KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, September 12, 2011

HARAKATI ZA TGNP JIJINI DAR - ES - SALAAM

wandishi wa habari wakiwa katika viwanja vya TGNP Jijini Dae - es - Salaam aliye vaa tisheti nyekundu ni mkugugenzi wa mipango TGNP kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania Liliana Liundi

Mkurugenzi wa TAMWA Ananilea Nkya akiongea na wandishi wa Habari kutoka mikoa ya Tanzania bara Wandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mkutano na mkurugenzi wa TAMWA Nchini Tanzania katika ukumbi wa TGNP Dar - es - salaam



mwandishi wa habari wa Uhuru FM Juma Nyumayo kutoka Mkoa wa Ruvuma akibadirishana Mawazo na Doto kutoka Mwanza wakati wa Tamasha la Wanawake linalo shirikisha watu zaidi 2500 kutoka Zambia,Kenya, Burundi,Rwanda, Uganda,Ghana ,Africa kusini,Marecani na Ufaransa

WARSHA YA TGNP LEO

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika warsha ya mafunzo

Waandishi wa habari wa nyanda za juu kusini waliopo katika mtandao wa TGNP wakiwa katika viwanja vya TGNP jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Tamasha la jinsia kuanzia Septemba 13 hadi 16 .

Sunday, September 11, 2011









Unapo safiri na Basi la Super Fello una pata vitu vya kujiburubisha kila mmoja kwenye kiti chake anakuwa na TV anayo imiliki kutoka kushoto ni Adamu Nindi akiangalilia TV na upande wa kulia mwandishi stive Mango akielekezwa stesheni mbalimbali zinazo patikana katika mtandao wa Super Felo Bus.

Saturday, September 10, 2011








Hiyo ndiyo hali halisi inavyo onyesha mahindi yalivyo shonana mda simrefu kuta kuwa hakuna sehemu ya kuweka













Uwanja wa Zimanimoto katika manspaa ya songea ambao hutumika kwa michezo mbalimbali mwaka huu umetoa mpya baada ya kuwa ghala la hifadhi ya kitengo cha chakula ,uwanja umeanza kuelemewa baada ya mahindi kufurika katika uwanja huo , Hiyo imetokana na usimamizi mzuri wa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Cristina Ishengoma kusimamia kilimo.

Friday, September 9, 2011



YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruhuwiko Shule inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania, amesema Mwanafunzi atayeshindwa kufanya vizuri katika Mtihani wa Kidaro cha Pili atakuwa hana nafasi katika Shule yake.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ruhuwiko Manispaa ya Songea Paulo J. Rugwaguza ameyasema hayo katika Mahafali ya kuwaaga wanafunzi wanaohitimu Kidato cha Nne mwaka huu .

Mwalimu Mkuu Rugwaguza amesema Kamati ya Shule ambayo ili shirikiana na Wazazi katika kikao kilicho keti wa Mwezi Juni Mwaka huu kiliamua kuweka mikakati ya kuinua Elimu katika Sekondari ya Ruhuwiko .Akitoa mrejesho wa Mwaka 2009 matokeo yalivyo kuwa amesema hali ilikuwa mbaya Wanafunzi waliopata Divisheni IV walikuwa 54, Divisheni III – 11, Divisheni II walikuwa 3 na Divisheni I alikuwa mmoja kutokana na hali hiyo Kamati iliadhimia kuangalia Upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili.

Mlezi wa Shule ya Ruhuwiko Canal. John Chacha amewataka Wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii.

Aidha Mlezi wa shule ya Ruhuwiko Sekondari amewashukuru wazazi wanaolipa ada kwa wakati pia amewahimiza wazazi wasiolipa ada kwa wakati wanawakosesha watoto Maendeleo katika kujipatia Elimu.

Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Kitengo cha Hifadhi ya Chakula Mkoa wa Ruvuma Mogan Mwaipyana amewataka wahitimu katika kumaliza kwao wazingatie sana Utaifa wa Tanzania.

Amewataka Wanafunzi kujitahidi katika Masomo ya Sayansi, ameushukuru Uongozi wa shule kwa kuongeza Kompyuta amesisitiza kuwa mtu asiye jua Compyuta ni sawa na mtu aseye soma kabisa.

Wazazi walioongea na MTANDAO WA YALIYOJIRI MKOANI RUVUMA wamewataka wanafunzi kuachana na mambo ya starehe waache Ngono uzembe, wakishindwa kwa kila kitu warudi kwenye Jembe la Mkono.

Jumla ya Wahitimu 186 wameweza kuhitimu kidato cha Nne, kazi iliyobaki hivi sasa ni kufanya vizuri katika Mtihani wao ulioko mbele yao.

Wanafunzi wameiomba Serikali kuongeza Vitabu vya Sayansi katika Shule, pia kuangalia suala la Umeme Shuleni, inachukua gharama kubwa kununua Mafuta.
Watu wavipaza sauti ambao walisimamisha shuguli za maafali kwa takiribani saa moja baada ya vipaza sauti kushindwa kwenda na wakati , hatimaye kumwita mshauri wa mgambo mkoa ambaye alikuja kuokoa jahaz










kushoto wapiga picha wakihangaika kupata matukio mbalimbali ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya secondary ya Luhuwiko manspaa ya Songea,kulia ni walimu wa secondary ya Luhuwiko wa kibadilishana mawazo kuhusu maafali ya shule yao.