Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Ruvuma Joel Mbewa akikabidhi taarifa ya uchaguzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge ikiwa ni ishara ya kumalizika kwa shughuli za uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika ukmbi wa mipango Mkoa wa Ruvuma kupokea nakala za Taarifa ya uchaguzi mkuu ili kupeleka katika vituo ambavyo wananchi watapata fursa ya kusoma taarifa hiyo.
Dr. Binilith Satano Mahenge akikagua Nakala ya Taarifaaada ya Uchaguzi mkuu mara baada ya kupokea maelezo yha hali ya uchaguzi ulivyoendeshwa katika Mkoa wa ruvuma kutoka kwa Mratibu wa Mkoa wa ruvuma Bw Joel Mbewa.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Binilirt Satano Mahenge akipokea taarifa hiyo amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taifa, amesema kupatikana kwa taarifa ya uchaguzi kuna maanisha uchaguzi sasa umekwisho kilichob aki ni kazi tu na siyo siasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akikabidhi nakala za Taarifa ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Songea Mjini ambaye ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Naftal Saiyoloy
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea Vijijini Wenselia Swai akipokea nakala za Tgaarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Dr Mahenge kwa ajili ya wanachi wa Eneo lake.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Mr Fungo akipokea Taarifa hiyo ili kuiwasilisha kwa wananchi wa Jimbo la Madaba waweze kuipitia. Kupatikana kwa taarifa hizo ni kuashiria uwazi wa Tume ya Uchaguzi kwa wanachi kufikia taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment