Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabiti Mwambungu ameongoza zoezi la usafi kuadhimisha sherehe za Uhuru kwa
kufanya usafi Soko kuu la Manspaa ya Songea, Stand ya Mabasi Songea,Hospitali
ya Mkoa na Mahakama kuu.Akishirikiana na Jeshi la Wananchi,Police Wafanya biashara na Wananchi wa kawaida
Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma amepiga marufukukwa mtu yeyote kutupa taka taka ovyo katika manspaa ya
Songea ,Mtu yeyote atakaye patikana akivunja amuri hiyo atapigwa faini au
kwenda jela.
Mkuu wa wa Mkoa wa
Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameya sema hayo kati wa kuazimsha sherehe za
uhuru zilizo fanyika Mkoani Ruvvuma kwa kufanya usafi katika maeneo ya
Stand Kuu,Hospitali,na Soko kuu la
manspaa ya Songea.
Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wakishiriki katika usafi
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee akikabidhi risala kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ili awakilishe kwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Said Thabiti Mwambungu amesma pamoja na na kutii amuri ya Rais wa Jamuhuri
ya Mungano wa Tanzania Mh John Pombe Maguli .Lakini maswala mengine inabidi
tujiwekee utaratibu wenyewe kama watu
kukojoa ovyo hadharani ,kutupa makopo ya maji pamoja na karatasi za vyocha amesema mtu yoyote atakaye kamatwa atatozwa faini ya
shilingi 50,000/= au kwenda jela
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akikagua usafi katika Maeneo Mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma
Jeshi la Police Mkoani Ruvuma likishiriki katika usafi siku ya Sherehe za Uhuru
Watu walio shiriki zoezi la usafi kwa mujibu wa Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wakipiga Picha na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuvuma
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Manspaa ya Songea akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu kulia ni Diwani wa kata ya Mjini Chitete
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Magret Malenga akiongoza zoezi la usafi katika Maeneo ya Vitongoji na vijiji vya Wilaya ya Nyasa. Pichani ni wananchi na OCD wilaya ya Nyasa SSP Amiri Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Magret Malenga amewaagiza Viongozi wa Vitongoji wa Kata na Mabalozi kusimamia zoezi la usafi katika maeneo yao na kufanya suala la usafi liwe endelevu ambapo kila tar 9 ya mwezi katika wilaya hiyo kutakuwa ukaguzi wa kuangalia maendeleo ya usafi katika kujinusu na maradhi ya milipuko katika wilaya hiyo.
Wananchi katika Ufukwe wa MbaMbabay wakifanya usafi katika maazimisho ya sherehe za Uhuru na Jamhuri wilayani Nyasa.
Hapo ni katika eneo la mwambao wa Ziwa Nyasa foroza ya Mbamba Bay wachuuzi wa ziwa Nyasa wakiongozwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa katika zoezi hilo kwa wilaya ya Nyasa ambalo lilizinduliwa tar 2 na mkuu wa wilaya ya Nyasa kwa kutembelea katika Hospitali za wilaya na katika mialo ya ziwa Nyasa ambako wavuvi wamepiga kambi kuhamasisha usafi na ujenzi wa vyoo.
Hapo ni katika Foroza ya Njambe wilayani Nyasa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akishirikiana na wachuuzi katika usafi siku ya Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Uhuru ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Magret Malenga akipokelewa na Wananchi wa Wilaya ya Nyasa mara baada ya kukamilisha zoezi la Usafi katika viwanja vya Stend ya Mbamba Bay wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya akiwa ameambatana na msafara wa wilaya ya Nyasa katika zoezi la usafi katika Kijiji cha Kihagala Kata ya kihagala wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.
Afisa mazingira wa wilaya ya Nyasa akikagua vyoo vya wananchi kadiri ya agizo la mkuu wa Wilaya ya Nyasa la kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kila mmoja ahakikishe anakua na choo na maeneo yanakuwa safi kujikinga na maradhi.
Mkuu waa wilaya ya Nyasa Magret Malenga amesema kiongozi atakayerudi nyuma katika kusimamia utekelezaji wa suala la usafi atachukuliwa hatua za kisheria kwa kutowatumikia wananchi.
Wafanyakazi wa Bank ya NMB baada ya kufanya usafi katika benk hiyo ya Songea
Hapy na Anna wa NMB wakiwa na furaha baada ya kukamilisha Amuri halali ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh .John Pombe Magufuli ya kumutaka kila mmoja afanye usafi
Ni Anna na Hapy wakitoa pozi la usafi huku wakisema nani kama Rais Magufuli usafi ni moja ya kanuni ya akina mama ,mama na usafi ni sawa na samaki na maji Hongera Anna na Hapy
Mzewe wa miradi leoi hii hana jinsi ana piga miradi ya usafi
POLICE walikuwa hawako nyuma katika usafi hapo wapo katika maeneo ya Sekondary ya Wasichana Songea
Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wamemwomba Rais wa Jamuhuri ya
Mungano wa Tasnzania John Pombe Magufuli kuitungia sheria sera ya wazee ya
mwaka 2003 pamoja na kuharakisha pesheni kwa wazee ili kunusuru maisha
yao.wadau wengine wamesema mwaka 1961 kauli mbiu ili kuwa uhuru na kazi hivyo
kufanya kazi ni moja ya kauli mbiu ya mwaka1961wakati tukipata uhuru
No comments:
Post a Comment