Kilimo kina manufaa endapo mkulima atazingatia kanuni bora za kilimo, Shirika la ACTN kwa kushirikiana na Mashirika mengine yanayojihusisha na masuala ya Kilimo ili kumletea tija mkulima kwa ufadhili wa Shirika la AGRA wanaendesha mradi wa miaka mitatu kupitia Mtandao wa Kilimo Hifadhi unaolenga kutoa Elimu ya ugan kwa wakulima kupitia Mashamba Darasa na majaribio ya urutubishaji wa Udongo. Katikati ni Mtaalamu wa Kilimo hifadhi kutoka ACTN Abiud Gamba akitoa Elimu ya Urutubishaji kwa wakulima wa Madaba katika moja ya Mashamba Darasa.
Wakulima wakiwezeshwa Elimu sahihi ya Kilimo wanazingatia kinachowashinda ni namna ya kuifikia Elimu hiyo hapo mkulima wa Madaba akifurahia kupata Elimu ya Kilimo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Kilimo, anaona Elimu ilichelewa kumfikia kwa kuwa ana matumaini ya kupata mazao mengi tofauti na kilimo alichokuwa anakitumia awali ambacho kilikuwa hakimpi tija.
Mtaalamu wa Kilimo kutoka Shirika la ACTN Bw Abiud Gamba akifurahi kuona mabadiliko yaliyojitokeza katika majaribio ya Mashamba darasa waliyoyafundisha kwa wakulima wa Madaba huku wakulima wakiwa na imani ya mafanikio kupitia elimu waliyoipata kutoka kwa Mashirika yanayounda Mtandao wa kilimo Hofadhi.
Wananchi kutoka Vijiji vya Songea Vijijini, Namtumbo,na Rudewa wakifuatilia Elimu ya Kilimo Hifadhi kutoka kwa Wataalamu mbalimbali wa Kilimo katika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani yaliyofanyika Madaba Wilayani Songea Vijijini mkoani Ruvuma.
Baadhi ya Wakulima wakisikiliza kwa Makili Elimu ya Uhifadhi wa Mazao.
Wananchi waliohudhuria katika Elimu ya Mkulima kupitia Mashamba Darasa wamefurahi kufikiwa na Elimu hiyo wameomba Maafisa Kilimo kuwapitia wakulima mara kwa mara na kutoa Elimu ya Kilimo bora na kuyashuru Mashirika yaliyoamua kuwabeba wakulima ili nao waweze kunufaika na kilimo kama ambavyo wafanya kazi wananufaika na kazi wanazozifanya. Wameiomba Serikali kuwatafutia Masoko ya Uhakika ya kuweza kuuzia Mazao yao.
Baadhi ya Mbegu Bora zinazouzwa na Mawakala wa pembejeo walioko Manispaa ya Songea zenye Ubora wa hali ya juu.
Wataalamu wa Vifungashio aina ya vifukofuko wakitoa Elimu ya uhifadhi wa kisasa unaompunguzia gharama mkulima na kuepukana na wadudu waaaribifu wanaoshambulia mazao ambavyo haviitaji mazao yapulizwe dawa ambazo kwa kiasi kikubwa zina uwezekano wa kumuathiri binadamu. Vifukofuko ni hifadhi nzuri ya mazao isiyo na madhara yoyote na inadumu kwa muda wa miaka mitatu.
wataalamu wa vifukofuko wakionyesha kwa vitendo matumizi ya vifungashio aina ya vifuko fuko kwa wakulima katika maadhimisho ya siku ya mkulima kwa wakulima waliohudhuria.
Mtaalamu wa Mbegu kutoka Kampuni ya SEEDCO Michael Rikanga akielekeza aina ya mbegu inayofaa kwa udongo wa wakulima wa Songea Vijijini.
Wataalamu wa Vifungashio wakionyesha aina ya vifungashio ambayo kwa sasa inapatikana Manispaa ya Songea na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai akiwaasa wananchi wa Wilaya ya Songea vijijini kuchangamkia fursa na kuitumia ipasavyo ili kuendana na kilimo chenye tija.
Viongozi wa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi wakiwa na Mawakala wa Pembejeo na Viongozi wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mashamba darasa na kujionea hali halisi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea akisalimiana na Viongozi wa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo wa Hifadhi.
Baadhi ya Wananchi wakiwa Madaba kufuatilia mafunzo ya Kilimo hifadhi wakati wa Maazimisho ya Siku ya mkuma Shambani Madaba.
Wananchi wakitafakari jinsi ya kuboresha Kilimo.
Hiki ni Kielelezo tosha kinachoonyesha jinsi gani Viongozi wanavyothamini kilimo, kielelezo hicho kinaonyesha mashirika yanayounda mtandao wa kilimo hifadhi yakilenga kumkomboa mkulima na umaskini.
Afisa na Mtalamu katika Shirika la ACTN Abiud Gamba akiwa katika moja ya Mashamba Darasa yaliyoko Madaba Songea Vijijini kujionea hali halisi ya Majaribio ya Mashamba Darasa.
Bw Shamba Mr Waziri kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songea akiratibu mambo ambayo yataweza kumsaidia mkulima kuweza kupata kipato zaidi kutokana na kazi yake ya Kilimo, kulia ni Diwani wa Viti Maalum wa Madaba.
Mgeni Rasmik katika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai akiwa na viongozi mbalimba
Wakala wa Pembejeo za Kilimo Mkoani Ruvuma Bi Rose Haule akielekeza Pembejeo zinazopatikana katika kwake Mtaa wa Serengeti Manispaa ya Songea.
Mtafiti wa Mazao kutoka kutoka Nyanda za Juu Kusini UYOLE Mkoani Mbeya Bw. Remi Mwakimbwala akitoa maelezokwa wakulima juu ya Matumizi sahihi ya Mbolea na aina ya udongo unaotumika katika Viwanja vya soko la Madaba Songea vijijini.
Wataalamu wa Mfumo mzuri wa uhifadhi wa Mazao kupitia vifuko fuko wakitoa elimu ya uhifadhi wa mazao na matumizi ya vifukofuko kwa wakulima wanaofanya majaribio ya Mashamba Darasa kutoka wilaya za Rudewa na Songea Vijijini .
Meneja wa Mradi kutoka Shirika la RUDi na mwakilishi wa AGRA Mr Frenk Mhando mwenye miwani akiwa kijiji cha Madaba yalikofanyika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani ambako majaribio ya Kilimo Hifadhi kupitia Mashamba darasa ya wakulima yanafanyika ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Mraji wa Miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment