MKuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge akiwa katika Chuo cha Ufundi VETA Mkoani Ruvuma akisoma na kupokea taarifa ya Utendaji wa kazi za Chuo cha Ufundi Songea.
Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge akiwa na uongozi wa juu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Songea kujadili changamoto zinazokikabili Chuo cha VETA ikiwemo ukosefu wa Mabweni na Ucheche wa wanafunzi wanaojiunga na Chuo hicho.
Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge akikagua Maeneo mbalimbali ya Chuo cha VETA akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo hicho Gideon Ole Lairambe.
Moja ya shughuli zinazofanywa na Vijana waliojiunga na Chuo cha Ufundi Stadi VETA ni kuendeleza Miradi ya Kilimo cha Bustani kwa kutengeneza mashine za kumwagilia maji zikiwa zinauzwa kwa thamani ya shilingi 30,000 kwa kila moja.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Songea Gideon Ole Lairambe akimtembeza Mkuu wa Mkoa kuendelea kukagua maeneo na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Chuo hicho.
Mwandishi wa Habari wa Jambo Leo akiendelea kuziba kamera ya Blog ya songeahabari katika Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma katika Chuo cha ufundi Stadi VETA Songea.
Wafanya kazi wa Chuo cha ufundi Stadi VETA ambao ni Wahandisi wakimsikiliza Mhandisi mwenzao Dkt binilith Satano Mahenge akiwataka kuongeza ujuzi katika vifaa vinavyotengenezwa chuoni hapo ili viwe na ubora na mtazao mzuri kuliko bidhaa zinazotengenezwa Nje ya Nchi.
Wahandisi wa Chuo cha Ufundi VETA Songea wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma jinsi ya kuongeza ubora chuo cha Veta kwa kuwapa mwongozo wa masomo ya ufundi kuwa sio lazima Mtoto ajifunze ufundi wa Magari na umeme, Mafunzo yote yanayotolewa VETA yanaweza kuongeza Ajira kwa vijana na kuongeza Uchumi kwa Nchi yetu ya Tanzania.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Songea Gideon Ole Lairambe akimuomba Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kusaidia kutafuta Ajira za Ufundi ili Vijana waweze kujifunza na kuweza kufanya kazi, jambo litakalosaidia kuongeza mapato katika Chuo cha Ufundi Stadi Songea.
Mhasibu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Eusebi Peter akisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa Dkt Binilith Mahenge kuhusu jinsi ya kukuza Mapato katika Chuo hicho cha Ufundi Stadi VETA Songea.
Wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Stadi Songea wakiendelea kusikiliza Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt binilithh Satano Mahenge .
Nao akina mama Wahandisi ambao wako katika kitengo cha Ushonaji, ususi wakisikiliza mbinu za uboreshaji wa Mavazi kwa kushona mitindo yenye kuwavutia wateja.
Wahandisi wanawake wenye fani za Computer na Type Writer wakipokea maagizo kutoka kwa mkuu wa m koa kuhusiana na kuendeleza Elimu ya TEHAMA ili iwasaidie wanafunzi wanaowafundisha.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge akikagua utengenezaji wa nguo aina ya Batiki iliyotengenezwa na wanachuo cha Ufundi Stadi VETA Songea. Mbele yake ni Mwenyekiti wa Chuo cha Ufundi.
No comments:
Post a Comment