Mtandao wa
Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kukabiliana na Vitendoi vya Unyanyasaji wa
Kijinsia Mpaka sasa kesi zaidi ya 400 katika kipindi cha 2012/2013 zime weza kuwabainika ,Na wanawake 6 waliobakwa na kuuwawa kesi zao ziko
Mahakamani . Kubwa zaidi Police Wanawake
wamefanikisha kujenga Jengo la polisi
Wanawake lililogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 30 ambalo mpaka sasahalijaanza kazi kutokana na kukosekana kwa Milango na
Madirisha.
Mtandao wa police wanawake Mkoa wa Ruvuma kila wakati wamekuwa wakijitolea kuona wagonjwa na kuwafariji wanasema huo ndio moyo wa mwanamke aliye zaliwa na Mwanamke mwenye Huruma
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma umewataka wanawake kuachana na vitendo vya kikatili kwa kutoa adhabu kali kwa Watoto pale wanapokosea. Pia kuachana na tabia ya kutelekeza Watoto na wengine kuwauwa.
Mwenyekiti wa Mtandao
wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo
ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha Wiki ya Polisi Wanawake ambayo iliongozana
na kutoa zawadi kwa wagonjwa 250 wakiwemo Wanawake waliojifungua 85 na Wanaume
waliolazwa Hospitali ya Mkoa.
Naye
Msimamizi wa Dawati la Polisi Wanawake wilaya ya Songea Mrakibu Msaidizi wa
Polisi Paulo Mashimbe amewataka wan aume nao kujitokeza katika kubanisha vitendo
vya unyanyasaji vinavyofanywa na Wanawake.
Wagonjwa Mbalimbali walipata zawadimbalimbali ikiwemo matunda,nguo,na sabuni za kufulia
WP Police wakike akionyesha mapenzi kwa mtoto aliyoko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
Mtoto akionyesha furaha baada ya kutembelewa na Mtandao wa Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Walta Soko amesema Wanawake wameumbwa kwa
Roho ya kuwa na huruma, wanawake waache kuiga tabia ya kuwa wakatili huko ni
kukosa Maadili halisi ya wanawake.
Naye Muuguzi wa Wodi ya Wazazi ya Wanawake amesema
Tendo la Polisi Wanawake kutoa Msaada ni tendo lenye fundisho kwa Wazazi wote
wa Kike na wa Kiume
No comments:
Post a Comment