KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, January 18, 2013

UCHAWI NIMOJA YA FANI KWA JAMII FULANI .TUFANYEJE ILI KUWARUDISHA KWETU



Ndugu zangu wasomaji wa Blog ya Songea Habari napenda kuwapongeza kwa mwaka 2012 kwa kutoa ushirikiano wa kuweza kuchangia katika Masuala yanayohusu jamii hasa jamii inayoishi pembezoni mwa Nchi na kuonyesha changamoto zinazowakabili.

Kwa habari za kina nilikuwa nikiifahamisha Jamii kwa kitu kinachoitwa uchawi ambacho ndicho changamoto kwa watu wanaoishi pembezoni.

Watu walio wengi huingiwa na hofu kufanya Maendeleo kwa kile kinachoitwa woga wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

                 Mganga wa jadi bint Frola Ndembo
Nikiwa katika kambi ya Mganga mashuhuri wa Nyanda za juu Kusini Mama Binti Flora Ndembo nimeweza kupata siri kubwa kuhusu uchawi. Wachawi wenyewe wamesema wamejiingiza katika uchawi baada ya kuona Jamii ikiwatenga, wale ambao ambao hawana uchumi wa kutosha ndio wanaunda umoja wa kuwatesa wenzao.
Add caption


Mkuu wa Wachawi kutoka Mwambao wa Ziwa Nyasa akiwa amesimama akieleza Jinsi alivyojiingiza katika Uchawi. Mguu unao uona wa kulia uliovimba kama Rungu, huo Mguu ni gia ya kupaa angani akigonga na Mguu wa kushoto ndipo huanza kuruka akielekea eneo alilo panga.

Tu kiachana na Mchawi mkuu wa Mwambao wa Ziwa Nyasa sasa tuangalie mchawi  wa Matimila Songea Vijijini ambaye alimua mtoto wake ambaye alikuwa Padiri akitangaza kujitoa katika Uchawi  amesema ameamua kujitoa baada ya wachawi wenzie kumuua mtoto wake ambaye alifikia ngazi ya kuwa Askofu; hapo ndipo alipoona kuwa uchawi hauna maana.

Nikiwa mchambuzi wa habari za ushirikina  niliamua kumuulizaa mzee kuwa mtoto wake ambaye alikuwa mtu wa Mungu aliwezaje kuuwawa wakati yeye ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wachawi. Alijibu hakuna mtu anayeweza kuuwa katika ukoo kama ndugu hajaidhinisha na sheria hiyo hufuatwa kwa makini ukikiuka taratibu unauwawa mwenyewe “ndivyo ilivyonikuta kwa mototo wangu

 
Nikiwa katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake kuweka rehani mwili wake baada
wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Nikiwa bado katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo, nilitiwa na fadhaha baada ya kumuona Binti mwenye umri wa miaka 10 aliyepewa uchawi na Mama yake na kuweza kupewa mboga ya akiba ambacho ni kidonda kilicho ubavuni ambacho yeye alikiri kuwa akikosa mboga hutumia kwa kuchovya kwenye kidonda. Maskini Binti huyo katika maisha yake hadi kufikia miaka hiyo 10 alikuwa akichukia shule kama nini lakini baada ya kufika kwa Binti Ndembo ameacha uchawi na kuomba akaendelee na Masomo

Kamanda wa POLICE aliye hamia Iringa Maiko Kamhanda kushotona Kamanda Mpya Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki
 Ndugu yangu nikiwa katika kambi hiyo na Binti Ndembo nimeona mambo mengi cha kufurahisha mganga huyo hana uchochezi. Yeye amekuwa akipatanisha ndugu hao na kuwa Jamii moja. Nikiwa Kambini hapo nimeshuhudia Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akitoa elimu Shirikishi kwa kutaka Jamii iachane na Mambo ya Ushirikina.

Mganga huyo mashuhuri mbali ya kutibu watu wenye asili ya Ushirikina lakini hata hivyo ameshaweza kukamata Majambazi Sugu, na wao kusalimisha silaha zao na kuachana na Ujambazi.

Jambo la kuingilia Masuala ya Ujambazi, Mganga huyo mashuhuri amepata misukosuko kwa kuwahi kupigwa risasi mbili na kukimbizwa Hospitali ambako alitolewa.

Amewahi kufungwa Kamba na kutupwa msituni na kuambiwa aachane na masuala ya kufuata Majambazi lakini uganga wake uliweza kumwokoa.

Pia kwa Mara ya Kwanza Mganga huyo aliweza kubainisha ndoa iliyofungwa kati ya Mama na Mtoto wake wa kuzaa mwenyewe. Hatimaye aliweza kuibainisha Ndoa hiyo hadharani.

   Ndugu zangu wasomaji, Shabaha yangu ni kutaka kuendelea kupata mawazo kutoka kwenu, kitu kikubwa ambacho kinasababisha Maendeleo kuto chukua Kasi ni Kushiriki katika Mambo ya Ushirikina.   Sasa hapa tumeona watu walio wengi wakiacha Uchawi na kutangaza Hadharani.

