Watalamu kutoka Mkoani Ruvuma waki ngoja kukabidhi Mwenge Mpakani mwa Mtwara na Ruvuma
Chipukizi kutoka Mtwara wakiwa tayari Kuupokea Mwenge kutoka Ruvuma
Kijana Chipukizi kutoka Mtwara akitoa Heshima kwa kwa mkimbiza Mwenge Mkoani Mtwara
Viongozi kutoka Mkoani Ruvuma wakiwa nanyumbu wakingoja Mwenge wa Uhuru ukitokea Wilaya ya Tunduru
Viongozi wa Chama na Serekari kutoka Mkoani Ruvuma wakiwa Tayari kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Viongozi wa Mkoa wa Mtwara
Kiongozi wa Ngazi za Juu Mkoani Ruvuma akiratibu mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bakari Naricho akikabidhi Mwenge Kwa kiongozi wa Mbio Za Mwenge
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bakari Naricho akikabidhi Mwenge Kwa kiongozi wa Mbio Za Mwengewa Uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa Noman Adamson Sigalla
Kaimu mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pro .Noman Sigalla King amsema miradi hiyo iliyo zinduliwa imeshirikisha nguvu za
Serekari kuu ,Serekari za Mitaa, Wananchi na Wafadhili
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chumu akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king' mara baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa wa Ruvuma.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king akitoa maelezo ya Miradi iliyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Omary Dendego wakisubiri kupokea mwenge kutoka Mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa Juma Khatibu Chumu amewaomba
Wananchi kuendelea kushirikiana katika kazi za maendeleo pia kuwaombea wakimbiza Mwenge kitaifa ili
waweze kukamilisha mbio za Mwenge Tanzania nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh
Halima Omary Dendego amesema Mwenge wa
Uhuru utakimbizwa katika Mkoa wa Mtwara na kuzindua Miraidi 47 yenye thamani ya
Shilingi Bilioni 96.
viongozi na wananchi mbalimbali wakiwa Wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara kushuhudia makabidhiano ya Mwenge kutoka Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi mbali mbali wakisubiri kutoka Mkoa wa Mtwara wakisubiri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.
Chipkizi wa Halaiki ya Mwenge wa Uhuru wa Mkoa wa Mtwara wakiwa tayari kwa kumpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wilayani Namnyumbu Mkoa wa Mtwara.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king' akiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma wakisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasili wilayani Nanyumbu kwa lengo la kukabidhi mwenge mkoani Mtwara baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa Police Mkoa wa Mtwara Yahaya Ramadhani akiwa na RPC Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela wa kiwa Mpakani Mtwara Kukabidhiwa Mwenge
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara.
RPC Mtwara na RPO Ruvuma
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara wakiwa wanasubiri kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Ruvuma ili kuanza Mbio zake katika Mkoa wa Mtwara
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara akiwa na Mbunge wa Tunduru wakiwa mpakani Nanyumbu mkoani Mtwara
Mwenge wa Uhuru ambao
uliwashwa 29/04/2015 na Rais wa Zanzibar
Dr Ally Mohamed Shein katika Uwanja wa Majimaji wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma
utakimbizwa kwa siku 161 na kuhitimishwa mbio zake mwezi wa kumi mwaka huu.Nikiripoti
kutoka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara ni Adamu Nindi wa Star tv
No comments:
Post a Comment