Jeshi la Police
Mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata Magunia 17 ya Bangi yakiwa na Uzito wa kilo
340.
Bangi iliyokamatwa ikiwa imepekiwa kwenye viloba kama inavyoonekana.
Kaimu Kamanda wa
Police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi amesema amesema Magunia hayo ya Bangi
yamekamatwa katika Kata ya Subira yakiwa kwenye Gari lenye namba za usajili
T588 BBJ ambapo Dereva wa Gari hilo na wenye
mizigo walilitelekeza gari hilo.
Kaimu Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi amesema baada ya kupata taarifa kwa Wasamaria wema walitoa tarifa ya kusafirisha bangi iliyo geuzwa kuwa ni Mahindi ,Mpunga na Mkaa kumbe katikati ya Mpunga na Mahindi viliwekwa viroba 17 vya bangi kama anavyo eleza kaimu kamanda wa police Said Mohamed
Viloba vya Bangi ambavyo vilihifadhiwa katikati ya viloba vya Mahindi na Mpunga ili kuonyesha wenye mzigo walikuwa wakisafirisha mazao.
Bangi ikiwa imefikishwa kituo kikuu cha Police Mkoa wa Ruvuma baada ya kukamatwa.
Namba za Gari iliyokuwa ikisafirisha Mzigo huo wa Madawa ya kulevya aina ya Bangi,
Bangi Iliyovunwa na kujazwa kwenye viloba ambayo ilihifadhiwa kwa ustadi mkubwa lakini Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kuinasa Bangi hiyo.
Viloba 17 vya Bangi iliyokamatwa kata ya Subira Manispaa ya Songea vikiwa vimepangwa pamoja.
Pamoja na Serikali kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uzalishaji, wako watu wanalima kwa wingi na kugeuza kama zao la biashara kwao katika kujinasua na umaskini, shehena za viloba vinavyoonekana hapo juu ni mali ghafi ya madawa ya kulevya ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda kutafuta soko.
Kaimu Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi amesema Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma wanamshikilia mwenye Gari aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 588
BBJ Said Mohamed kwa mahojiano . Bangi hiyo inasadikiwa ili kuwa ikipelekwa mikoa jirani . Kaimu Kamanda wa Police ameomba yeyote mwenye taarifa za Uhalifu atoe taarifa Police.
Police kwa kushirikiana na Wananchi wataweza kupunguza uhalifu wa watanzania, wanachoomba ni ushirikiano wa raia pindi viashiria vya uhalifu vinapotokea.
Kaimu Kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi akitoa ufafanuzi wa jinsi walivyoikamata Bangi hiyo.
Bangi.
No comments:
Post a Comment