Ndugu
zangu wasomaji wa Blog ya Songea Habari napenda kuwapongeza kwa mwaka 2012 kwa
kutoa ushirikiano wa kuweza kuchangia katika Masuala yanayohusu jamii hasa
jamii inayoishi pembezoni mwa Nchi na kuonyesha changamoto zinazowakabili.
Kwa
habari za kina nilikuwa nikiifahamisha Jamii kwa kitu kinachoitwa uchawi
ambacho ndicho changamoto kwa watu wanaoishi pembezoni.
Mganga wa jadi bint Frola
Ndembo
Nikiwa
katika kambi ya Mganga mashuhuri wa Nyanda za juu Kusini Mama Binti Flora
Ndembo nimeweza kupata siri kubwa kuhusu uchawi. Wachawi wenyewe wamesema
wamejiingiza katika uchawi baada ya kuona Jamii ikiwatenga, wale ambao ambao
hawana uchumi wa kutosha ndio wanaunda umoja wa kuwatesa wenzao.
Add caption |
Mkuu wa Wachawi kutoka
Mwambao wa Ziwa Nyasa akiwa amesimama akieleza Jinsi alivyojiingiza katika
Uchawi. Mguu unao uona wa kulia uliovimba kama
Rungu, huo Mguu ni gia ya kupaa angani akigonga na Mguu wa kushoto ndipo huanza
kuruka akielekea eneo alilo panga.
Tu kiachana na Mchawi mkuu wa Mwambao wa Ziwa Nyasa sasa tuangalie mchawi wa Matimila Songea Vijijini ambaye alimua mtoto wake ambaye alikuwa Padiri akitangaza kujitoa katika Uchawi amesema ameamua kujitoa baada ya wachawi wenzie kumuua mtoto
wake ambaye alifikia ngazi ya kuwa Askofu; hapo ndipo alipoona kuwa uchawi
hauna maana.
Nikiwa
katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika
maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi
mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake
kuweka rehani mwili wake baada wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Nikiwa bado katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo, nilitiwa na fadhaha baada ya kumuona Binti mwenye umri wa miaka 10 aliyepewa uchawi na Mama yake na kuweza kupewa mboga ya akiba ambacho ni kidonda kilicho ubavuni ambacho yeye alikiri kuwa akikosa mboga hutumia kwa kuchovya kwenye kidonda. Maskini Binti huyo katika maisha yake hadi kufikia miaka hiyo 10 alikuwa akichukia shule kama nini lakini baada ya kufika kwa Binti Ndembo ameacha uchawi na kuomba akaendelee na Masomo
Kamanda
wa POLICE aliye hamia Iringa Maiko Kamhanda kushotona Kamanda Mpya Mkoa wa
Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki
Ndugu yangu nikiwa katika kambi hiyo na Binti
Ndembo nimeona mambo mengi cha kufurahisha mganga huyo hana uchochezi. Yeye
amekuwa akipatanisha ndugu hao na kuwa Jamii moja. Nikiwa Kambini hapo
nimeshuhudia Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akitoa elimu Shirikishi kwa kutaka Jamii iachane
na Mambo ya Ushirikina.
Mganga
huyo mashuhuri mbali ya kutibu watu wenye asili ya Ushirikina lakini hata hivyo
ameshaweza kukamata Majambazi Sugu, na wao kusalimisha silaha zao na kuachana
na Ujambazi.
Jambo
la kuingilia Masuala ya Ujambazi, Mganga huyo mashuhuri amepata misukosuko kwa
kuwahi kupigwa risasi mbili na kukimbizwa Hospitali ambako alitolewa.
Amewahi
kufungwa Kamba na kutupwa msituni na kuambiwa aachane na masuala ya kufuata
Majambazi lakini uganga wake uliweza kumwokoa.
Pia
kwa Mara ya Kwanza Mganga huyo aliweza kubainisha ndoa iliyofungwa kati ya Mama
na Mtoto wake wa kuzaa mwenyewe. Hatimaye aliweza kuibainisha Ndoa hiyo
hadharani.
Ndugu zangu wasomaji, Shabaha yangu ni
kutaka kuendelea kupata mawazo kutoka kwenu, kitu kikubwa ambacho kinasababisha
Maendeleo kuto chukua Kasi ni Kushiriki katika Mambo ya Ushirikina. Sasa hapa tumeona watu walio wengi wakiacha
Uchawi na kutangaza Hadharani.
Hii ni Ruvuma Jee Mikoa mingine Ukombozi
utatoka wapi?
Wasomi na watu wenye Vipaji watume Elimu yao kuutokomeza
Ushirikina na wale wenye Ushirikina wajitoe Hadharani kuachana na USHIRIKINA.
No comments:
Post a Comment