Dr Binilith Satano Mahenge, akipokea tarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shamba la Aviv
Mkurugenzi
wa AVIV Meda Medppa amesema anaishukuru kuona wananchi wanao zunguka kampuni
wanalima kahawa na kwa mwaka huvuna tani 20,000 nakulipwa kwa kilo shilingi
3500
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge
amesema ili kuongeza ajira katika Mkoa wa Ruvuma pamoja na Kampuni ya AVIVI kuajiri wafanyakazi 1800 swala hilo halitoshi
. jambo la msingi ni kuhakikisha kampuni ya Avivi ina jenga kiwanda cha
kusindika kahawa mkoani Ruvuma ili kutangaza jina la Tanzania pale itakapo onekana
lebo ya kahawa ya mkoa waruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith
Mahenge ameitaka Kampuni ya AVIVI inayofanya shughuli za Kilimo cha Kahawa
wakiwa wana miliki shamba lenye ukubwa
wa hekita 1900 ambapo kwa mwaka huvuna
tani 1200 wanauwezo wa kujenga kiwanda cha kusindika kahawa jambo litakalo weza
kuifahamisha Ruvuma Ijulikane kwa kuweka
lebo ya usindikaji kahawa kutoka Mkoa wa Ruvuma
Shamba la
Kahawa la Kampuni ya AVIVI linahudumia vijiji 19 vinavyozunguka shamba hilo
ambapo mwaka jana wana kijiji waliweza kuuza Tani 20 za Kahawa na Wananchi 120
kupata Ajira kwenye Mtambo wa kukoboa Kahawa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge akikagua utendaji wa kiwanda cha kukoboa kahawa kikiwa na uwezo wa kukoboa tani mbili kwa siku
Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya AVIVI Frola Hauko amewaomba wananchi wanaozunguka Shamba la
AVIVI kuchangamkia fursa za kuweza kulima Kahawa kwa kuwa Soko lipo. Naye Bwana
shamba wa Shamba la Kahawa Hamuza Kasimu amesema Shammba la Kahawa la Kampuni ya AVIVI
mwaka huu lina tarajia kuvuna tani 1200
Mkurugenzi wa Aviv akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge katika kiwanda cha kukoboa Kahawa Eneo la Lipokela
Mmoja wa Viongozi katika shamba la kahawa la Aviv katika eneo la Lipokela
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akionyehswa kahawa inayo zalishwa na Kampuni ya Aviv
Eneo la kusafisha kahawa katika kiwanda cha kukoboa kahawa
W3atalamu wa ufungaji umeme wakitoa Tarifa ya kutekeleza kauri ya Waziri Mkuu ya kutoa Umeme katika Kampuni ya Aviv
No comments:
Post a Comment