Mawakala wa mbegu wakitoa Elimu ya Matumizi sahihi ya upandaji wa mbegu bora katika sherehe za siku ya Mkulima zilizofanyika Kijiji cha Amani Kata ya Amani Wilayani Rudewa Mkoani Njombe.
Afisa Miradi wa Shirika la ACTN Tanzania Deogratias Ngotio katikati akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mr Naftali Mundo ambaye ni Afisa kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Ludewa (kulia) na kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Kilimo Hifadhi kutoka Shirika la ACTN Abiud Gamba wakiwa katika sherehe za Siku ya mkulima zilizofanyika Kijiji cha Amani Wilayani Rudewa chini ya utekelezaji wa majaribia ya mashamba darasa kutoka katika Vijiji 10 vya wilaya ya Ludewa.
Mmiliki wa Shamba Darasa lililopo kijiji cha Amani Bw. Kastory Hotman Mlelwa akifurahia Mabadiliko ya uzalishaji wa zao la Mahindi baada ya Kupata Elimu ya Kilimo hifadhi toka kwa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi yakiongozwa na Shirika la ACTN. Amasema Elimu ya Kilimo hifadhi ni nzuri kwa kuwa inapunguza gharama za vibarua kwa muda mfupi na upatikanaji wa mazao unakuwa wenye tija.
Bw. Emmanuel Christopher Mwakibala ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Dawa za kuua Magugu aina ya SYNGENTA , Primagram Gold akitoa Elimu ya matumizi sahihi ya dawa ya kuondoa magugu shambani kwa wakulima wa Wilaya ya Ludewa siku ya sherehe ya siku ya wakulima iliyofanyika Kijiji cha Amani na kujionea matokeo ya uzalishaji baada ya kupata elimu ya Kilimo Bora.
Wakulima wa Wilaya ya Ludewa wametoa ushuhuda wa faida wanayoipata baada ya kupata Elimu ya Kilimo hifadhi na Urutubishaji wa udongo wameongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutoka Majunia 5 hadi 7 waliyokuwa wakiyapata wakati wakilima kilimo cha mazoea na sasa ambapo wanapata gunia 15 hadi 25 kwa kufuata Elimu ya Kilimo Hifadhi.
Wakulima wa Ludewa wameyaomba Mashirika yanayoendesha Elimu ya kilimo Hifadhi na ya pembejeo za Kilimo kupanua wigo wa usambazaji wa elimu ya Kilimo Bora chenye tija ili iweze kuwafikia wakulima wengi kwa kuwa Kilimo ndiyo uti wa Mgongo wa Tanzania ambacho kinaajiri watu wengi hivyo elimu hii ikiwafikia wengi taifa litaepukana na umaskini.
.
Wakulima wa Vijiji vya Amani, Mkongobaki, Mavanga, Mundindi na vijiji vingine vya wilaya ya Ludewa wakiwa katika sherehe za siku ya Mkulima Kijiji cha Amani wameiomba serikali kusimamia suala la masoko ya mazao wanayozalisha ili wapate faida kupitia kilimo chao.
Wakulima wa Ludewa wameomba kutafutiwa masoko ya uhakika ili waongeze bidii wakiwa na imani ya uhakika wa kuuza mazao yao kulingana na kauli mbiu ya Kilimo kwanza, wamesema mwaka jana waliyumba katika masoko ambapo uzalishaji ulikuwa mkubwa lakini tatizo lilikuwa upande wa masoko.
Wakulima waliopata Elimu ya Kilimo Hifadhi kutoka wilaya ya Ludewa wamefurahishwa na elimu ya kilimo hifadhi wameomba kwa wale wanaohusika na usmbazaji wa pembejeo kuwafikishia pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuendana na misimu ya Kilimo.
Shamba darasa la Kilimo hifadhi lililopo Kijiji cha Amani Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe.
Wakulima kupitia Risala yao wameiomba Serikali kusimamia taasisi za Benki ili kukubali kupitisha fedha za rudhuku ya pembejeo za Kilimo kuzipitisha kwenye Benki zao ili wakulima wasihangaike.
Mawakala wa Pembejeo za Kilimo na mwakilishi wa Mviwata Mkoa wa njombe wakiwa katika ghafla ya siku ya wakulima kijiji cha Amani wilayani Ludewa.
Mgeni Rasmi katika sherehe za siku ya Mkulima Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wilaya ya Ludewa Mr Naftali Mundo akimpongeza Msoma Risala kwa niaba ya Wakulima wa Wilaya ya Ludewa. Kushoto ni Afisa Miradi kutoka Shirika la ACTN Tanzania Bw. Deogratias Ngotio.
Wawakilishi kutoka Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi ya ACTN
Wakulima wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe
wamefanikiwa kuzalisha Mazao ya Mahindi baada ya kupata Elimu ya Kilimo Hifadhi
ambapo kwa Ekari hivi sasa hupata Magunia 25 na kuendelea.
Wakulima hao wamesema baada ya kuachana na Kilimo cha
Mazao ambapo walikuwa wakipata gunia 3 – 7 lakini hivi sasa wanaweza kuzalisha
Mahindi kwa uwingi na kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kujenga, kusomesha
na kumudu gharama za matibabu kwa familia.
Mwaka 2014 -2015 Wakulima wa Wilaya ya Ludewa wameshindwa
kufikia lengo la kulima mazao ya chakula
kwa wingi kutokana na Mabenki kujitoa
kutopokea Ruzuku ya kilimo kutoka Serikalini na kutegemea benki moja ya Wananchi ya Njombe ambayo ilitoa kiasi cha
shilingi milioni 50 tu kiasi ambacho hakikutosheleza.
Afisa Miradi kutoka shirika la ACTN Tanzani Deogratias Ngotio akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mr. Naftali Mundo wakati wa sherehe za siku ya mkulima Amani kukagua matokeo ya majaribi ya Mashamba Darasa kwa kutumia Elimu ya Kilimo hifadhi chini ya shirika la ACTN.
Bi. Mwantumu Omary Kutoka shirika la utafiti ka Kilimo la IITA akitoa Elimu ya Matumizi Bora ya Ardhi katika Kilimo kwa wakulima wa Wilaya ya Ludewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Ludewa Naftali Mundo amewaomba wakulima kuunda ushirika ili waweze kuwafikiwa na Wataalamu waweze kutoa Elimu ya Kilimo Hifadhi kwa Wakulima wengi
Mwakilishi wa Kampuni ya SYNGENTA inayotoa dawa za kuuwa magugu Prigram Gold Bw. Emmanuel Christopher Mwakibala amewataka wakulima kuzingati Elimu ya matumizi ya Pembejeo za Kilimo kwa kuzingatia wakati mwafaka na matumizi sahihi ili kuona tija.