Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiukabidhi Mwenhe wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge pamoja na Wakimbiza Mwenge kitaifa 6 wakiongozwa na Amour Hamad Amour.
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Njombe amesema Mwenge wa Uhuru
ukiwa Mkoani Ruvuma utazindua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kukagua
miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 11,998,633,922
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akianisha Miradi hiyo amesema Miradi 18 yenye
thamani ya shilingi 1,865,866,706 itafunguliwa miradi 20 yenye thamani
ya shilingi 5,239,260,020 itazinduliwa, miradi 17 yenye thamani ya shilingi
3,898 ,325 kuwekwa mawe ya msingi na miradi 16 ya thamani ya shilingi 995,412,000 itakaguliwa.
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuingia Mkoa wa Ruruma ulikimbizwa kilometa 1289 katika
Halimashauri 8 za Madaba, Manispaa ya Songea, Mbinga mjini, Nyasa, Mbinga Vijijini, Songea Vijijini, Namtumbo na Tunduru.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tayari kwa kuanza mbio zake katika Halmashauri ya Madaba.Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel akipokea Mwenge wa Uhuru ishara ya kuwa umekwishawasili kwenye Halmashauri za wilaya ya Songea kwa ajili ya kukagua miradi katika Halmashauri za Wilaya ya Songea.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Madaba uliweza kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa Saccos ya Mahanje, Mradi wa Maji, Mradi wa Shamba la Mahindi na kushindwa kuzindua Mradi wa Bwalo la Chakula la shule ya Msingi Mahanje kutokana na kutokidhi vigezo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamadi Amour ameupongeza Mradi wa Sacos ya Mahanje kwa
kuweza kuendesha vizuri sacos yao, amewaomba kutoa toa mashariti magumu kwa wananchi wanaokopeshwa ili huduma ya Saccos iwanufaishe wananchi wengi.
Meneja wa Sacoss ya Mahanje Halmashauri ya Madaba akitoa taarifa ya Mradi wa Sacoss kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ndugu Amour Hamad Amour
Mradi wa Bwalo la Chakula la Shule ya Msingi Mahanje uliwekwa jiwe la msingi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu
Aidha kiongozin wa mbio za Mwenge alikataa kuzindua mradi wa Bwalo la chakula katika Shule ya Msingi Mahanje uliogharimu kiasi cha shilingi milini 19 kutokana na kuonekana dalili za udanganyifu na kuwa mradi huo umechukua muda mrefu toka ulipowekewa jiwe la msingi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu
Wakiainisha sababu za kutofungua mradi huo katika halmashauri ya Madaba wakimbiza mwenge kitaifa walisema mradi huo unaonyesha umechelewa kutoa huduma kwa wanafunzi toka ulipozinduliwa na kuongeza jambo hilo linaonyesha kutowatendea haki wanafunzi kwa muda mrefu na kwamba hata kiwango cha ujenzi hakikuwa sahihi kwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa alisema lengo la Mwenge wa Uhuru ni kuzindua miradi yenye tija kwa wananchi ambayo itafuatiliwa na kuhakikisha kweli wananchi watapata huduma stahiki kwa maendeleo yao kulingana na mradi husika.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Manspaa ya Songea uliweza kuzindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi
miradi 10 ya maendeleo ikiwemo Mradi wa
maji Ruhuwiko, Mradi wa kiwanda cha maziwa Nane nane Msamala, Mradi wa madarasa Shule ya Msingi Tusiende mbali Mshangano,
Miradi mingine iliyokaguliwa katika Manispaa ya Songea ni pamoja na mradi wa mabwawa ya samaki mradi wa Kituo cha Afya Lilambo, Kuzindua Kituo cha madawa ya kulevya (UMAT) Mahenge, kukabidhi Hundi kwa vikundi vya wajasiliamali Vijana na wanawake Songea, kuweka jiwe la msingi la Daraja la Mugela na kutembelea shamba la mahindi la Ekari 10 Sinai Manispaa ya Songea.
Mwenge wa uhuru uliweza kukagua kituo cha UMATI ambacho kina hudumia watu walioathirika na madawa ya kulevya wapatao 208 wakiwemo wanawake 8 na wanaume 200,
katika tarifa iliyosomwa na Mratibu wa Masuala ya Madawa ya Kulevya Felista Kibona ilianisha wauza madawa 16 wamekamatwa na
watu 9 kesi zao zipo mahakamani na watu wawili wana tumikia kifungo baada ya
kupatikana na hatia
Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 ni Shiriki kikamilifu katika kukuza Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya Wananchi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo katika viwanja vya Mshangano stend ambapo ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kitaifa ulitolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa
wkimbiza Mwenge kitaifa wakishuhudia mapokezi ya wakaazi wa manispaa ya Songea waliojitokeza kwa wingi katika Viwanja vya kituo cha stend ya Daladala Mshangano
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa Bega kwa Bega na wakimbiza mwenge kitaifa kuhakikisha wanakuwa salama siku zote ambazo wanazunguka katika Halamashauri za wilaya ya Songea.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Amour HamAd Amour akizindua Mradi wa Madarasa 9 katika shule ya msingi Tusiende Mbali kata ya Mshangano iliyo jengwa kwa nguvu za wananchi kwa asilimia 80% na serikali kuchangia 20% kwa garama ya shilingi milioni 32 ameupongeza mradi huo na kusema unalenga kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa vijana watakaosoma shuleni hapo
Amour amesema kuboresha miundo mbinu ya kusomea ni dhahiri kuwa tunaandaa vijana wetu ambao watakuja kusaidia baadaye, amewasifu wazazi kwa kujenga shule bora ya kisasa na kusema mtoto akisoma katika mazingira mazuri ni tutegemee kupata watalamu watakao simamia viwanda katika taifa hili.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru akiwa Manispaa ya Songea aliweza kugawa Neti kwa Wazee.
Kiongozi wa mbio za
mwenge kitaifa amewasa wazazi kuzingatia elimu kwa kuwasomesha watoto wao na kufuata vigezo vyote vya Elimu ili mtoto apate elimu bora ikiwemo kuwa na
madarasa bora ya kusomea
Viongozi wa Manispaa ya Songea wakihakikisha Usalama wa Mwenge wa Uhuru kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama
Mwenge wa Uhuru uliweza kuzindua Mradi wa Kiwanda cha Maziwa na kusema dhana ya uanzishaji wa Viwanda isitafsiriwe kuwa ni lazima kumiliki kiwanda kikubwa bali ni namna unavyoweza kuyapa thamani mazao yako yakaweza kuuzika kwa bei yenye tija.
Wananchi waliojitokeza kushiriki katika mbio za Mwenge wa Uhuru wamepongeza Viongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa kupitia kwa makini miradi inayozinduliwa.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luhira Manispaa ya Songea waliojitokeza kushuhudia Mwenge wa Uhuru
Mradi wa Mabwawa ya Samaki uliokaguliwa na Mwenge wa Uhuru kitaifa
Mradi wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa Uliopo Msamala Manispaa ya Songea
Mwenge wa Uhuru 2017 katika Manispaa ya Songea umeizindua miradi 10 katika iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 897miradi
No comments:
Post a Comment