Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya
shilingi Milioni 3 kwa mwezi sasa
inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama
hawatayarekebisha kwa muda wa miezi
mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.
Naibu Waziri wa Afya
akiongeza kuhusu Madai ya Watumishi wa Sekta ya Afya, amesema Serikali
inajipanga kulipa Madeni hayo imeanza Mwezi Januari Mwaka huu na itaendelea
kuwalipa Watumishi wote wanaodai stahiki zao.
Ziara ya Naibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr.
Kigwangala ni ya kushitukiza ameweza kutembelea wodi ya watoto, Maabara na
sehemu ya Upasuaji na kukuta changamoto ya baadhi ya Mashine za maabara zikiwa
mbovu na Sehemu ya Upasuaji Vitanda vikiwa vimepitwa na wakati.
Akielezea kuhusu mafanikio ya kutumia mfumo wa
Mashine za ELECTRONIC katika Hospitali ya Rufaa ya Mhimbili asema mapato yame ongezeka mara mbili kuliko mwanzoPia amezipongeza Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma na Hospitali ya Mjimwema kwa kuweza kuboresha Huduma za Mama na Mtoto.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya amesema Hospitali ya
Mkoa hivi sasa baada ya kufunga Mashine za ukusanyaji mapato za ki electroniki
imeweza kuongeza Makusanyo kutoka
shilingi milioni moja laki mbili hadi kufikia milioni 60 kwa mwezi , Naye Mganga Mkuu wa hosptali ya Mkoa
amesema Vifo vya Mama na Mtoto sasa vimepungua kila wanawake 100,000 vifo 95 tu
vinavyotokea.
NAIBU
WAZIRI WA AFYA JINSIA WAZEE NA WATOTO DR. HAMISI KIGWANGALA AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA
HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA NA KITUO CHA AFYA
CHA MJIMWEMA NA KUKUTA CHANGAMOTO YA BAADHI YA MASHINE ZA MAABARA MBOVU NA
BAADHI YA VITANDA VIBOVU KATK CHUMBA CHA UPASUAJI.
Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangala ameyasema hayo katika ziara ya
kusitukiza mkoani Ruvuma alipo tembelea
Hospitali ya songea na Hospitali ya mji mwema Manspaa ya songea
Naibu Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto Dr Hamisi Kigwangala amesema
ukusanyaji wa Mapato kwa kutumia Mfumo wa Electronic umeweza kuongeza Mapato
katika Maeneo yote ya hospitali zinazotumia mfumo wa Mashine za ELECTRONIC
Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili hapo awali ilikuwa inakusanya Mapato kwa kupata Bilioni 2 milini 700 kwa sasa inapata Bilioni 4 milini 400 kwa mwezi. Jambo ambalo linaweza kupunguza
Changamoto zinazowakabili watumishi kwa kulipa Madeni ya Malimbikizi ya madeni
wanayodai.
Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya
shilingi Milioni 3 kwa mwezi sasa
inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama
hawatayarekebisha kwa muda wa miezi
mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.
No comments:
Post a Comment