  Hii ni Ruvuma Jee Mikoa mingine Ukombozi utatoka wapi?
 Wasomi na watu wenye Vipaji watume Elimu yao kuutokomeza Ushirikina na wale wenye Ushirikina wajitoe Hadharani kuachana na USHIRIKINA.   




Friday, January 11, 2013

Nijambo la kushukuru Jeshi la POLICE Mkoa wa Ruvuma kwa kuweza kutambua mchango unao tolelewa na waandishiwa wa Habari katika kukemea vitendo viovu vya unyanyasajiwa kijinsia kwa watoto nawanawake.Hii inatia moyo kwa kusamini michango yawaandishi.

KwaMfano kazi kubwa iliyofanywa na mwandishi waHabariwa StarTv kuifahamisha Serekari kuzima motouliokuwa ukiunguzamaakaayamawe  yaRwanda wilayan iMbinga  na sasa  makaa  hayo kupata mwekezaji  lakini hakuna cheti  walashukururani kutoka NDC pamoja na kuandika barua chungumzima lakini jeshi lapolice bila hiyana wame tambua mchango wawaandishi waHabari Hongera IGP Saidi Mwema

Thursday, January 10, 2013

POLICE WAAGA MWAKA KWAKUTUNUKIA WAANDISHI VYETI VYA UFANYAJI KAZI BORA

 Mwandishi wa Habari wa Star televisheni na Radio Free Afrika Songea Bw Adam Nindi akikabidhiwa Cheti cha pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (kulia)  ikiwa ni zawadi ya utendaji kazi nzuri katika kuzitangaza  kazi nzuri zinazofanywa na Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma na kukemea masuala ya haki za wanawake na watoto (ukatili wa kijinsia). Zawadi hiyo imetolewa na jeshi la Polisi   likikiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa (mwenye suti nyeusi katikati) Deusdedit Kaizilege  Nsimeki katika sherehe za kuukaribisha mwaka 2013.
 Picha hiyo hapo juu ni Mwandishi waTBC Gerson Msigwa akipewacheti cha pongezi kutokana na juhudi za kutangaza kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi bila kuegemea upande wowote, Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kazielege Nsimeki na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
 Pichani juu Askari wa FFU Songea Lema akiwa katika ukakamavu mbele ya mgeni rasmi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma akielekea kupokea cheti na zawadi kwa utendaji nzuri katika kazi.

Picha ya chini ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kazielege Nsimike akitoa neno la mbele kwa wageni waalikwa katika hafla ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa.
 Mwandishi wa Uhuru FM Juma Nyumayo akipokea tunzo ya cheti kilichotolewa na Jeshi la polisi kwa utendaji nzuri wa kazi za polisi mkoani Ruvuma hususani masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa kushirikiana na Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma.
 Juma Nyumayo mwandishi wa Uhuru FM akippongezwa na Kamanda wa Polisi Mko Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kukabidhiwa cheti.
 Askari wa FFU akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa kwa utendaji nzuri wa kazi.
 Picha ya juu ni Askari akienda kupokea tunzo ya cheti cha utendaji nzuri wa kazi.
Jeshi la Polisi katika kuthamini na kuhamasisha askari kujituma katika kazi na kufanya kazi kwa haki imewazawadia vyeti na pesa taslimu askari waliofanya vizuri mwaka 2012 . Mama huyu  ni Askari wa upelelezi akipokea cheti cha pongezi kwa utendaji kazi nzuri wa kazi.  Picha ya chini ni Askari akipewa cheti na zawadi katika haflahiyo.
 Umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu picha hiyo inamwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said T.Mwambungu akiwa na mke wake katika hafla ya mwaka mpya iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi.
 Baadhi ya wadau na Maafisa wa polisi wakiwa katika sherehe za mwaka mpya Katikati ni Mama Mdaula mfanya biashara wa mafuta  mdau wa Jeshi la Polisi na kulia mwenye suti nyeusi ni Kamanda wa Kikosi cha FFU Malile.
 Waandishi wa habari wakionekana katika nyuso za furaha wakimshangilia askari Lema baada ya kupewa zawadi ya kufanya kazi nzuri. katikati ni Askari Lema akiwa na Mkewe Mwandihi wa Mwananchi Joyce Joliga Kulia ni Catherine Nyoni mwandishi wa TBC1 Songea na kushoto bi Cresensia Kapinga wa majira
 Kumaliza mwaka na kuingia mwaka mpya ni majaliwa ya mwenyezi Mungu hapo juu ni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi mjini Songea.
 Maafisa wa Polisi wakisherekea kuumaliza mwaka 2012 na kuuona mwaka 2013 katika sherehe za mwaka mpya zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma mwanzoni mwa mwezi Januari.
 Hapo juu ni risasi zilizokamatwa na Polisi ambazo zingeweza kuhatarisha maisha ya watu na wanyama pori katika mbuga, mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki kwa kushirikiana na raia wema.
 Ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kuuona mwaka Polisi mkoani Ruvuma imweza kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka 2013 kwa kuandaa hafla iliyowakutanisha wadau, familia za askari na maafisa wa polisi na mastafu kutoka wilaya za mkoa wa Ruvuma hapo juu ni baadhi ya waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 OCD wa wilaya ya Songea Kasoro kushoto akiwa na Afande Mashimbi wakiwa katika kikao cha wadau wa polisi kujajili namna ya kukabiliana vitendo vya uhalifu.
 Jeshi la polisi limejitahidi kuendesha msako mkali kwa mwaka 2012 na kuweza kukamata silaha mbalimbali katika maeneo tofauti ya mkoa wa Ruvuma kamazinavyoonekana hapo juu na askari wakizichambua katika makundi yanayofanana.
Jeshi la Polisi Mkoai wa Ruvuma katika oparesheni ya kutokomeza ujangiri na uhalifu wa kutumia silaha mwaka 20012 limeweza kufanikiwa kukamata silaha 270 ambazo zilikuwa zikitumika katika ujangiri wa wanyamapori na kuhatarisha maisha ya watu katika uhalifu. Hapo juu ni baadhi ya silaha ambazo zimekamatwa.

