Waziri wa Kilimo Mifugo
na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba ametoa
agizo hilo baada ya kuangalia muda maalumu wa kununua Mahindi kwa wananchi na
kugundua muda wa kuanza ununuzi unachelewa hadi mwezi wa nane kwa kusubiria Mahindi yakauke jambo linalopelekea
wananchi kuamua kuuza mahindi kwa hasara kwa wafanyabiashara wadogo kwa shilingi 250 hadi 350 badala ya bei ya
kitengo ya shilingi 600
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Dr Tizeba amesema sasa hivi kila jambo linakwenda kwa teknologia ya kisasa muda wa kutegemea jua kukausha mazao
umepitwa na wakati. Jambo la muhimu ni kitengo cha kuhifadhi nafaka kuwa na
mashine ya kuweza kukausha mahindi jambo hilo litaweza kumkomboa mwananchi kwa kuuza mazao yeke kwa muda
Mwafaka.
Waziri wa Kilimo pia amekemea suala la
mahindi kuwa na daraja la chini wakati kitengo kina maghala ambayo yana ubora wa kisasa, akieleza hasara waliyoipata Serikari mwaka jauzi amesema zaidi ya tani 8000 zilikuwa na daraja la chini na
mahindi hayo yalilazimika kuuzwa kwa shilingi 350 badala ya kuuza shilingi 600
kwa kilo .amesema jambo hilo hataki kusikia tena.Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Nchini Tanzania Dr Charles John Tizeba katika ziara yake mkoani Ruvuma amewahimiza wananchi kulima mahindi kwa wing ili kukabiliana na hali ya hewa
Amesema nyanda za juu
kusini zitaendelea kuwa na mvua nyingi, hivyo mahindi
watakayozalisha mwaka huu yatakuwa na soko kwa kuwa soko la mahindi ni kubwa.
Waziri wa
Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba amesema Mawakala waliokuwa
wakisambaza Pembejeo za Kilimo Nchini Tanzania wamechelewa kulipwa fedha zao kutokana na madai yao ya malipo yenye
thamani ya shilingi bilioni 5.1 kupishana na hali halisi ambayo ni shilingi
milioni 238, Waziri amesema Serikali ingapata hasara kwa kuwalipa mawakala
kiasi cha shilingi bilioni 4.1.
Waziri wa
Kilimo Mifugo na uvuvi Dr Charles Tizeba amesema baada uhakiki na kubaini
Malipo halali Serikali itanza kulipa Malipo halali yaliyobainika baada ya
uchunguzi wa kina kwa kuhoji kila mtu aliyepata ruzuku ya pembejeo.
Waziri wa
Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba akizungumzia suala la ununuzi
Mahindi kupitia Hifadhi ya Chakula amesema Serikali iliweza kuidhinisha ununuzi
wa Mahindi Tani 22,000 lakini Tani zilizonunuliwa Hifadhi ya Kanda ya Songea ni
Tani 10,000.
Waziri wa
Kilimo Dr Charles Tizeba amesema sababu ya kupata Tani 10,000 imetokana na soko
kukua, Hifadhi ya Chakula ilikuwa ikinunua kwa bei ya shilingi 580 kwa kilo
vijijini na mjini kwa kilo shilingi 600 lakini hata hivyo wafanya biashara
waliongeza na kununua kwa shilingi 680 kwa kilo jambo lililowapelekea wakulima
kukimbilia kuuza mahindi yao kwa wafanya biashara. Jambo ambalo Serikali
imefurahia kwa kuona Mkulima anafaidika na Kilimo na hiyo ndiyo shabaha ya
Serikali kutaka kumuokoa mkulima.
Amesema huu
ni uzembe wa wasismamizi katika vitengo vya Hifadhi amesema hataki kusikia
suala la mazao kuwa chini ya kiwango (under grad) endapo suala hilo litatokea
tena basi Mkuu wa Kitengo atakuwa amejifukuza kazi.
