Mwandishi wa Habari wa Star televisheni na Radio Free Afrika Songea Bw Adam Nindi akikabidhiwa Cheti cha pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (kulia) ikiwa ni zawadi ya utendaji kazi nzuri katika kuzitangaza kazi nzuri zinazofanywa na Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma na kukemea masuala ya haki za wanawake na watoto (ukatili wa kijinsia). Zawadi hiyo imetolewa na jeshi la Polisi likikiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa (mwenye suti nyeusi katikati) Deusdedit Kaizilege Nsimeki katika sherehe za kuukaribisha mwaka 2013.
Picha hiyo hapo juu ni Mwandishi waTBC Gerson Msigwa akipewacheti cha pongezi kutokana na juhudi za kutangaza kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi bila kuegemea upande wowote, Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kazielege Nsimeki na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.Pichani juu Askari wa FFU Songea Lema akiwa katika ukakamavu mbele ya mgeni rasmi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma akielekea kupokea cheti na zawadi kwa utendaji nzuri katika kazi.
Picha ya chini ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kazielege Nsimike akitoa neno la mbele kwa wageni waalikwa katika hafla ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa.
Mwandishi wa Uhuru FM Juma Nyumayo akipokea tunzo ya cheti kilichotolewa na Jeshi la polisi kwa utendaji nzuri wa kazi za polisi mkoani Ruvuma hususani masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa kushirikiana na Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma.
Juma Nyumayo mwandishi wa Uhuru FM akippongezwa na Kamanda wa Polisi Mko Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kukabidhiwa cheti.
Askari wa FFU akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa kwa utendaji nzuri wa kazi.
Picha ya juu ni Askari akienda kupokea tunzo ya cheti cha utendaji nzuri wa kazi.
Jeshi la Polisi katika kuthamini na kuhamasisha askari kujituma katika kazi na kufanya kazi kwa haki imewazawadia vyeti na pesa taslimu askari waliofanya vizuri mwaka 2012 . Mama huyu ni Askari wa upelelezi akipokea cheti cha pongezi kwa utendaji kazi nzuri wa kazi. Picha ya chini ni Askari akipewa cheti na zawadi katika haflahiyo.
Umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu picha hiyo inamwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said T.Mwambungu akiwa na mke wake katika hafla ya mwaka mpya iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya wadau na Maafisa wa polisi wakiwa katika sherehe za mwaka mpya Katikati ni Mama Mdaula mfanya biashara wa mafuta mdau wa Jeshi la Polisi na kulia mwenye suti nyeusi ni Kamanda wa Kikosi cha FFU Malile.
Waandishi wa habari wakionekana katika nyuso za furaha wakimshangilia askari Lema baada ya kupewa zawadi ya kufanya kazi nzuri. katikati ni Askari Lema akiwa na Mkewe Mwandihi wa Mwananchi Joyce Joliga Kulia ni Catherine Nyoni mwandishi wa TBC1 Songea na kushoto bi Cresensia Kapinga wa majira
Kumaliza mwaka na kuingia mwaka mpya ni majaliwa ya mwenyezi Mungu hapo juu ni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi mjini Songea.
Maafisa wa Polisi wakisherekea kuumaliza mwaka 2012 na kuuona mwaka 2013 katika sherehe za mwaka mpya zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma mwanzoni mwa mwezi Januari.
Hapo juu ni risasi zilizokamatwa na Polisi ambazo zingeweza kuhatarisha maisha ya watu na wanyama pori katika mbuga, mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki kwa kushirikiana na raia wema.
Ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kuuona mwaka Polisi mkoani Ruvuma imweza kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka 2013 kwa kuandaa hafla iliyowakutanisha wadau, familia za askari na maafisa wa polisi na mastafu kutoka wilaya za mkoa wa Ruvuma hapo juu ni baadhi ya waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
OCD wa wilaya ya Songea Kasoro kushoto akiwa na Afande Mashimbi wakiwa katika kikao cha wadau wa polisi kujajili namna ya kukabiliana vitendo vya uhalifu.
Jeshi la polisi limejitahidi kuendesha msako mkali kwa mwaka 2012 na kuweza kukamata silaha mbalimbali katika maeneo tofauti ya mkoa wa Ruvuma kamazinavyoonekana hapo juu na askari wakizichambua katika makundi yanayofanana.
Jeshi la Polisi Mkoai wa Ruvuma katika oparesheni ya kutokomeza ujangiri na uhalifu wa kutumia silaha mwaka 20012 limeweza kufanikiwa kukamata silaha 270 ambazo zilikuwa zikitumika katika ujangiri wa wanyamapori na kuhatarisha maisha ya watu katika uhalifu. Hapo juu ni baadhi ya silaha ambazo zimekamatwa.
No comments:
Post a Comment