Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ametoa agizo kwa Mkurugenzi
wa Manispaa ya Songea kuhakikisha Vyoo vya Hospitali ya Mjimwema na Shule ya
Msingi Majengo vinazibuliwa ili kutoa fursa kwa wagonjwa na wanafunzi kutumia
vyoo hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu alichukua hatua hiyo ya
kutembelea katika Hospitali ya Mjimwema baada ya kusikia kuwa wagonjwa
wanajisaida kwaenye ndoo au mifuko ya
Rambo na kutupa wanako jua wenyewe.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ametoa agizo hilo
kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Jenifa Omolo baada ya kuona mazingira machafu
yaliyopo katika hospitali ya mji mwema. katika ziara ya kusitukiza hospitarini
hapo baada ya kusikia wagonjwa wanaji
saidia kwenye ndoo kutokana na vyoo hivyo kuziba
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika Ziara yake kusitukiza aliyo ifanya
katika Shule ya msingi ya Majengo
yenye wanafunzi 470 amebaini shule hiyo kutokuwa na choo na wanafunzi
kulazimika kujisaidia vichochoroni na katika nyumba jirani hatari zaidi wengine
kujisaidia kandokando ya mto Ruvuma
Wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Mjimwema Manispaa ya
Songea wamesema adha wanayoipata ni pamoja na harufu inayotoka katika vyoo
hivyo, wamesema usafi umefanywa baada ya kubaini kuwa Mkuu wa Mkoa anatembelea
Hospitarini hapo.
No comments:
Post a Comment