KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, September 21, 2016

KWA NINI AJALI ZINATOKEA MARA KWA MARA NA KUWEZA KUMALIZA WATU

Ni hivi juzi tu tuimeshuhudia watu kumi na mbili wakiwa wa mepoteza Maisha na wengine 30 kujeruhiwa baada ya Basi linye namba za usajili T429 DEU aina ya Zongtong liitwayo NEW FORCE  kupinduka na kusababisha ajali

Jee nikitu gani ambacho kina sababisha ajali kwa mda mrefu  ? Nimechunguza chazo cha ajali zinazo tokea nime baini kuwa Madereva ndio chanzo cha ajali wakichangia na kitu kinacho itwa Toch ambayo huangalia sipidi za magari

Kwa nini nimesema Madereva ni chanzo cha ajali Madereva hupeana tarifa kujua kuwa Trafiki yuko wapi Mwenye Tochi ikiisha julikana baada ya kupewa tarifa na Dereva Mwenzake ana jua eneo hili halina Asikari na kuanza  kukimbia kwa kasi ili kufidia dakika alizo chelewa kwa kuogopa  Asikari wa usalama barabarani

Jambo jingine ukiangalia usafiri kati ya Songea na Dar es salaam kuna mabasi zaidi ya 9 ambayo kila basi lina taka kupata wateje.Mwendo wa  mabasi hayoni  kilometa moja kwa dakika ili likitoka Songea kwenda Dar es salaam ili weze kuingia kati ya   saa mbili hadi saa tatu  usiku

kwa maana hiyo kila Dereva anataka kupata umarufu kwa kufika mapema. Ukiangalia Mmumiliki wa Super Fello Omary Omary yeye  ana mikakati  yake na wafanyakazi amesha waambia wafanyakazi wake ukikimbiza gari Trafiki aka kukamata fedha hiyo ya kulipa faini ita toka ita toka mfukoni mwako hivyo Madereva wana kuwa macho katika kuendesha  Mabasi na kuogopa kutumia posho zao jambo linalo salimisha Roho za Abiria .

Abilia mara zote wanashuhudia wakisikia  sauti zaMadereva  wakipeana tarifa kwa madereva walio nyuma ili kujua Asikari wa Usalama  Barabarani wapo maeneo gani ,Hapo ndipo linapo anza tatizo la kukimbiza mabasi ,Chaajabu ni kuwa hata kama Dereva ana kimbia sijaona hata siku moja abiria akisema Dereva punguza mwendo badala yake Abilia hulala usingizi na kusitukia ajali ikitokea au breki ikifun g"hafula Jambo ambalo watu hubaki kupiga kelele jambo ambalo halisaidii.

Sasa kwa kumalizia nasema Ajali nyingi zina tokea zina tokana na Madereva kufanya Mashindanoili   kwa kukimbiza magari ili kufika mapema kule unako kwenda.

Abiria waache kukaa kimya pale wanapo ona madereva wakikimbiza  magari .Lamuhimu ni kuwa  namba ambazo hutolewa kwaajili ya kutoa tarifa pale dereva anapo liuka taratibu za usalama Barabarani kwa kupiga simu kwa kamanda wa Polisi

No comments:

Post a Comment