Wananchi wa Kata ya Majimaji wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakieleza kero zao kwa viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Mkoa wa Ruvuma wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kusahauliwa katika fursa mbalimbali zinapotokea mkoani ikiwemo miradi ya TASAFU ya kaya Maskini.
Wananchi wa Kata ya Majimaji wakiwa katika Mkutano wa hadhara wakati wa Ziara ya Mwenyekiti na Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma.
Wazee wa Wilaya ya Tunduru wakiwa katika Mkutano wa Hadhara na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu muhagama katika viwanja vya Baraza la Idi mjini Tunduru.
Kijana Msanii mwenye kipaji cha uimbaji wa nyimbo za muziki wa HIP HAP Juma Selemani kutoka kijiji cha Mnenje Kata ya Majimaji mwenye micro phone masikioni mara baada ya kutumbuiza.
Washereheshaji wa Mkutano wa hadhara wakitumbuiza katika mkutano wa hadha uliofanyika kijiji cha Majimaji Kata ya Majimaji Mkoani Ruvuma. Watoto wa kike wanaaswa kuzingatia masomo.
Wilaya za Tunduru na Namtumbo ndizo zinazoongoza kwa kushuka kiwango cha Elimu kutokana na Tatizo la Mimba za Utotoni zinazosababisha watoto wengi kukatiza masomo.
Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja akihutubia wananchi wa Wilaya ya Tunduru, amewaomba wana CCM kudumisha upendo kwa wapinzani ili waweze kuwashawishi kurudi CCM, amesema Mpinzani asigeuzwe adui awe rafiki wa karibu itasaidia kujua hali ikoje. Amesema pia wana CCM waache tabia ya kuwa ukimuona mwana CCM amesimama na mpinzani basi naye anatuhumiwa kuwa ni Mpinzani.
Wajumbe Ukumbini Baraza la UWT Tunduru.
Wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Tunduru wakiwa ukumbini katika mkutano wa Baraza la UWT walipotembelewa na Viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka Mkoani.
Mwaasisi wa UWT Wilaya ya Tunduru Bibi Husna Makanji amewaomba wakina mama wa UWT kuilea Jumuiya ya UWT na kuilinda kwa kudumisha umoja na mshikamano, waache malumbano yasiyo na faida yataifanya kuiua Jumuia badala ya kuiendelea. Amesema katika Jumuiya za chama cha Mapinduzi jumuiaya ya akina mama ndiyo Msingi wa Chama ikiyumba jumuiya hiyo chama hakiwezi kwenda vizuri.
Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Tunduru wakiwa katika Ukumbi wa UWT wilaya ya Tunduru.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru kaskazini Eng Ramo Makani amesema ni jukumu la wananchi kuwapima wagombea kwa yale waliyoyafanya na sera zao kuangalia ukweli uko wapi, wasichague kwa ushabiki.Amesema akina mama ndio Jeshi linalotegemewa katika kutengeneza Dola wanapaswa kuwa makini na wagombea wanaojitokeza.
Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Tunduru Mariam Msongela akiwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamedi Masanja nje ya ofisi za UWT wilaya ya Tunduru wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa kutembelea Mabaraza ya Wilaya.
Pamoja na yote pia wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura wakati ukifika wasiuze shahada watimize haki ya msingi ya kikatiba.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Eng Ramo Makani akiwa Ofisini kwake Jimboni Tunduru.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu muhagama amewatahadharisha wanawake kuwa makini katika kuchagua viongozi waadilifu wakati ukifika wa uchaguzi wa Wabunge na Madiwani mwezi Oktoba. Amesema ni vizuri kumchagua mtu atakayewasaidia wananchi, mwenye kushiriki katika kutatua matatizo ya waliomchagua.
Wanachama wa UWT Mkoa wa Ruvuma wakifurahia elimu ya Ujasiliamali katika Kikao cha Baraza la kawaida cha Viongozi wa UWT Wilaya ya Namtumbo na Uongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni Diwani wa Viti Maalum Remina Nchimbi.
Mjumbe wa UWT Taifa na Mjumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma Doto Nyirenda akitoa Elimu ya Ujasiliamali kwa akina Mama wa UWT Wilaya ya Namtumbo. Amesema wakati umefika sasa ni lazima siasa zetu ziendane na uchumi kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Chama cha Mapinduzi na katika Halmashauri zetu.
Amesema wakina mama wakifanya hivyo kwa kubuni miradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi itasaidia kuongeza wigo wa soko la ajira, ujasiliamali unapunguza tatizo la ajira.
Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wamehaidi kukipa ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi ujao.
Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja amesema
utakuta Idadi ya wanawake katika Maeneo mbalimbali ni kubwa kuliko wanaume,
lakini wanapogombea uongozi wanaume hutia fitina ambayo inawafanya wanawake
wasimchague mwenzao tabia ambayo si njema iachwe mara moja ili na wanawake wapate fursa ya kushika hatamu ya uongozi katika ngazi mbalimbali .
Katika ziara hiyo ya viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma kikubwa wanawaasa wanawake kupendana na kuchaguana popote anaposimama mwanamke kugombea wengine wawe mstari wa mbele kumuunga mkono mwanamke mwenzao.
Nao Vijana wa UVCM kupitia vyuo vikuu wamewasisitiza wanawake kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kuwasomesha watoto wao ili waje kuwa viongozi wa Ngazi za Juu, wamesema Mkoa wa Ruvuma ni Miongoni mwa mikoa yenye bahati ya kupata viongozi mahiri wanaosimamia ipasavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha Maendeleo yanapatikana Mkoani Ruvuma.
Wanasema Ruvuma hivi sasa kuna Vyuo vikuu Vivyopungua vitatu lakini itashangaza kuona wengi wanaosoma katika vyuo hivyo ni waja ambao si wazaliwa wa Mkoa huo ni wajibu wa Jumuia ya UWT kwa kushirikiana na wadau wengine wa Elimu mkoani hapa kutoa msukumo wa vijana wao kupenda kujiendeleza kielimu. (Picha hiyo juu ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Ruhuwiko Songea)
Viongozi wa UWT wilaya ya Namtumbo, kulia mwenye kitenge ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Namtumbo Bi Maria Hamisi Kapinga.
Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Masanja amewataka wanaume
kuwaunga mkono wanawake wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya
kuwachonganisha ili wasielewane na kushindwa kuwachagua wanawake wenzao katika
Uongozi.
Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Masanja ameyasema hayo
akiwa katika Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini wakati wa Ziara ya kuzungukia Mabaraza ya Wanawake wa UWT katika wilaya zake
tano.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu Muhagama amesisitiza Jamii kuacha tabia ya kuwaoza watoto katika umri mdogo kufanya hivyo ni kuwanyima haki ya kupata elimu.
Ziara ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma imelenga kuwapa hamasa
wanawake kugombea katika viti mbalimbali kuanzia mitaa hadi Taifa .Pamoja na
kutoa elimu ya ujasilia mali
il wanawake waji kwamue katika
umasikini .
Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph Computer Enginiaring ambao pia ni wanachama wa UV CCM wakiwa katika kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini.
Katibu wa UWT Wilaya ya Songea Vijijini Selina Ngonyani akiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Mama Nguluse uliopo viwanja vya Nane nane Mjini Songea muda mfupi kabla ya kuanza Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini
Wajumbe wa UWT wilaya ya Songea vijijini wakiwa katika Mkutano wa Baraza la UWT wilaya walipotembelewa na viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma,
Kuruthumu Muhagama amewataka wanawake kushawishi jamii ili iweze kuwasomesha
wanawake, mtoto wa kike akielimika anaweza kuwa mkombozi katika familia. Ameyasema hayo wakati akiwa ziarani wilayani Tunduru katika kutembelea mabaraza ya UWT wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment