KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, August 25, 2013

WATOTO WANAO ISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI SONGEA WAPATA MSAADA WA CHAKULA KUTOKA POLICE SONGEA


Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimike akiwakilishwa na Kamishina Msaidizi wa Police George Chiposi  amelitaka jeshi la Police na Wananchi kwa ujumula kuwa na tabia ya Huruma Upendo kwa watoto ambao wamepoteza wazazi wao .

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Akiwakilishwa na Kamishina Masaidizi wa Police Goerge Chiposi amesema wimbi la Watoto wanao ishi katika Mazingira Hatarishi lina zidi kuongezeka kutokana na watoto kupoteza wazazi wawili pia Mfarakano katika Ndoa ,Watoto wana baki bila Malezi ni juu ya Jamii sasa kuchukua Hatua ya kuwa sadia
Kamishina wa Police George Chiposi amesema karine zote zilizopita Jeshi la Police ndilo lililo kuwa kitishio cha watoto hivyo Watoto  walitokea kuichukiwa Jeshi la Police .sasa Police wanatakiwa kubali hali hiyo kivitendo

Mumiliki wa kituo cha  kulelea watoto cha St Antony  Anna Majic kilichopo mfaranyaki songea  amesema ameshukuru kupata ushirikiano na jeshi la Police  kwa kupata msaada  wa vyakula  huo ni ujumbe tosha kwa watoto.



Katika kilele cha siku ya Police Mkoani Ruvuma kumeandamana na Police wanawake kufanya semina ya jinsi ya kukomesha vitendo viovu wanavyo fanyiwa jamii.pia kutoa elimu katika maeneo mbalimbali jinsi ya kuwa fanya wananchi wasaidiane na police kutokomeza vitendo vya kiuhalifu

POLICE SONGEA WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA RUVUMA


Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa  kukabiliana na Vitendoi vya Unyanyasaji wa Kijinsia Mpaka sasa kesi zaidi ya 400 katika kipindi cha 2012/2013 zime weza  kuwabainika ,Na  wanawake 6 waliobakwa na kuuwawa kesi zao ziko Mahakamani . Kubwa zaidi  Police Wanawake wamefanikisha kujenga  Jengo la polisi Wanawake lililogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 30 ambalo  mpaka sasahalijaanza kazi  kutokana na kukosekana kwa Milango na Madirisha.

 Mtandao wa police wanawake Mkoa wa Ruvuma kila wakati wamekuwa wakijitolea kuona wagonjwa na kuwafariji wanasema huo ndio moyo wa mwanamke aliye zaliwa na Mwanamke mwenye Huruma
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umewataka wanawake kuachana na vitendo vya kikatili kwa kutoa adhabu kali kwa Watoto pale wanapokosea. Pia kuachana na tabia ya kutelekeza Watoto na wengine kuwauwa.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha Wiki ya Polisi Wanawake ambayo iliongozana na kutoa zawadi kwa wagonjwa 250 wakiwemo Wanawake waliojifungua 85 na Wanaume waliolazwa Hospitali ya Mkoa.


Naye Msimamizi wa Dawati la Polisi Wanawake wilaya ya Songea Mrakibu Msaidizi wa Polisi Paulo Mashimbe amewataka wan aume nao kujitokeza katika kubanisha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na Wanawake.

 Wagonjwa Mbalimbali walipata zawadimbalimbali ikiwemo matunda,nguo,na sabuni za kufulia
 WP Police wakike akionyesha mapenzi kwa mtoto aliyoko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
 Mtoto akionyesha furaha baada ya kutembelewa na Mtandao wa Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma


Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  Walta Soko amesema Wanawake wameumbwa kwa Roho ya kuwa na huruma, wanawake waache kuiga tabia ya kuwa wakatili huko ni kukosa  Maadili halisi ya wanawake.
Naye Muuguzi wa Wodi ya Wazazi ya Wanawake amesema Tendo la Polisi Wanawake kutoa Msaada ni tendo lenye fundisho kwa Wazazi wote wa Kike na wa Kiume

