Wanaume Mkoani Ruvuma wametakiwa kujitokelza ili
kuuelezea Ukatili wanaofanyiwa na wake zao, imeelezwa siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia
zinaihusu jamii Nzima ikiwemo wanawake wanaume na watoto.
Mgeni rasmi katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Ruvuma Mkurugenzi wa AICIL amesema wanawake huwatesa wanaume kwa kisingizio cha usawa wa kijinsiawa asilimia 50% kwa 50% amesema huo sio usawa uliolengwa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Ruvuma Renatus Mkude
amewaomba wananchi kutoa maoni ya Marekebisho ya Sheria ambazo zitasaidia
kutokomeza Ukatili wa Kijinsia miongoni mwa jamii.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la Msaada wa Kisheria AICIL Agness Haule akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kukimbiza kuku Mtoto Rehema Kassim katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Jinsia na watoto zilizofanyika katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma
Wajumbe wa dawati la Jinsia na watoto wa Mkoa wa Ruvuma wakifurahia kufanikisha maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka 2017 chini ya Usimamizi wa Mwenyekiti wa Dawati hilo Anna Tembo .
Watoto wakiburudika na sanaa mbalimbali katika maadhimisho hayo
Wajumbe wa Dawati waliohudhuria Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia mwaka 2017, kulia ni Diwani wa Viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA.
Mjumbe wa Dawati la Jinsia mkoani Ruvuma ambaye pia ni Askari Salumu akipokea zawadi kwa mgeni Rasmi kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya Maadalizi ya Sherehe za Siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia baada ya kushinda katika mchezo wa kuvuta kamba.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa Jinsia na watoto Mkurugenzi wa AICIL Agness Haule akitazamabaadhi ya picha zinazoonyesha vitendo vya ukatili waliofanyiwa watu mbalimbali katika Banda la Dawati la Jinsia wakati Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Fadhila Chacha akitoa Maelezo ya Kesi wanazokutana nazo na aina ya ukatili unaojitokeza mara kwa mara ikiwemo wamama kuwachoma moto watoto, kuwachapa watoto kupita kiasia na baadhi ya wanawake kuwamwagia maji ya moto waume zao na waume kuwajeruhi wake zao.
Kikundi cha Ngoma ya asili almaarufu Lizombe kutoka Lizaboni Manispaa ya Songea wakitoa ujumbe wa haki za mtoto kwa njia ya burudani wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa Jinsia na watoto.
Wadau wa Kupinga Vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye uwanja wa Majimaji Mkoani Ruvuma.
Katika Kuadhimisha Kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Jinsia na watoto Mkoani Ruvuma Dawati la jinsia liliwezesha kutoa Elimu kwa wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma kwa njia za ngoma za asili, vyombo vya habari, katika mikutano ya hadhara na kutembelea shule za msingi na sekondari kuelimisha wanafunzi.
Watoto wakijipanga kuanza zoezi la kukimbiza kuku ikiwa sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Mkoani Ruvuma.
Watoto nao wana nafasi yao katika jamii pia wana haki ya kusikilizwa na kutoa maoni, watoto wakiwa katika maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea katika maadhimisho hayo watoto walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali na kusikiliza hotuba za viongozi mbalimbali juu ya ustawi wa mtoto.
No comments:
Post a Comment