefu. Pia amewakumbusha wananchi kutumia Vizuri mawasiliano kwa lengo la kuleta maendeleo wasitumie kwa jili ya kutuma meseji au mawasilikano yenye kuashiria uvunjifu wa amani.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa akitoa Ufafanuzi kwa wananchi wa Kata ya Kihungu waiohudhuria shughuli ya Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano ya Simu wa TTCL uliojengwa chini ya Mpango wa Serikali wa Kusambaza Mawasiliano V ijijini kazi kubwa ya wananchi ni kujitokeza kuitumia huduma kwa umakini.
Wananchi wa Kata ya Kihungu na Vijiji jirani vinavyoizunguka kata hiyo wakiwa na Nyuso za furaha baada ya kupata Mawasiliano na kujiona na wao wako kwenye ulimwengu wa utandawazi kupitia Mawasiliano ya TTCL.
Meneja wa TTCL Nyanda za juu Kusini Juvenal Utafu amesema Wananchi wategemee kupata mawasiliano mazuri kutokana na kuboreka kwa huduma za TTCL. Lengo likiwa kufikisha huduma kwa Wananchi walio Pembezoni. Mnara uliozinduliwa umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 51 na Laki Tatu.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki ambako Mradi Umetekelezwa Mh. Gaudensi Kayombo amewataka Viongozi TTCL kuboresha huduma zaidi kwa kupeleka huduma katika maeneo mengi zaidi ambako mawasilino ni tatizo.
Wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL Kijiji cha Kihungu Kata ya Kihungu wakifuatilia tukio la uzinduzi kwa karibu mahali ambapo mnara umejengwa.
Meneja wa TTCL Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akiongoza Msafara wa Mgeni Rasmi kuelekea kwenye eneo la uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa TTCL Kijijini Kihungu Kata ya kihungu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Mgeni Rasmi katika ghafla ya Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano ya Simu wa TTCL Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akifanya Mawasiliano kuthibitisha kama Mawasiliano yako vizuri ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Mawasiliano hayo yaliyowezeshwa na Shirika la TTCL kupitia Mpango wa kusambaza huduma za Mawasiliano Vijijini.
Shambra shambra na Nderemo unazolziona ni furaha kubwa ya Wakazi wa Kijiji cha Kihungu kwa kufikiwa na huduma ya Mawasiliano katika Kata ya Kihungu ambayo itawarahisishia kuharakisha shughuli za Maendeleo kupitia Mawasilikano ya Simu ambayo haikuwa rahisi kuwafikia hapo awali. Hiki ni Kikundi cha Ngoma aina ya Kihoda ikisherehesha wakati wa uzinduzi wa Mnara.
Maafisa wa TTCL wakisimamia na kuongoza Zoezi la Kutoa zawadi ya Simu kwa Viongozi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi, kutoka kulia mwenye maiki ni Meneja wa Biashara TTCL Mkoa wa Ruvuma Victor Njila, anayefuatia ni fundi Umeme wa Kampuni ya Simu ya TTCL Abrahamu Msangi, anayefuatia ni Afisa Mauzo Bw. Domisian Kumburu na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Nyanda za kusini Juvenal Utafu akifuatilia kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kihungu akipokea zawadi ya simu kwa Mgeni Rasmi kwa ajili ya mawasilikano katika Shule ili kurahisisha utoaji wa tgaarifa na shughuli mbalimbali za shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akionyesha Mfano wa Mawasilikano kupitia simu zinazouzwa na Kampuni ya TTCL zinazotoa Mawasilikano kupitia ,mnara uliozinduliwa Kijijini Kihungu Wilayani Mbinga. Amewataka wananchi kununua simu hizo na kufurahia mawasilino hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akiuthibitishia Umma uliopo katika sherehe za Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL kwa kutumia simu hiyo kufanya mawasiliano mbele ya wananchi. Simu unayoiona hapo ni nzuri inanunuliwa kwa gharama ya chini kiasi cha Tsh. 45,000 na unawekewa muda wa hewani wa sh 50,000.
Mkurugenzi wa TTCL Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akimpa mkono Diwani wa Kata ya Kihungu Bonifance mpepo mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya simu kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Kata.
Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudensi Kayombo anayefuatia ni Mkuu wa wilaya ya Mbinga na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanda za juu kusini wakielekea kwenye eneo la uziknduzi wa Mnara.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki akihutubia Wananchi wa Kata ya Kihungu wakati wa Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL.
Eneo ambapo Mnara umejengwa kama unavyoonekana pichani limetolewa Bure na Wananchi wa Kijiji cha Kihungu ili kunusuru madhara waliyokuwa wakiyapata kwa kukosa mawasilikano kutokana na kuwaletea ugumu wa kufikisha mawasiliano.
Wakazi wa Kijiji cha Kihungu wakiwa foleni ya kuhakikisha wanapata huduma ya kununua simu na watoa huduma wakiendelea kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa.
wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi katika ghafula ya uzinduzi wa Mnara.
Huo ni mwonekano wa Jengo ambapo Mnara umejengwa kijijini Kihungu.
Hapo ni eneo amb apo uzinduzi umefanywa.
Watoa Huduma kwa wateja kutoka kampuni ya TTCL Mkoa wa Ruvuma wakiendelea na huduma ya kuuza simu na kutoa elimu ya matumizi ya simu hizo kwa wateja Kijijini Kihungu siku ya Uzinduzi wa Mnara wa Simu, kutoka kulia ni Gothad Gama na anayefuatia ni Sikudhani ponera
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL
Mkurugenzi wa Nyanda za Juu kusini Juvenal Utafu akimpokea Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga.
Mgeni Rasimi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akisalimiana na Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa kwenye eneo la Uzinduzi.
Mkurugenzi wa Nyanda za Juu Kusini akibadilishana Mawazo na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga jinsi ya Kuboresha huduma zaidi ili kuwafikia wananchi wengi.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma John Nindwa kushoto akiwa na Afisa Biashara wa TTCL Victor Njilwa katika Viwanja vya Uzinduzi wa Mnara wa Simu wa TTCL Kijijini Kihungu.
Mganga wa Zahanati ya Kihungu akipokea Zawadi ya Simu kwa ajili ya Mawasiliano ya Zahanati
Diwani wa Kata ya Kihungu akifurahia zawadi ya Simu ya TTCL kwa kuwa itarahisisha mawasiliano katika utendaji wake wa kazi.
Wakala Mkubwa wa TTCL Kata ya Kihungu Mwalimu Ndunguru akijipatia zawadi ya Simu kwa ajili ya matumizi ya shughuli za uwakala katika kuongeza ufanisi wa kazi zake kwa wateja.
No comments:
Post a Comment