Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiongoza kikao cha RCC akieleza kipato cha wastani cha Mwana Ruvuma kuwa ni shilingi 2,082,167 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la asilimia 8% ikilinganishwa na mwaka 2013 ambapo ilikuwa shilingi 1,913,516
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akielezea kuhusu mkutano wa ujirani mwema na nchi ya msumbiji uliofanyika 18/2/2016 na kudai katika mambo yaliyo zungumuzwa ni pamoja na manyanyaso yanayo fanyika mipakani mwa nchi hizo na jinsi ya kuzuia wahamiaji haramu kwa kulida mipaka inayo pakana na mkoa Lichinga Nyasa na mikoa ya Mtwara na Ruvuma
Wajumbe wametakiwa kuelimisha wananchi umuhimu wa kuzingatia usafi ili kuendelea kujiepusha na Magonjwa ya mlipuko.
Uzalishaji wa Chakula Mkoa wa Ruvuma katika msimu wa 2014/2015 ulivuka lengo kufikia Tani 1,564,283huku wastani wa mahitaji ya chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma ni Tani 469,172 ziada ikiwa Tani 1,095,111
Uzalishaji wa Mahindi pekee Mkoa wa Ruvuma msimu wa 2014/2015 mavuno yalikuwa Tani 689,123 sawa na ongezeko la asilimia 17.3 za Hekta zilizolimwa.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo msimu huu wa 2015/2016 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema Mkoa umepokea Vocha 234,000 za mbolea ya kupandia na kukuzia na mbegu za mahindi chotara zilizolengwa kuzinufaisha Kaya 78,000 za wakulima. Katika ugawaji wa pembejeo changamoto ni baadhi ya watumishi kujihusisha kukwamisha utekelezaji wa malengo hayo kwa kushirikiana na mawakala wasio waadilifu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kusimamia ipasavyo suala la pembejeo za kilimo na kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuhujumu zoezi hilo lisifanikiwe, sambamba na viongozi wa Vijiji na kata.
Aidha amesisitiza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuwataka NFRA kuacha kununua mahindi kupitia mawakala badala yake wakanunue vijijini kwa wananchi wenyewe kwa bei itakayoelekezwa na Serikali.
Akizungumzia kuhusu Elimu bure amesema wazazi wanapaswa kulipia nauli za wanafunzi, kulipia magodoro, shuka na vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa Bweni na zenye hosteli za Serikali pia ni jukumu lao kuendelea kujitolea nguvu kazi na mali ili kuleta ustawi wa maendeleo ya shule zilizoko ndani ya Jamii.
Wakuu wa Idara katika Kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) Mkoani Ruvuma
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Jabir Shimweri katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Ruvuma kujadili maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.
Wajumbe wa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma.
Wananchi wametakiwa kutoa hamasa kwa watoto ili wapende kusoma masomo ya sayansi toka wakiwa katika Elimu ya Msingi na kuwawekewa Mazingira mazuri ya kusoma ili wapende sayayansi hali ambayo itasaidi siku zijazo kuondoa changamoto za upungufu wa Walimu wa Sayansi. Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma wakipokea maagizo ya utekelezaji wa Shughuli za maendeleo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na namna wanavyopaswa kusimamia utekelezaji huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Kilimo na kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa mapato kupitia Rasilimali za Utalii na Madini kwa maslahi ya wananchi wakishirikiana na Wakurugenzi wao. Wakuu hao wametakiwa kuchukua hatua dhidi ya viongozi wanaokiuka maadili ya kazi kwa kupelekea kukwama kwa shughuli yoyote ya maendeleo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia miongozo na mikakati katika kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo ulinzi wa mali na usalama wa Raia.
Wajumbe wa Kikao cha kamati ya Ushauri Mkoa wa Ruvuma wameomba Serikali kusimamia suala la Malipo ya wakandarasi wa Maghala ya kuhifadhi chakula hususani ghala la Halmashauri ya wilaya ya Madaba ambalo ujenzi wake umekamilika na tayari limeshaanza kutumiwa katika msimu wa Kilimo wa 2014/2015.
Sekretarieti katika Kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma wameomba wadau kuchangamkia fursa zilizopo za Maendeleo ikiwemo uhifadhi wa Misitu na Mabenki ya Biashara katika kujileta maendeleo na kukuza Pato la kila mwananchi mmoja mmoja.
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Ruvuma.
Aidha katika Kikao cha Kamati ya Ushauri wameombwa wadau na wabunge wa mkoa wa Ruvuma kusimamia Maboresho ya Hospitali za Wilaya ili ziweze kutoa huduma bora na kupunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Wajumbe wameomba kuangalia upya vyama vya ushirika jinsi vinavyofanya kazi ili viendane na malengo yaliyokusudiwa ya kuboresha hali za wananchi kupitia kilimo na siyo kumdidimiza mwananchi.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya mkoa kutoka sekta zote za maeendeleo Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya katika Kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) Mkoa wa Ruvuma.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma wakichambua mada katika kikao cha Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Ruvuma wameomba ushirikiano toka kwa wadau wengine wa maendeleo pale inapohitajika kushirikiana katika utekelezaji ama utatuzi wa jambo fulani mfano Jeshi la polisi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha utalii wetu wa ndani unapewa nafasi kubwa kwa maslahi ya wananchi wa mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla pia kudumisha tamaduni zetu za asili kasma sehemu ya utalii.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Ruvuma wamesema ni lazima kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi kwa weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.