Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge alipotembelea Taasisi ya Kihuma kuona shughuli za Maendeleo akiwa na Dr Matomola katikati Mkuu wa Taasisi ya KIUMA na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko. Dr Matomola ameomba Rais kutembelea kwenye Taasisi yake katika sherehe za jubilei ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Dr matomola akielezea namna wanavytoa mchango wa maendeleo kupitia Taasisi yake ya KIUMA wilayanik Tunduru ambayo inatoa Elimu kuanzia ngazi ya Sekondari Chuo cha Ufundi Stadi Veta na Chuo cha Wauguzi ambapo inahusisha na utoaji huduma za Afya kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru.
Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa kufikisha ujumbe Serikali wa kuomba kupatiwa mkoas wa SELUU ili kusogeza huduma karibu kwa Wananchi kuliko sasa ambapo kutoka tunduru hadi Makao makuu ya Mkoa ni umbali wa KM 280.
Jamii ya Wafugaji waliopo eneo la Mtina wilayani Tunduru walipotembelewa katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wametakiwa kuhama eneo hilo kwa kuwa ni eneo la Hifadhik ya Seluu Serikali inawatafutia Eneo la kuhamia.
Jamii ya Wafugaji walioko Kijiji cha Mtina wanafuga Ng`ombe zaidi ya 1500 ambapo pana familia zaidi ya 500 kutoka kwenye jamii hiyo ya wafugaji. Wafugaji hao wameomba ma Afisa Mifugo kuwatembelea na kuwapa Elimu ya ufugaji wa Kisasa na ushauri mbalimbali katika ufugaji.
Mkuu Mkoa wa Ruvuma akihutubia Wananchi wa Kijiji cha Matemanga aliweza kubaini kero ya Maji na kusua sua kwa Miradi ya maji inayoendelea wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma DR Binilith Satano Mahenge katika Ziara hiyo wilayani Tunduru aliweza kubaini
Jumla
ya Miradi kumi ya Maji iliyogharimu kiasi cha Shilingi
4,462,364,220.00 ambayo haikumridhisha utekelezaji wake.
Katika Ziara hiyo pia aliweza kukagua ujenzi wa Barabara ya Tunduru - Songea kwa kiwango cha lami ambayo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake inayotarajia kukamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.
Hiyo ni sehemu ya ujenzi wa Barabara hiyo katika daraja la Mto Nampungu yenye urefu wa mita 100 kama inavyoonekana wakati mkuu wa mkoa Dr Mahenge na Msafara wake wakikagua ujenzi wa Barabara.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akiwa katika Mto Nampungu ambako ujenzi wa Daraja kubwa unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Mahenge akiwa katika Kijiji cha Lukumbule ambako kuna Mradi wa Maji unaendelea akielekea kwenye Matanki ya maji kukagua hali ya maendeleo ya ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa akimba maelekezo ya namna ulivyotekelezwa mradi huo wa maji katika Kijiji cha Lukumbure.
Tanki la Maji katika Mradi wa Lukumbule
uliogharimu kiasi cha Shilingi 475,472,151 ambao
umefikia Asilimia 95% .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge akikagua Mradi huo
alilazimika
kupanda juu ya Tank la Maji kujua uimara wa Tank hilo kama anavyoonekana hapo juu.
Mkuu
wa Mkoa katika ziara hiyo amebaini uzembe ulio fanywa na wahandisi wa Maji wilaya ya Tunduru kulipa fedha bila kufutilia
miradi hiyo na kupelekea miradi 9 kutokamilika wakati fedha zake zimetoka, kutokana na hilo amelazimika kuunda tume ili kujua jinsi zilivyotumika fedha za miradi hiyo.
Wananchi wa Wilaya ya Tunduru wamemuomba Mkuu wa mkoa wa ruvuma kuwafuatilia watendaji wake kujua namna wanavyowatumikia wananchi ambapo amewataka wananchi kuwa watulivu yeye atahakikisha maji yanapatikana Tunduru na hatua zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhujumu miradi ya maji.
Wananchi wajasilikamali wa wsilaya ya Tunduru wakifurahia kutembelewa na Mkuu wa Mkoa kubaini kero zao huku wakiwa na imani ya kusimamiwa na kuhakikisha wanasonga mbele kwa kuinua uchumi wilayani humo.
Mjasiliamali tina wilayani Tunduru
Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Dr. Mahenge pia alitembelea Kiwanda cha kubangua Korosho kilichopo wilaya ya tunduru kuona hali ya uendeshaji wa kiwanda hicho na changamoto zinazojitokeza.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma DKT Binilith Satano Mahenge alipopewa
Taarifa ya Miradi ya maji na Kaimu
Mhandisi wa Maji wilaya ya Tunduru Michael Kasangano aligunduwa kutolewa kwa Kiasi cha
Shilingi 1, 983,584,119.90 fedha
ambazo zimechukuliwa pasipo kufanyika kazi katika baadhi ya Maeneo ya Miradi ya maji.
Katika ziara hiyo imebaini
miradi mbalimbali ya maendeleo ime kuwa na usimamizi hafifu na kuitia hasara
serekari kutokana na uzembe wa Wakuu wa idara