Shirika la watawa wa
Mtakatifu Aginesi lilianza Chipole songea vijijini ilikiwa na watawa 10 lakini
hivi sasa lina watawa 800 kauli mbiu ni sala na kazi kwa miaka hiyo 75 shirika
la mtakatifu Agines lina miliki shule za msingi, sekondari, pamoja na mtambo wa
kufua umeme ambao mpaka mwezi wa kumi mwaka huu uta samaza umeme wilaya ya
Mbinga na wilaya ya songea
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo
la Kanisa la Mtakatifu Matiasi Kalemba Damian Daniel Dallu amesema
mahusiano mazuri yatakayo fanywa kati ya wakristo na waislamu yataweza
kuendeleza mani tuliyo nayo nchini Tanzania ,Mkristo asione kero unapo
tolewa mwadhana kwa waislamu na mwislamu asione kero anapo sikia kengele
ikigonga kanisani
Kiongozi mkuu wa watawa wa Abasia ya
Peramiho Abate Anastasius OSB amewataka wa umini wa kikirsto hasa
wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hapo mwezi
wa kumi mwaka huu .kwani historia ina onyesha wanawake wanaweza . mfano mzuri
ni Nchi ya Uingereza ambako yulo malikia Elithabet na ujerumani kuwa na malika
Maadhimisho ya Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Watawa Wabenedictin Masista wa Shirika la Mtakatifu Agness Chipole Songea Vijijini. Pichani ni Masista wawili wakisherekea Jubilei ya Miaka 50 ya Maisha kitawa katika Shirika hilo.
Pamoja na kusherekea Jubilei ya Miaka 75 ya Shirila La Masista la Mtakatifu Agness pia Masista 8 wamespongezwa kwa kutimiza Jubilei ya Miaka 25ya usista na wawili wakisherekea Jubilei ya Miaka 50 ya utawa, Hapo wanajubilei wakihapa mbele ya Kiongozi wa Shirika Mama Mkuu na Askofu wa jimbo Katoliki la Songea.
Masista waliosherekea Jubilei wakizunguka Altare kusherehekea mara baada ya kupongwezwa na kusaini hati ya baraka za Papa.
Mwandishi wa Habari kutoka Star Tv Songea Bi Judith Lugoye akifurahi kupata Baraka za Masista waliopata Jubilei ya miaka 25 katika kanisa la Shirika la Mtakatifu Agness Chipole Songea Vijijini mara baada ya ibada maalum ya jubilei iliyoongozwa na Askofu msemwa wa Jimbo la Tunduru - Masasi.
Mafundi Mitambo ambao waliweza kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika sherehe za Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Mtakatifu Agness Chipole wakiwa kazini.
Masista Wanajubilei wakiapa mbele ya viongozi wao ikiwa ni ishara ya kuklubali kuendelea kulinda na kuyatetea maisha ya Kikristu katika Utawa.
Kama ilivyo kwa nyanja zingine kuwa mtu anapovuka hatua moja kwenda nyingine ni lazima apongezwe na wenzake, hapo Masista wakongwe wakipita mbele ya wanajubilei kuwapongeza kwa hatua waliyoifikia.
Wanajubilei Masista wa Shirika la Mtakatifu Agness Chipole wakipokea Baraka toka kwa Askofu mbele ya Altare ya Kanisa Katoliki lililopo Chipole Songea Vijijini ambako Makao Makuu ya Shirika yapo.
Watawa wapya waliongia katika Utawa wakishuhudia jubilei ya wakubwa wao na kujionea maisha ya kitawa jinsi yanavyohitaji uvumilivu na kumtegemea Mungu katika sala.
kila taasisi ina Taratibu na Kanuni zake katika kuwaenze Waasisi, Pichani ni Wanajubilei watawa wa Miaka 50 ya Maisha ya Usista katika Shirika la Mtakatifu Agness wakishukuru na kufurahia zawadi ambayo wameenziwa ya kupewa fimbo za kutembelea kutokana na umri wao, fimbo hizo ni ishara kuwa wameshafikia utu uzima lakini bado wana wajibu wa kumtumikia kristu.
Wanakwaya Masista waliosherehesha katika Ibada ya Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Masista wa Mtgakatifu Agness Chipole wakiiomba kwa shangwe. Hapo unaona jinsi gani Mashirika nao walivyojaliwa vipaji vya aina mbalimbali Sista akipiga Kinanda bila wasiwasi ni karama ya aina yake.
Mama Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agness Chipole akisalimiana na Watawa wageni waliokuja kuungana nao katika Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Mtakatifu Agness Chipole muda mfupi kabla ya kuanza Misa Takatifu ya Jubilei.
Shirika la Masisita la Mtakatifu Agness Chipole Songea Vijijini lilianza likiwa na Masista 8 lakini hadi hivi leo linapotimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake lina Masista 8000 na miradi mbalimbali ya kiuchumi kutokana na usimamizi na uongozi bora wa shirika hilo.
Masista wa Shirika la Chipole pamoja na kujitegemeza katika kuliendesha shirika kupitia kidogo wanachokipata katika miradi yao wana Kituo cha Kulelea watoto Yatima ambacho kwa kiasi kikubwa kinaendeshwa na wao wenyewe na baadi ya weahisani wachache wenye mapenzi mema ambao huwatembele Watoto yatima na kuwasaidia vitu vidogo vidogo ikiwa ni pamoja na mavazi, sabuni na chakula.
