Mhashamu ASkofu Mkuu
wa kanisa la Redeemed Assemblies of God Tanzania amewataka waumini wa dini ya
kikrsito kumkimbilia Mungu ili kuweza kukabiliana na mambo ya ufisadi na
Dhuluma inayofanywa na watu wasio mwogopa Mungu.
Mhashamu Askofu Mkuu wa kanisa la Redeemed Asemblies of
God Simon Kisote Silumba ameyasema hayo katika ibada ya kusherekea sikukuu ya Crismas Mkoani RUVUMA, Amesema ili viongozi waweze kuwa waadilifu wanatakiwa kuachana vitendo vya kudhulumu mali ya wanyonge
Naye Mhashamu Asikofu wa KKT Dayosis ya Ruvuma Amon John Mwenda amewataka waumini
katika kukabiliana na hali ya uchumi wajikite katika kufanya kazi zilizo halali.
Mchungaji wa kanisa la Angilikani Erasto Haule amewaomba waumini kutokata tamaa katika maisha wategemee nguvu za Mungu Waepukane na viongozi wanao zingatia Rushwa.
Vijana waumini wa dini ya kikristo wameomba waumini wa dini
ya kikristo kupingana na vitendo vya Rushwa.
Vijana wametakiwa
kuwa mfano katika Jamii kwa kuzingatia Mila na Desturi za kitanzania kwa kusimamia usafi katika
Maeneo yao na kuheshimu wakubwa wanaowazidi umri.
Katika kuendeleza Maadili mema kwa wanawake wametakiwa kujiandaa kuwa viongozi wa Familia siku za baadaye huku wakimtanguliza Mungu
Mchungaji wa kanisa la REDEEMED Asemblies of God Hilda Silumba amewataka vijana wava e mavazi yenye heshima.
Mkoa wa Ruvuma umesherehekea kwa usalama Sikukuu ya Krismas 2017 hasa kwa kuzingatia suala la Ulinzi wa Watoto kutowaacha peke yao, wazazi walio wengi wameonekana wakiambatana na watoto wao.
No comments:
Post a Comment