Katika Ziara yake pia Mh. Joseph Mwagama ameweza kugawa
Pikipiki 3 pamoja na Baiskeli kwaajili ya mlemavu na Baiskeli nyingine kupeleka katika kituo cha Afya Madaba.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph
Mwagama kufanya ziara jimboni kwake toka alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la
Madaba ambalo ni jimbo jipya.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama akiendesha Pikipiki
Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama akiendesha Pikipiki
Mbunge wa Jimbo la
Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama amesema njia rahisi ya kuwainua
Wananchi ni kutafuta mazao ambayo wakiuza yanaweza kutatua matatizo yao kwa haraka.
Mbunge wa Jimbo la
Madaba ameyasema hayo wakati akigawa Tani sita za mbegu ya Tangawizi zenye
thamani ya Shilingi Milioni 21 kwa wakulima wa Jimbo la Madaba ili wajiandae
kulima zao la Tangawizi ambalo tayari limeshapata soko Nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito Mhagama amesema Mazao ambayo yanaonyesha kuwainua wananchi kiuchumi ni kazi ya Viongozi kuwahimiza Wananchi kulima mazao hayo, kama Mbaazi, Aliseti, Maharage na Tangawizi
Mratibu wa Shirika la RUCODIA Ladislaus Bigambo amesema
shirika lilianza na wanachama wakulima 300 lakini mpaka sasa wamefikia wakulima
2745, mbegu zilizopandwa wakati huo zilikuwa kilo 10 lakini sasa kuna Tani
9000.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama akianisha miradi ambayo ana taka kuitekeleza katika jimbo la madaba huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Madaba Robeti Mageni
Wananchi wa Jimbo la Madaba wakipokea misaada hiyo
wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kulenga katika kuinua uchumi wa mtu
wa kati kwa kutoa mbegu za Tangawizi na vitendea kazi.
Wamesema kukiwepo na Rasilimali Ardhi na watu wakipewa
nyenzo Tanzania haikuwa
miongoni mwa Nchi zinazolalamika na umaskini kwani mito
ipo, maziwa yapo pamoja na mvua za kutosha, wamesema hivi sasa Tangawizi ya Tanzania inatakiwa sana
Nchini Kenya
pia baada ya kuipima imeonyesha ina ubora haina sumu ya kuweza kuwadhuru
Binadamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Madaba akipokea Mbegu za Tangawizi kwa Mh.Joseph Kizito Mhagama
Mbunge wa Jimbo la Madaba Songea Vijijini Joseph Kizito
Mhagama amesema Mazao ambayo yanaonyesha kuwainua wananchi kiuchumi ni kazi ya
Viongozi kuwahimiza Wananchi kulima mazao hayo, kama
Mbaazi, Aliseti, Maharage na Tangawizi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Madaba Robeti Mageni akiwa ameshika Tangawizi huku akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutoa Tani 6 Zenye Thamani ya Shilingi milioni Ishirini na Moja
No comments:
Post a Comment