Monday, January 7, 2013

MATUKIOYA UNYANYASAJI WAWATOTO

Kamanda wa  Polisi wazamaniMaiko kamuhanda akimkaribisha Kamanda mpya Deusdedit KaizilegeNsimeki mkoaniRuvuma baada ya yeye kupata uhamisho kuelekea Mkoa wa Iringa. Kulia niKamanda aliyehama na  kushoto ni  Kamanda anayekaribishwa Mkoani  Ruvuma.                                   
Pichani ni mtoto mwenye  umri wa miaka  kumi aliyepigwa na Baba yake wa kambo  (mlezi) nakumsababishia majerahamakubwa  baada ya kupoteza shilingi  mia aliyopewa kwenda kusagia mahindi mama yake akiwa safarini.                                                                                                                           
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdediti  Kaizilege  Nsmeki akitoa neno la asante baada ya kupokelewa na  Kamanda MaikoKamuhanda anayehama Mkoa wa Ruvuma kuelekea Mkoani Iringa
Mama wa mtotoaliyejeruhiwa na  Baba wa kambo akichunguza mwanae kwauchungu sehemu alizojeruhiwa,wamama waige moyo  wa kuwa  na  huruma  na uchungu  kwa watoto wao kwa kuepuka adhabu kalidhidi ya  watoto wadogo.lakini  mama huyu ameshindwa  kutoa ushirikiano kwaenye vyombo vya haki (Mahakama)  ili aliyetendakosa hiloachukuliwe hatua.
Hali halisi yamajerahaaliyopata mtoto  huyo hapojuu  baada  ya kupoteza  shilingi  miamoja.
Baba  wa kambo aliyemjeruhi mtotobaada  ya  kupoteza  shilingi miamoja  katikati  ni  mtotoaliyejeruhiwa   akiwa  na  mama yake  mzazi.
Kushoto  ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la  Songea  Andrew  Chatwanga  akiwa Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma dkt Daniel  Malekela  wakijadili jinsi ya  kuendeleza  Hospitali  hiyo ya  Mkoa.
Mwenyekiti wa  Mtandao   wa Polisi wanawake  Mkoa  wa  Ruvuma  Ana  Tembo akiwa katika   mazoezi  tayari  kwa kukabiliana na  ukatili dhidi  ya mama na  mtoto
Jambo    kubwa  katika  maisha  ya binadam ni  kuhakikisha  anapata  afyabora lakini   binadamu   wenye uchu wa  mali  huweka pesa mbele kuliko  afya za binadamu. Viongozi  waManispaa  ya  Songea wamefanikiwa  kukamata  vyakula  na  vipodozivilivyokwisha   muda  wake  vyenye   thamani  ya  shilingi1,058,700
Vifaa  vilivyokamatwa  nakuteketezwa  kwa   moto   vikionekana  hapo juu
Muonekano wa vyakula  vilivyoteketezwa  kutokana   na  kuharibika  na  kwisha  muda  wake kwa matumizi ya bin





Picha hiyo  hapo  juu ni  moto ukitekeketeza  vipodozi  na  vyakula  vilivyokwisha  muda  wa  matumizi  kama  vilivyoonekana  hapo  juu  kabla  ya  kuteketezwa.




ADAMU NINDI NA TUNZO YAPOLICE

ADAMU MZUZA NINDI KUTUNUKIWA CHETINA JESHI LA POLICE MKOANI RUVUMA KWA UTETEZI WAWANAWAKE NA WATOTO KATIKA KUPAMBNANA NA UKATILI WA KIJINSIA