KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, September 9, 2011



YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruhuwiko Shule inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania, amesema Mwanafunzi atayeshindwa kufanya vizuri katika Mtihani wa Kidaro cha Pili atakuwa hana nafasi katika Shule yake.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ruhuwiko Manispaa ya Songea Paulo J. Rugwaguza ameyasema hayo katika Mahafali ya kuwaaga wanafunzi wanaohitimu Kidato cha Nne mwaka huu .

Mwalimu Mkuu Rugwaguza amesema Kamati ya Shule ambayo ili shirikiana na Wazazi katika kikao kilicho keti wa Mwezi Juni Mwaka huu kiliamua kuweka mikakati ya kuinua Elimu katika Sekondari ya Ruhuwiko .Akitoa mrejesho wa Mwaka 2009 matokeo yalivyo kuwa amesema hali ilikuwa mbaya Wanafunzi waliopata Divisheni IV walikuwa 54, Divisheni III – 11, Divisheni II walikuwa 3 na Divisheni I alikuwa mmoja kutokana na hali hiyo Kamati iliadhimia kuangalia Upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili.

Mlezi wa Shule ya Ruhuwiko Canal. John Chacha amewataka Wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii.

Aidha Mlezi wa shule ya Ruhuwiko Sekondari amewashukuru wazazi wanaolipa ada kwa wakati pia amewahimiza wazazi wasiolipa ada kwa wakati wanawakosesha watoto Maendeleo katika kujipatia Elimu.

Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Kitengo cha Hifadhi ya Chakula Mkoa wa Ruvuma Mogan Mwaipyana amewataka wahitimu katika kumaliza kwao wazingatie sana Utaifa wa Tanzania.

Amewataka Wanafunzi kujitahidi katika Masomo ya Sayansi, ameushukuru Uongozi wa shule kwa kuongeza Kompyuta amesisitiza kuwa mtu asiye jua Compyuta ni sawa na mtu aseye soma kabisa.

Wazazi walioongea na MTANDAO WA YALIYOJIRI MKOANI RUVUMA wamewataka wanafunzi kuachana na mambo ya starehe waache Ngono uzembe, wakishindwa kwa kila kitu warudi kwenye Jembe la Mkono.

Jumla ya Wahitimu 186 wameweza kuhitimu kidato cha Nne, kazi iliyobaki hivi sasa ni kufanya vizuri katika Mtihani wao ulioko mbele yao.

Wanafunzi wameiomba Serikali kuongeza Vitabu vya Sayansi katika Shule, pia kuangalia suala la Umeme Shuleni, inachukua gharama kubwa kununua Mafuta.

No comments:

Post a Comment