Maisha ya Kitawa ni Maisha ya kujitoa zaidi kwa ajili ya wengine, ni kama mwanga wa mshumaa unavyowaka ili wengine wafurahi na unapozima hauna faida kwa wanaopata mwanga huo ni sawa na Masista ambao wanawaka kwa ajili ya kuhudumia Jamii. Hapo Masista wakifurahi kutimiza miaka 50 katika kuleta nuru kwa jamii wakisubiri faida mbele ya mwenyezi mungu.
Mhashamu Askofu Mkuu
wa Jimbo la kanisa la Mtakatifu Matiasi Kalemba Songea Damiani Daniel Dallu amewataka waumini wa Dini ya Kristo kuhedshimu
madhehebu mbalimbali ya dini na kuepuka maswala ambayo yana weza kuleta
uvunjifu wa amani chanzo kikiwa ni dini’
Masista wa Shirika la Mtakatifu Agness wana Miradi mbalimbali kielimu na kiuchumi ikiwepo Shule za Sekondari, Ufundi na Shule za Msingi ambazo zote zinafanya vizuri kitaaluma chini ya usim,amizi wa Mama mkuu na Askofu Mkuu wa jimbo la Songea Mhashamu Askofu Damian Daniel Dalu. Pia Shirika lina Mradi wa Utambo wa Umeme wa tulila ambao unatarajia kufua umeme hivi karibuni na kusaidia wananchi wa Vijiji vya Wilaya za Mbinga na Songea Vijijini.
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Kanisa la Mtakatifu Matiasi Kalemba Damiani Daniel Dallu amesema hayo wakati wakuadhimisha miaka 75 ya Jibilei ya watawa wa Chipole Songea Vijijini Mkoani Ruvuma
Shirika la Masista la Mtakatifu Agness ni Miongoni mwa Taasisi zinazoisaidia Serikali katika Shughuli za maendeleo kwa wananchi na hasa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia elimu.
Watawa wana jubilei wakimuomba Mwenyezi Mungu kuendelea kuwapigania katika miaka 25 mingine ili waweze kutumikia na kufundisha Jamii katika maisha ya kumtegemea Kristu.
Sr. Flora Komba OSB
Masiksta walio tayari kuishi kama Mshumaa unavyowaka ili kuhakikisha jamii inayowazunguka inapata huduma na mafanikio kupitia utawa wao.
Askofu Kastory Msemwa wa Jimbo la tunduru Masasi akiendesha Misa takatifu katika uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Masista wa Mtakatifu Agness Chipole.
Ibada ya Jubilei iliambatana na Matoleo kama shukrani kwa kutimiza miaka yote 75 katika hali ya amani na utulivu. Waumini wakimtolea Mungu sadaka ya Shukrani. |
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Askofu Damikan Daniel Dalu akiongoza mamia ya watawa na wananchi waliojitokeza kuja kusherekea uzinduzi wa Jubilei nje ya kanisa Chipole mara baada ya ibada.
Wanajubilei wakitoka ndani kastika jumba lao kuelekea kuungana na wenzao katika Maandamano ya Maadhimiksho ya Misa takatifu ya uzinduzi wa Jubilei.
Mapadre wa makanisa mbalimbali waliokuja kuwaunga mkoano watawa wenzao masista wa Mtakatifu Agness, muda mfupi kabla ya Ibada kuanza.
Maandamano ya kuelekea Kanisani katika Ibada ya Uzinduzi wa Jubilei ya Mika 75 ya Shirika la Masista wa Mtakatifu Agness iliyofanyika Chipole Songea Vijijini ambayo kilele chake kitakuwa Mwezi jun mwaka 2016.
Sr. Karista Soko OSB akifurahia maisha ya ukristu ndani ya mikaka 50 ya utawea ambapo amejifunza mengi na kuvuka vikwazo vingi na kuvumilia.
Sr Flora Komba OSB kutoka Shirika la Mtakatifu Agness Chipole akionekana kwa hekima ya aina yake mara baada ya ibada ya Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika ambayo imeambatana na Jubilei yake ya miaka 25 ya usista.
Masista wakiwa wamependeza na wanang`aa kuashiria usafi wa mioyo na tabia kama ambavyo wengi wana amini, wametakiwa kuthubutu kujitoa hata katika nafasi za juu za uongozi ikiwemo Urais kwa kuwa wana uwezo na karama ya aina yake kama ambavyo wanaendesha mashirika yao kwa misingi ya Utawala Bora.
Masista wakifurahia Utawa na kutamani na wao kufikia Jubilei ya Miaka 25 na zaidi kama wakubwa wao walivyowatangulia.
Masista wakipokea Baraka ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Yesu Kristu aendelee kuwa nao katika maisha yao ya utawa.
Mhashamu Askofu Msemwa wa Jimbo la Tunduru Masasi akiongoza Ibada ya Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Mtakatifu Agness kwa Mwaliko wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Mhashamu Askofu Damian Daniel Dalu.
Masista katika Ibada ya Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Shirika la Mtakatifu Agness iliyofanyika Shirikani katika Kijiji cha Chipole Songea Vijijini Mkoani Ruvuma na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi waliotoka maeneo mbal;imbali ya Mkoa wa Ruvuma.
Waumini wakishuhudia matukio yaliyokuwa yanaendelea katika Ibada ya Uzinduzi wa Jubilei.
Abate wa Peramiho Abate Anastasius Anastasius akikwapongeza Masista waliopata Jubilei katika Maisha ya kitawa na kuwatakla kuendelea kumtegemea Mungu kwa kuwa wao wana vipaji na karama nyingi ambazo zinajidhihirisha katika maeneo mbal;imbali ambamo masista wamesambaa kufanya kazi mbalimbali wakiwemo mainjinia, waalimu, mafundi ufundi wa aina mbalimbali wapo maeneo mengi kuhudumia jamii.
safi sana....
ReplyDelete