Waziri wa
Kilimo Mifugo na uvuvi akifafanua kuhusu suala la vitengo kuchelewa kuanza
msimu wa ununuzi wa mazao yakiwemo
mahindi hadi mwezi wa nane kwa madai ya kusubiri unyaufu , Waziri Tizeba
amesema baada ya teknolojia za kisasa
kuongezeka hakula sababu ya kusubiri jua likaushe Mahindi, bali vitengo vya
Wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa vitafute mashine ya kakaushia mahindi ili
wananchi mara wanapovuna waweze kuvuna mara moja badala ya kukaa zaidi ya miezi
mitatu wakisubiri kufunguliwa kwa magulio maagizo hayo yameenda sambamba na
kuanza kwa gulio la Tumbaku.
Waziri
wa Kilimo Mifugo na uvuvi Dr Charles Tizeba amesema kiongozi yeyote
atakayesababisha kuteremka kwa daraja la Mazao yanayozalishwa na wananchi
kuteremka baada ya kuingizwa ghalani basi kiongozi huyo atakuwa amejifukuza kazi
Waziri wa
Kilimo akiongelea kuhusu suala la Ruzuku za Pembejeo za kilimo amesema mfumo wa
ruzuku hauwezi kukwamua changamoto za kilimo amesema jambo la muhimu ni
Serikali kushusha bei za Pembejeo kwa kuagiza kwa wazalishaji badala ya kununua
kwa madalali, akitoa mfano amesema pembejeo imeteremka kwa asilimia 38% kwa
sasa mfuko wa mbolea unauzwa kwa shilingi 48,000 Serikali inafanya jitihada
pembejeo iweze kuteremka hadi iuzwe kama inavyouzwa sukari.
Dr. Tizeba akiwa Mkoani Ruvuma aliweza kutembelea Maghala ya watu binafsi na
Maghala ya Serikali na kuona hali ya chakula na kuridhika kutokana na chakula
kilivyo katika Maghala hayo.
Waziri amewaomba
wanaouza chakula kwenda sambamba na kipato cha mtanzania bila kusababisha mfumuko
wa bei ambao mtu wakawaida atashindwa kununua chakula hicho
Waziri wa Kilimo katika Ziara hiyo alitembelea soko la mazao la Manzese na kuongea na wananchi na wafanyabiasha ya mazao wa soko hilo lililopo Manispaa ya SongeaWaziri wa Kilimo Dr Tizeba akiongea na wafanyabiashara wa SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Waziri wa Kilimo aliwatembelea wafanya biashara hao kujua changamoto zinazowakabili katika zao la Mahindi.
Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi akiwa ziara katika manispaa ya Songea kusikiliza kero za wakulima katika msimu huu wa kilimo
Waziri akifafanua kwa wakaazi wa Manispaa ya Songea juu ya Malengo ya wizara ya kilimo katika kumsaidia mkulima aweze kulima kwa tija
Wafanyabiashara wa Soko la SODECO Manzese wakimsikiliza waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi alipowatembelea katika eneo lao
Waziri Mkuu aliweza kutembelea wafanya biashara ya Mahindi wenye maghala binafsi
Waziri na Wakulima Manzese Soko la SODECO Manispaa ya Songea
Wafanya Biashara ya mazao katika soko la SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Waziri Tizeba akihoji juu ya Ununuzi wa Mahindi kwa wafanya biashara wadogo
Ghala la Mtu binafsi Mtakanini wilayani Namtumbo ambalo alilitemb elea waziri wa Kilimo kuona namna waavyohifadhi mazao yao.
Waziri wa Kilimo akiongea na Mfanya Biashara ya mazao Mzee Alfani mwenye akiba ta Tani 80 za Mahindi ambaye ameagiza wataalamu kumsadia utaalamu wa jinsi ya kuhifadhi mahindi yasiharibike.
Waziri akishauri njia bora za kuhifadhi nafaka na kuzifanya zisiharibike amesema zisipohifadhiwa kitaalamu wafanyabiashara watapata hasara.
Waziri akiwa Nyumbani kwa Mzee Yasini mfanya Biashara wa Mahindi katika Kijiji cha Mtakanini wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma
Shehena ya Mahindi yakiwa katika Hifadhi ya Chakula ya Kanda ya Songea
Watumishi wa Wakala wa hifadhi ya Chakula Kitengo cha Kanda ya Songea wakipokea Maagizo toka kwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi
No comments:
Post a Comment