Tuesday, August 20, 2013

UMEWAHI KUONA NYWELE NDEFU KWA MWAFRIKA HEBU ONA

Dada yangu Asha Mandela ana nywele ndefu ambazo humpa kazi ya kuzisuka hepu onna zilivyo Tanda katika ukumbi wake

WAHARIRI WAANDAMIZI WA GAZETI LA HABARI LEO WAKIPEWA MAELEZO BAADA YA KUTEMBELEA ENEO LA KUZALISHA VIFARANGA VYA SAMAKI ENEO LA LUHILA SONGEA

 Maafisa  waandamizi wa Gazeti la Serikali la Habari Leo  Dativa Minja na Beda Msimbe kutoka Dar es Salaam walipotembelea katika Bwawa la Kuzalisha vifaranga vya Samaki la Luhila Manispaa ya Songea Kwa Mjibu ya Tarifa alizo pewa Juma Nyumayo na Afisa Uvuvi amesema kuna Vifaranga vya Samaki vipatavyo 127,617
 Kiongozi wa Habari Leo Dativa Minja akiwa na Mwenyeji wake Mwariri Mwandamizi wa Magazeti ya Kanda ya Kusini TUJIFUNZE Juma Nyumayo wakiangalia hali ya uzalishaji wa Samaki kwa njia ya kisasa.Ambapo Wanchi wa Wilaya ya songea wamefaidika kwa kuuziwa  vifaranga 75,850
 Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa yaMajaribio ya Uzalishaji wa Vifaranga kwa njia ya kisasa ambapo kwa sasa Mkoa umefanikiwa kupandikiza Samaki Dume kuzalisha Vifaranga.Pichanini ni Kiongozi kutoka Habari Leo Dativa Minja akiangalia Bwawa hilo lililopo Luhila Manispaa ya Songea  alipotembelea Mkoani Ruvuma kwa kazi maalumu.
 Maafisa Waandamazi wa Gazeti la Serikali la Habari Leo Bw. Beda Msimbe na Dativa Minja wakipewa maelezo ya kina kuhusu uzalishaji wa Vifaranga katika Bwawa la Luhila lililopo Manispaa ya Songea.
 Maafisa Waandamazi wa Gazeti la Serikali la Habari Leo Bw. Beda Msimbe na Dativa Minja wakisikiliza kwa makini kuhusu uzalishaji wa Vifaranga na njia zinazotumika kuboresha ufugaji wa Samaki katika Bwawa la Uzalishaji wa Samaki Luhila Manispaa ya Songea.

AKINA MAMA WAFURAHIKUWAONA WAUME ZAO KATIKA MACHIMBO YA URENIAM

 Wake wa Wafanya kazi wa Mgodi wa Urenium Namtumbo wakielekea Mgodini(mkuju) kuwatembelea waume zao ambao huwatembelea kila baada ya miezi mitatu.
 Wake wa Wafanya kazi wa Mgodi wa Urenium Mkuju Namtumbo wakipata chakula cha pamoja na waume zao walipokwenda kuwatembelea mgodini hapo.
 Wake wa wafanyakazi wa Mgodini wakitembelea maeneo mbalimbali yanayozunguka Mgodi wa Urenium Namtumbo wakiangalia kazi wanazozifanya waume zao na namna inavyoonekana Urenium.
 Wadau mbalimbali wakiangalia Urenium kabla yakuchimbwa na kupata maelekezo toka kwa wafanyakazi wa mgodi jinsi wanavyofanya kazi ya uchimbaji wa urenium.
Mtaalamu wa Jiolojia(mwenye shati la Kijani) katika Mgodi wa Urenium Mkuju Namtumbo akiwatoa hofu wake za wafanyakazi wa Mgodi kuwa Urenium haisababishi watu kupunguza nguvu zakiume kama ambayo wananchi wengi wamekuwa wakiamini kuwa Urenium inapunguza nguvu za kiume. Aliyevaa Jaketi jekundu ni mwariri mwandamizi wa Gazeti la Habari Leo kutoka Dar-es-salaam alipotembelea mgodini hapo.

