Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Rajabu Mtiula
amesema kwa kiasi kikubwa wadau mbalimbali wameweza kuchangia kukabiliana na
upungufu wa madawati kati ya watu waliochangia ni pamoja na Mbunge wa jimbo la
peramiho Jenista Mhagama pamoja na Madiwani ambao wamechangia Madawati 60.
Halmashauri nya
Wilaya ya Songea yenye wanafunzi 28,045 kwa Shule za msingi na wanafunzi
3706 wa Shule za Sekondari imeweza
kukabiliana na upungufu wa Madawati Madawati 13,013 yanayohitajika hadi
kubakiwa na upungufu wa Madawati 301.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai, amewashukuru wadau wote waliowezesha
kufanikisha zoezi la Madawati katika Halmashauri Songea vijijini.
Afisa Elimu Shule za Msingi Tanu Kameka ameelezea jinsi ya upungufu
wa Madawati ulivyo na kuweka Mikakati ya
kukamilisha upungufu huo hadi kufikia mwezi wa 7 mwaka huu.kuta kuwa hakuna
upungufu tena
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini ambayo imebakiwa na
upungufu wa Madawati 301 katika Bajeti yake ya 2016/2017 imetenga shilingi
milioni35 ili kumaliza tatizo la upungufu wa Madawati.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Juma Ally amesema juhudi
za Serikali pamoja na wananchi zime weza kufanikisha kutatua tatizo la Madawati.
Kazi kubwa kwa wanafunzi ni kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waje walete
maendeleo katika Jamii.
No comments:
Post a Comment