Wananchi wanao ishi katika mwambao
wa ziwa Nyasa wametakiwa kuacha mtindo wa kuchafua mazingira kwa kuoshea Magari,Pikipiki,pamoja
na kufua nguo huko ni kuhatarisha maisha ya viumbe wa kiwemo sa maki kwa kula
sumu na sumu hiyo inaweza kuwa dhuru watu baada ya kula samaki wenye sumu
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi
Binilithi Satano Mahenge ameyasema hayo wakati wa kufanya usafi mwambao wa
zaiwa nyasa wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma kiatika kuadhimisha siku
ya mazingira Duniani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilithi Satano
Mahenge amesema kufanya usafi mwambao wa ziwa nyasa ni kujiwekea utajili
mara wakifika watalii kutembelea ufukwe huo wa ziwa nyasaMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge amesema wananchi wakiimarisha usafi katika Ufukwe wa Ziwa Nyasa wata weza kuwafanya watalii watakao kuja kuweza kuwa shawishi watalii wengine kuja Mwambao wa ziwa jambo ambalo lita kuza uchumi katika Wilaya Nyasa Mkoani Ruvuma Tanzania pia litawezesha kuingiza fedha za kigeni.
Mkuu wa kituo cha Police Wilaya ya Nyasa
ambaye alishiriki katika usafi amesema jeshi la police kazi yake ni kusimamia
sheria itahakikisha ufukwe wa ziwa Nyasa unakuwa safi yeyote atakaye vunja
kanuni za usafi sheria itachukua mkondo wake.
Zoezi la Usafi wa Mazingira likiendelea likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika fukwe za Ziwa Nyasa.Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema amefarijika sana kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kushiriki pamoja na wananchi wa wilaya ya Nyasa katika shughuli za usafi wa Mazingira ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kuhifadhi mazingira na kuyaweka safi daima.
Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa akiendelea na zoezi la usafi wa Mazingira katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira ambayo wakaazi wa Wilaya ya Nyasa waliadhimisha kwa kufanya usafi kwenye fukwe zinazozunguka Ziwa Nyasa.
Nao wanafunzi walio hojiana na RFA
wameahidi kufanya usafi wa Mazingira na kuboresha club ya Mazingira wanachohitaji ni ufadhili wa vitendea kazi kutoka kwa wadau na viongozi mbalimbali pichani Nemia James akifanya usafi mwambao wa Ziwa nyasa.
Mwansshi wa Star TV na mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari Bw. Adam Nindi akiwa katika hoteli ya Masisita Mbamba Bay katika kufuatilia hali ya Uhifadhi na usafi wa Mazingira yanayozunguka mwambao wa Ziwa Nyasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akiwa katika Hosteli ya Masista iliyoko Mbamba Bay mara baada ya shughuli za Usafi wa Mazingira, kulia ni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Nyasa Mr Mbambe
Wananchi walioshiriki katika kufanya usafi maeneo ya fukwe za Ziwa Nyasa wameahidi kuwa walinzi katika fukwe hizo ili kuhakikisha zinavutia wageni kuja kutalii.
Katika kuazimisha siku ya Mazingira wilaya ya Nyasa iliadhimisha kwa kufanya usafi kwenye fukwe za Ziwa Nyasa chini ya Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge na wadau wengine wa Mazingira.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma
Mhandisi Binilithi Satano Mahenge akiwa wilaya ya Nyasa amevunja
kamati ya usimamizi wa usafi Mbambabay baada ya wajumbe wake kuto
hudhuria katika usafi pamoja na kushindwa kuwa baini wanao vua samaki kwa
kutumia Gonga au njia ya Baruti
No comments:
Post a Comment