Thursday, August 15, 2013

BINADAMU ANA TAKIWA KUIGA MAISHA YA KINYONGA HUJIBADILISHA WAKATI SHIDA NA HUJIBADILI WAKATI WA RAHA

 Mazingira ya wanyama mbalimbali huishi sawa na eneo wanalo taka wanyama kama kinyonga, Kenge, Mjusi hutafuta maeneo ambayo wanaweza kupata kitoweo kwa urahisi kama vipepeo nzige na samaki wadogo katika kisiwa hiki cha pomonda kuna kila aina ya mijusi ya Rangi pia Vingonga wa kila namuna
 Moja ya Vivutio kwa Watali ni Vinyonga wa ana mbali mbali kama unavyo mwona huyo hapo juu .Lakini la msingi kinyonga huishi kwa utalamu anapo taka mawindo fulani hujibadili na sehemu aliyopo.Nivizuri nao binaadamu wa kajifunza hali ya Kinyonga ili wakati wa Shida  wajue kuna shida na wakati wa raha wakalijiua hilo
 Kinyonga hana Rangi isipo kuwa Mwenyezi Mungu amempa kinyonga Uwezo wa kujibadili kutokana na Hali ya Mazingira ilivyo ana uwezo wa kujikinga ha Hatari kutokana na Hali ilivyo, Hapo Kajibadili akiwa Katika Jiwe kubwa eneo la Pomonda.
 Maua yanapo chanua huonyesha furaha na yapo nyauka huonyesha mwisho wa uhai wa Binadamuhata Binadamu humia maua yanapo chanua kuonyesha furaha .Hakuna  anaye tumia ua likiwa lime nyauka

Wednesday, August 14, 2013

WATU WAO ISHI PEMBEZONI HUWA WAKWANZA KUFAIDI MATUNDA YA WAGENI KUTOKA NJE NDIVYO ILIVYO KWA WATU WA LITISHA



 Wasanii wa Ngoma ya Asili ya Kinyasa ijulikanayo kwa jina la Mganda wakitumbuiza katika Sherehe ya Jubilei ya Miaka 25 ya Huduma ya Afya ya Msingi iliyofanyika katika Kijiji cha Litisha Peramiho Songea Vijijini.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho Dr. Ansgar Stuffe (kushoto) akiwa na wageni wake kutoka Ujerumani Rais wa Benki ya Ujerumani Frant Mader na Binti yake Franz Mader wakikagua mabanda ya utekelezaji wa shughuli za Afya ya Msingi zinazosimamiwa na Dr. Ansgar Stuffe katika kuboresha Afya za Jamii iliyo pembezoni.
 Dr Ansgar Stuffe akiwa na wananchi wa Kata ya Ruvuma katika kusherekea jubilei ya Miaka 25 ya Utekelezaji wa Huduma ya Afya ya Msingi kwa wakazi wa Tarafa ya Ruvuma Peramiho Songea Vijijini
Ngoma ya Mganda ikishirikisha wanawake hebu ona wanawake wanavyo sakata ngoma , hii ni kuonyesha Wanawake wanaweza
 Wahudumu wa Afya Vijijini (WAVI) wakifurahia Mafanikio ya Mradi wa Afya ya Msingi katika kipindi cha miaka 25, 1988 - 2013 kwa wananchi waishio pembezoni kata ya Ruvuma wilayani Songea Vijijini. Juhudi hizo zinatokana na jitihada za Dr. Ansgar kwa kushirikiana na Wahudumu wa Afya katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa yakiisumbua jamii hiyo.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho na Mfadhili wa Mradi wa Huduma ya Afya ya Msingi Vijijini akikagua Mabanda ya Maonyesho ya namna ya kujikinga na Afya Bora katika kuadhinisha jubilei ya Miaka 25 ya Utekelezaji wa Huduma hiyo kwa kuboresha huduma ya maji, kinga ya Malaria kwa kuwapa chandarua na kutokomeza magonjwa yaliyosahaulika.

