Kaimu Mkurugenzi
Manispaa ya Songea Rafaeli Malini ameyasema hayo wakati akizungumza na
Waandishi wa habari, amesema kwa sasa katika Manispaa ya Songea Vyama vya
Kisiasa vimekuwa vikipachika Mabango kwenye Nyaya za Umeme, simu na Nyumba za
watu ambapo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Kampeni za Uchaguzi Mkoa wa Ruvuma
zinaendelea kwa kishindo kila Chama kikiwa na uhakika wa kushinda Oktoba 25.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Rafaeli Malini amesema amejaribu kuwasiliana na Vyama vya Siasa kuwa aqmbia wanachama wao kuacha kubandika Mabango bila idhini ya watu wanaomiliki katika maeneo hayo pia kuacha kuning’iniza mabango katika nyaya za umeme
Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini Frank Mwaisumba amewaomba
Viongozi wa Serikali za Mitaa mahali walipo kusimamia na kukemea kwa mtu yeyote
atakayeonekana akibandika Mabango katika sehemu zisizohusika, Vijana
wamewahimiza Vijana wenzao kuacha tabia ya kuhatarisha maisha yao kwa kuweka Mabango kwenye Nyaya za Umeme
Wananchi wa Manispaa
ya Songea wametakiwa kuacha mambo ambayo yanaweza kuwafanya wapoteze maisha
ikiwa ni pamoja na kupachika mabango kwenye nyaya za umeme.
Katibu wa Uwt Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja amesema
kuning`iniza Mabango na kuchana Mabango ya Vyama vya siasa ni kinyume cha
Sheria.
|
Kaimu Meneja wa TANESCO Haruna Mwachula akiongea kwa njia ya
simu amesema kutundika Mabango kwenye Nyaya za Umeme ni kulihujumu Shirika la
TANESCO na kulikosesha mapato. Pia ni kuhatarisha Maisha kwa wanao tundika na
wapiti njia.