Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania imetoa
msaada wa madawati 500 kwenye Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma yakiwa na thamani ya shilingi milioni kumi na
tano[15,000,000/=
Msaada huo unatokana na sehemu ya mapato wanayoyapata katika Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari ikiwa ni utaratibu waliojiwekea kurudisha sehemu
ya faida kwa jamii inayowazunguka kwa kuchagia shughuli za Maendeleo kwa
kijamii. Wanafunzi wa Sekondari ya Mbamba Bay wakiwawakilisha wanafunzi wenzao waliopokea msaada wa Madawati hayo wameishukuru Mamlaka ya usimamizi wa Bandari kwa kuona umuhimu wa kusaidia katika Sekta ya Elimu kwa kuwa kufanya hivyo kutawafanya wao waongeze hario ya kujifunza.
Shule ya Sekondari ya Mbamba Bay ni miongoni mwa shule zilizonufaika na msaada wa Madawati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kupitia bandari ya Mbamba Bay ambayo inapatikana Halmashauri ya wilaya ya Nyasa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbamba Bay
Wanafunzi wa Sekondari ya Mbamba Bay halmashauri ya wilaya ya Nyasa wameishukuru serikali kwa kuwajali katika kuimarisha miundombinu ya shule na vifaa vya kujifunzia wameomba wazazi na walezi kuongeza hari ya kusomesha watoto.
Maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari wakishuhudia tukio la kukabidhi Madawati katika Shule ya Sekondari ya Mbamba Bay.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania Francisca kajumulo amesema ili kuboresha elimu katika sekondari ya Mbambabay na kupatata wasomi wazuri nilazima kujenga mazingiura mazuri kwa
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Francisca Kajumulo Urio amesema ili kuboresha
elimu katika Sekondari ya Mbambabay na kupatata wasomi wazuri ni lazima kujenga
mazingiura mazuri kwa wanafunzi Mamulaka
ya Usimamizi wa Bandari imeamua kutoa msaada wa madawatiu 500 na kuahidi kutoa
zawadi kwa wanafunzi watakao pata daraja la kwanza katika mitihani ya kidato cha sita na kidato cha nne.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa
Isabela Chilumba amewaasa wanafunzi kuachana na maswala ya ngono uzembe ili
waweze kumaliza masomo yao na kuweza kujenga nchi yao hapo baadaye, Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema wilaya ya nyasa kwa sasa ina ziada ya madawati
500 kwa SMekondari na 400 kwa shule za msingi
Meneja wa Bandari ya Nyasa na Itungi kyela Bw. Ajuaye Msese ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii ya wakazi wa mwambao wa Ziwa Nyasa.
Wanafunzi wa shule ya Secondary ya Mbambabay wakipokea msaada wa Madawati hayo kwa niaba ya wenzao wa shule zingine wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuweka mikakati mizuri ya kuboresha elimuNchini.
Kaimu Mkurungenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania amesema Serikali kwa sasa ina jenga meli yenye uwezo wa
kuchukua abiria 200 na mizigo tani 200 jambo litakalo punguza changamoto ya
usafiri kwa watanzania na nchi jirani za
Malawi na Msumbiji
Wafunzi wakiongozwa na Janet Mgaya wameshukuru kwa
msaada wa madawati, nao wavulana wameiomba Serikali kuwajengea mabweni ili wakati wa usiku
waweze kujisomea wakiwa shuleni kama ilivyoboresha mabweni ya wasichana.
Wanafunzi wa Sekondari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma wakifurahi pamoja na Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari baada ya kuwakabidhi Madawati.Wanafunzi hao pamoja na kupokea msaada wa Madawati wamesema wanasikitishwa kuona wanafunzi wanaotoka maeneo ya Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wanakuwa na mwamko mdogo wa elimu tofauti na wale wanaokuja kutoka mikoa ya Nje ya Ruvuma.
Wanafunzi wameomba wazazi kuhimiza watoto wao wasome kwa bidii kwa kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya Elimu shuleni hapo ni aibu kuona wenyeji wanashindwa kunufaika na uwekezaji huo kwa kuwaacha wageni wakisoma kwa bidii.
Hayo ni baadhi ya Majengo ambayo yamejengwa kwa ustadi wa hali ya juu yanayopatikana katika Sekondari ya Mbamba Bay wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Jengo linaloonekana ni Hosteli ya Ghorofa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 200 jambo ambalo linawafanya wanafunzi wakiwa shuleni hapo kuongeza hamasa ya kusoma kwa bidii kutokana na kuwepo kwa makazi bora.
Mwonekano wa Jengo la Bweni la wasichana katika Sekondari ya Mbamba Bay.
Hosteli yenye hadhi ya chuo Kikuu inapatikana katika sekondari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa kinachotarajiwa ni kuwa watoto wa shule hii watalipa fadhila kwa kuongoza katika ufaulu kutokana na uwepo wa miundombinu imara ya shule.
Pamoja na Maboresho ya Majengo lakini pia shule hii ina bahati ya kuwa na vifaa vya Maabara.
Maabara ya Masomo ya sayansi ikiwa imesheheni vifaa kama inavyoonekana piachani
Vifaa kama hivyo vya Maaabara vinapatikana kwenye shule chache hivyo hakuna sababu kwa wanafunzi wanaotoka katika shule ya Mbamba Bay kushindwa kufikia malengo wanapokuwa shuleni jambo la msingi ni kuachana na mambo yasiyo na umuhimu kwa wakati wanapokuwa shule.
Hili ni moja ya Madarasa ambayo yanapatikana katika shule hiyo ambayo inadhihirisha kuwa Elimu bora inapatikana kokote kinachotakiwa ni wanafunzi kujituma katika masomo. |
No comments:
Post a Comment