Benk ya NMB
Tanzania kwa mwaka 2015 imetenga kiasi
cha shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya
majanga mbalimbali ikiwa na pomoja na maswala yanayo husu Elimu ,Afya, ikiwa na
pamoja na sherehe za kitaifa kama sherehe za
mwenge.
Meneja wa Benk ya NMB
Tawi la Songea Rehema Nasibu ameya sema hayo wakati akikabidhi sale za hallaiki
ya Mwenge katika ikulu ndogo songea
zikiwa na thamani ya shilingi milioni 31.
Meneja wa Benki ya
NMB Tawi la songea Rehema Nassibu amesema msaada unao tolewa na Benk ya
NMB kwa wananchi ni moja ya kuonyesha
kuwa faida inayo patikana ina rudi kwa wananchi ili ifanye kazi za maendeleo
Meneja wa Benki ya NMB Bibi Rehema Nassib akimwonyesha sample ya sare za TRUCKSUT zitakazotumiwa na chipkizi wa Halaiki katika Sherehe za Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru 2015.
Mkururenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma said Thabit Mwambungu wakikagua Sare za Vijana wa Halaiki itakayotumbuiza katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwenye Uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Said Thabit Mwambungu akifurahi kuona Benki ya NMB inavto wajali wananchi wake kwa kuthubutu kushiriki katika kufanikisha Shughuli mbalimbali za Maendeleo zinazofanyika Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kulia Mh. Said Thabit Mwambungu akipokea zawadi ya Trucksut za Halaiki kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Bibi Rehema Nassib.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma said Thabit Mwambungu Mwenye Suti katikati akiwa na Viongozi waandamizi wa Benki ya NMB na viongozi wa Manispaa ya Songea, kulia ni Afisa Biashara wa Mkoa wa Ruvuma Nehemia James na anayefuatia ni Kaim RAS Joel Mbewa.
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Benki ya NMB Tawi la Songea na Mstahiki Meya wa Maniospaa ya Songea Charles Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa wakiwa na wakufunzi wa Halaiki baada ya kukabidhiwa zawadi ya Sare za Halaiki
Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB Kushoto na Afisa Masoko wa Benki ya NMB wakibadilishana Mawazo namna ya kufanikisha zoezi la kukabidhi zawadi ya Sare za halaiki kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu, muda mfupi kabla ya kukabidhi Ikulu Ndogo Songea.
Stafu wa Benki ya NMB Tawi la Songea wakiwa tayari kwa kukabidhi TRUCKSUT 1000 kwa ajili ya Halaiki ya Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu kitaifa mbio zake zinazinduliwa Songea Mkoani Ruvuma tar. 29/04/2015 katika Uwanja wa Majimaji.
Maafisa Kutoka Bnki ya NMB Tawi la Songea wakifurahia kufanikisha lengo la kurudisha faida kwa wananchi kupitia kushiriki katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii, hapo ni muda mfupi kabla ya kukabidhi Sare aina ya Trucksut kwa ajili ya watoto wa Halaiki ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Ruvuma. Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Rehema Nassib, Kushoto ni Afisa Mahusiano Bw. Shaban na kulia ni Afisa Masoko.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Rehema Nassib akifafanua dhima ya Benki ya NMB kuamu kusaidia Shughuli za jamii ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana katika Benki hiyo kwa Wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama aliyesimama Katikati akifurahia Msaada wa jezi za Rtucksut zilizotolewa na NMB kwa ajili ya Halaiki ya Sherehe za Mwenge Mwaka huu Mkoani Ruvuma. Kulia Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Joeli Mbewa
Kushoto ni Mkufunzi Mkuu wa Halaiki ya chipkizi wa Mkoa wa Ruvuma wanaotarajia kusheherehesha siku ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge 29/04/2015 kitaifa Mkoani Ruvuma Manispaa ya Songea.
Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiwa na Wakufunzi wa Halaiki, Ikulu Ndogo Songea Mkoani Ruvuma
Maafisa wa Benki ya NMB wakiwa na Viongozi mbalimbali kushuhudia tukio la Kupokea Sare ya Vijana wa Halaiki aina ya Rtucksut 1000 zilizotolewa kwa ufadhili wa Benki ya NMB.
Wakufunzi wa Halaiki na Viongozi waandamizi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakisubiri kupokea mavazi ya Vijana wa Halaiki ya Mwenge.
Wakufunzi wa Halaiki ambao wanawanoa Vijana Chipukizi watakaosherehesha katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge mwaka Huu Kitaifa Mkoani Ruvuma.
Waandishi wa Habari wakiwa katika kazi Ikulu ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Pichani ni Mwakilishi wa Redio Free Afrika na Star Tv Bi Judith Lugoye na anayeonekana kwa mbele ni Mwakilishi wa TBC Songea Hamza Mashole.
Meneja wa Benk ya NMB Songea Rehema Nasibu akiwa na Afisa Biashara Nemia wakati wakiwa Ikulu ndogo katika Manspaa ya Songea wakati wa kukabidhi Sare za Halaiki kwa Mkuu waMkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu
Wadau m balimbali wa Maendeleo waliojitokeza kupokea Msaada wa Sare za Halaiki kwa ajili ya Sherehe za Mwenge wa uhuru wakisubiri kwa hamu kupokea zawadi hiyo katika Ukumbi wa Ikulu ndogo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mjini Songea
wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB Tawi la Songea Bw Shaban akihakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika kufanikisha zoezi la kukabidhi pea 1000 za Truck sut zikiwa na thamani ya Shilingi milioni 31 kwa ajili ya vijana wa Halaiki ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru, anayefuatia ni Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tawi la Songea, anayefuata ni Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Afisa Biashara wa Mkoa Bw. Nehemia James.
nice bloh and article, thanks for sharing
ReplyDelete