BEDA UNAIONAJE SONGEA KATIKA UTAFITI WAKO WAAMBIE WASIO UJUA MKOA WA RUVUMA

 Hayo ni maeneo anayo fanyia kazi bwana Beda Msibwe katika kutangaza vivutio vya Moa wa Ruvuma hiyo ni hotell mashuri ambayouna pata vyakula vya asili vya mtanzania
 Crista Park Mo tell ni moja ya vivutio kwa wageni mkoani hapa vyakula vyote vya kigeni hupatika katika hoteli hiiina wahudumu walio enda shule na kuhitimu vizuri,uingiapo hapo una weza kusahau hata nyumbani
Beda Msimbwe baada ya kupata chakula katika Motel ya Crita Park akionyesha furaha kwa jinsi chakula kilivyo bora alio kuwa nao ni mabloger wa Mkoa wa Ruvuma kushoto  Adam Mzuza Nindi  Demasho blog
Demasho akimwonyesha maeneo ndugu Beda Msimbwe katika eneo Songea Mjini
Nimekuambia ndugu yangu moja ya vivutio vizuri Mkoani hapa ni chakula cha uhakika kama unavyo kiona huo una itwa Ugali kwa Samaki

WANANCHI WANAO ISHI PEMBEZONI HUISHI KWA MATATIZO HASA KATIKA UTAFUTAJI PESA

 Jamii ya Watanzania wengi walioko pembezoni mwa Nchi katika kisomo chao wameweva kupata elimu kwa akina mama kuuza bagia kama unavyo ziona hapo juu lakini pamoja na hayo hakuna anaye weza kuzungumuza kuhusu bidhaa hiyo uki onekana una zungumuzia au kununua una onekana Mshamba.
 Katika Utengenezaji wa Bagia uko aina nyingi bagia imeweza kuwa somesha watu wengi kutokana na gharama zake pia kwa vijijini ndicho kitafuno kikubwa ambacho kuanzia mtoto hadi mkubwa ana uwezo wa kukimudu jee unaye soma Blog hii umesomeshwa kwa mtindo gani, kama ni mtindo huu basio uwapo kijijini jaribu kuwa ungisha wa uzaji wa bidhaa hizi
 Kama sikosei hakuna mtu asiye juua usafiri wa kijijini ni upi rahisi Gari za Vijijini ambo huweza kusafirisha bidhaa kiurahisi ni Punda hap[omama baada ya kutengeza pombe iitwayo Komoni ikiwa ime wekwa kwenye Gudulia tayari kwa kwenda kuuza
 Watoto wenye umuri wa miaka 9-12 ndio wanao kuwa madereva wa kuendesha mikokoteni ya Punda wanasema kufanya hivyo kuna wasaidia kuweza kupata sare za shule, mahitaji muhimuya nyumbanipamoja na kuwa safirisha watu kwenda hospitalini, Jee wewe una mchango gani katika usafishaji wa Bidhaa vijijini
 Punda anapo safiri huweza kujua kanununi zote za Barabarani akiambiwa simama huweza kusimama akiambiwa kimbia basi hukimbia lakini kama nilivyo sema madereva wa Usafiri huoa ni watoto walio chini ya miaka 12 hapoakiwa kijijiji cha morogoro kuelekea mashambani
 Mama akiwa ana pokea pombe aliyo mtuma kijana aliye chini ya miaka 12 hapo ana ipeleka kilabuni tayari kwa kuuza
 Katika kuadhimisha miaka 25 ya Huduma ya Afya ya Msingi Tarafa ya Ruvuma mpiga mbiu ya mgambo akiwa ita watu kusogea eneo la Sherehe uwanja wa Litisha Songea vijijini
 Mtaji ulio wajuu kasa vijijini ni uuzaji wa pombe za kienyeji wanywaji hudai kuwa unapo kunywa pombe za kienyeji zina leta nguvu hata katika utayarishaji wa kilimo.jambo lingine huwa tiba wa watu wanao ishi vijijini ukiangalia ongezeko la wangonjwa vijijini na mjini wagonjwa wengi hutoka mijini
 Mzee Marufu litisha akinywa Pombe ya kienyeji ijulukanayo kwa jina la Komoni Mzee Myakaya ana serma bila kuonja pombe ya kienyeji hawezi kufanya kazi yoyote ile
Usisahau Usafiri wetu vijijini tunapo zungumuza swala la Mkurabita tuangalie sana vijijini kweli ifikapo  2025 tutaweza uondoea umasikini waja wazito hawata safirishwa na punda, eneo la kilimo hatuta tegemea mifugo kwa ajili ya plau