KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, October 2, 2012

KUKAA KIMYA KWA WANDISHI WA HABARI KWA SABABISHA ONGEZEKO LA UHALIFU

 Hii ni ajali iliyotokea kilometa 30 kutoka Iringa Mjini wakati Magari matatu yalipogongana na kusababisha Gari la Supper Feo linalotoka Iringa kwenda Songea kubonyea kwa nyuma, ndani ya Basi hilo kulikuwepo na Mkongwe wa habari Adam Nindi ambaye alikuwa Iringa kikazi.
 Moja ya maboresho ni Serikali pale inapotoa elimu kwa waendesha pikipiki na Magari ili kupunguza Ajali za Barabarani, katika picha hii Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Mh Said Thabit Mwambungu aliweza kutoa vyeti kwa waendesha pikipiki wapatao 240 katika uwanja wa Majimaji baada ya kuhitimu Mafunzo ya kuendesha pikipiki kwa usalama kupitia Chuo chs mafunzo ya Ufundi VETA Mkoa wa Ruvuma
 Ili kupunguza ajali pikipiki zote zinazoingia barabarani zinatakiwa kukaguliwa kuhakikisha ziko salama na haziwezi kusababisha ajali zikiwa barabarani
 Madereva wanatakiwa kuwa waangalifu na kuweza kuzifahamu alama za usalama Barabarani, Dereva asipofuata kanuni za Usalama Barabarani matokeo yake ni kusababisha ajali. Hebu angalia Barabara ilivyo alama zote zinaonekana ili kumsaidia dereva apite vizuri.
 Ufikapo katika Mji wa Iringa ili uwe na Uhakika wa usalama wako kwa kuepuka kuibiwa au kuuweka mwili wako katika afya nzuri ni bora kufikia NICK MOTEL ambapo pana ulinzi wa uhakika na chakula kizuri. Picha ya hapo juu ni Mkongwe wa habari Adam Nindi akipata kifungua kinywa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Hoteli ya NICK MOTEL.
 Mtandao ambao unawasaidia Watanzania kwa kupunguza maumivu ya gharama za mawasiliano ni Air tel hapo watu mbalimbali wakichukua fedha zao kupitia Air tel Money
Kwa kipindi kifupi kilichopita Waandishi wa Habari walisusia kuandika habari za kipolisi, utafiti uliofanywa na Blog hii umebaini kuwa kwa asilimia kubwa wahalifu wamefurahi kuona makosa wanayoyafanya hayaripotiwi pamoja na hayo hata ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka na wananchi kukosa huduma muhimu ya kujua kinachoendelea na kusababisha watu ambao wanapenda uvunjifu wa amani kujiweka katika kivuli cha kuunga mkono Mgomo wa Waandishi wa Habari huku wakijua ni moja ya kumkosesha mwananchi haki ya msingi ya kikatiba ya kupata habari.

Pamoja na hayo Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma walipata joto la jiwe baada ya wao kuibiwa Vifaa vyao na vibaka na hatimaye Jeshi la polisi kuwasaidia kuwapata wahalifu ambao wamefikishwa kwenye chombo cha Dola ambachi ni mahakama lakini kwa aibu habari hiyo haijaandikwa popote pale, Je hii imekula kwa wanahabari au kwa Polisi? ni vizuri vyombo vinavyohusika kuangalia kwa makini suala lililosababisha mgomo wa Waandishi wa Habari. Pichani juu Jeshi la Polisi linaonyesha likiendelea kutoa huduma kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment