Wataalamu wa Afya na Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Masuala ya Wazee wana wajibu wa kuhakikisha wazee wanahudumiwa ipasavyo kiafya na kuwawezesha kiuchumi katika kila fursa zinazotokea kwenye halmashauri zao.
Wataalamu wa Afya na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Wakuu wa Idara wakiwa katika Kikao cha pamoja cha Wazee wa Baraza Huru la Wazee kutoka Halmashauri ya Songea na Manispaa wakijadili changamoto na zinazowakabili wazee katika maisha ya uzee na kuzeeka na kuweka mikakati ya kuziondoa changamoto hizo.
Wadau wa Masuala ya wazee wameliomba Jeshi la police kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaosababisha mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina. Hayo yamejitokeza katika Semina ya kujengea uwezo wa masuala ya wazee inayoendeshwa na Shirika la kuhidumia Wazee la PADI baada ya wazee wawili kufa kwa kusadikiwa kuwa wamekunywa dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu kwa lengo la kuwatoa uchawi.
Wataalamu kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya Songea wakiainisha mahitaji ya wazee na kuyapangia mikakati ya kuyatekeleza kupitia mifuko mbalimbali ndani ya idara zao.
Washiriki wa Mafunzo ya kujadili changamoto zinazowakabili wazee na namna ya kuzitatua kwa kutumia Rasilimali zilizoko katika Halmashauri Mafunzo yaliyoendeshwa na Shirika linalohudumia Wazee la PADI kwa ufadhili wa Help Age International. Katika Ukumbi wa Unangwa Manispaa ya Songea.
Wazee wa Mabaraza huru ya Wazee kutoka Halmashauri za wilaya ya Songea na Manispaa wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kuitungia sheria Sera ya Wazee ya Mwaka 2003 ili iweze kuwasaidia wanaponyimwa haki zao waweze kudai kwa kutumia sheria hiyo.
Wazee Mkoani Ruvuma kupitia Mabaraza huru ya wazee wameziomba taasisi za kifedha na Halmashauri kuwakopesha na wazee pindi mafungu yanapotokea kwa kuwa wapo wenye uwezo wa kumudu kufanya biashara ndogo ndogo na kujiingizia kipato, wamesema wao hawawezi kutoroka kwa kuwa umri wao hauwaruhusu kuhangaika.
Wazee wamesema changamoto zinazowakabili ni kutelekezewa wimbi kubwa la wategemezi au wajukuu wakati kipato chao ni kidogo wameiomba Serikali iwapatie Pensheni kwa wazee ili iweze kuwasaidia kuishi vizuri na wategemezi wao.
Watoa huduma za Afya kutoka Hospitali za Taasisi za Dini za St. Benedict Matogoro na St. Camilius Songea zilizoingia Mkataba na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuwachangia wazee gharama za matibabu kutoka katika hospitali hizo.
Wazee wanaonufaika na Mikopo inayotolewa na Shirika la kuhudumia Wazee la PADI wameweza kununua mifugo na kufuga kuku, mbuzi na kulima bustani na kufanikiwa kurejesha mikopo hiyo kwa asilimia 99%
Mzee akitafakari hatma ya maisha ya uzeeni.
Mkurugenzi wa Shirika la PADI linalohudumia wazee Tanzania Iskaka Msigwa akihakikisha kila mdau anapata elimu sahihi ya uzee na kuzeeka na kutambua changamoto zinazowakabili wazee ili kushirikiana katika kuzitatua hatimaye Wazee waishi maisha salama na ya amani.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbazli nao hawakuachwa nyumana Shirika la PADI katika kuhakikisha wanapata Elimu ya Uzee na Kuzeeka ili waweze kuielimisha jamii kuachana na mila potofu za kuona kuwa wazee ndio wanaohusika na ushirikina. Waandishi wakiwa katika Ukumbi wa Unangwa Manispaa ya Songea.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Bw. Amon Mtega wa Songea akifurahi kupata uelewa juu ya changamoto zinazowakabili wazee katika maisha ya uzee.
Wakuu wa idara wa halamashauri ya Manispaa ya Songea baada ya kujengewa uwezo na uelewa juu ya masuala ya wazee na stahiki zao kupitia Shirika linalohudumia Wazee tanzania la PADI lenye makao yake Makuu Manispaa ya Songea sasa wameanza kutenga bajeti ya kulipia kadi za CHF kwa ajili ya matibabu ya wazee kwenye hospitali za Serikali na Hospitali binafsi za Mtakatifu Benedict Matogoro na ya Mtakatifu Camilius Songea.
Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea wakiwa katika kikao cha Baraza Huru la wazee wa Manispaa ya Songea na Halmashauri ya wilaya wakipanga mikakati ya kuboresha Maisha ya Wazee kupitia vyanzo mbalimbali vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Wazee wakitafakari jinsi ya kujikwamua na mauaji ya wazee yanayoendelea Nchini kutokana na Imani za kishirikina katika viwanja vya Ukumbi wa Unangwa Songea Boys Manispaa ya Songea. Aliye kulia mwenye Suti ni Mkongwe wa habari Adam Mzuza Nindi na Mmiliki wa blog hii.
No comments:
Post a Comment