Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh Seleman Jafo akiwa ziara ya Siku mbili Mkoani Ruvuma aliweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo kwenye halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma ambapo alihitimisha ziara hiyo katika Halmashauri ya Madaba ambako alikagua Mradi wa Stend ya mabasi na kuelekea mkoani Njombe.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Jafo amesema kinachosababisha miradi ya Halmashauri kutotekelezwa kwa viwango na ubora ni kutokana na wasimamizi na watendaji kudai asilimia
katika miradi wanayoitoa kwa wakandarasi jambo linaloifanya miradi hiyo
kujengwa chini ya kiwango.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh Seleman Jafo aliyasema hayo wakati akiongea na Watumishi wa Halmashauri za Songea Vijijini na Manispaa ya Songea katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Naibu Waziri Jafo alitoa ujumbe huo baada ya kuona baadhi
ya miradi aliyoikagua ikiwa chini ya kiwango na kutoa agizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa kupitia upya miradi hiyo
kuangalia utaratibu uliotumika katika kutoa tenda.
Watumishi wa halmashauri za Manispaa ya Songea na Songea Vijijini wakisikiliza kwa makini maagizo kutoka kwa waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Seleman Jafo juu ya Utendaji wa Watumishi katika maeneo ya kazi.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh
Selemani Jafo katika Ziara hiyo amewataka Watendaji kuwa watumishi wa wananchi
badala ya kukwamisha kazi zinazohitaji utekelezaji mara moja na kazi hizo kutoziweka kwa muda mrefu.
Aidha Naibu Waziri
wa Nchi Mh Jafo amekemea vikali suala la kutanguliza rushwa katika utoaji wa tenda kwenye halmashauri. (Pichani ni Naibu Waziri wa Nchi kushoto Mh Seleman Jafo akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea alhaji Shaweji nje ya ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Naibu waziri wa Nchi |Seleman Jafo akuacha kuwakumbusha watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoe badala yake wajikite katika kuwahudumia wananchi kwa wakati.
Naibu Waziri wa Nchi akiagana na viongozi wa Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea vijijini mara baada ya kuongea na watumishi wa halmashauri hizo.
Naibu waziri wa Nchi TAMISEMI akiwa katika Mradi
wa vibanda 221 vya Stend ya Mabasi vinavyojengwa kwa nguvu za wananchi katika Halmashauri ya Madaba wilayaniSongea
Naibu waziri Jafo akipokea taarifa ya ujenzi wa Vibanda 221 katika eneo la stend ya Madaba kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kushoto Bw. Shafi Mpenda, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Shafi Mpenda amesema Mradi wa Vibanda 221 vya stend unajengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri ambapo ukikamilika utakua chini ya halmashauri mara baada ya kumaliza mkataba na wafanya biashara,
Watumishi wa Halmashauri ya Madaba wameaidi kufuata maelekezo ya serikali katika kutekeleza majukumu yao wamemuomba Naibu waziri kuwaongezea watumishi pindi ajira zitakapotoka.
Watumishi wa Halmashauri ya Madaba wakifuatilia maagizo ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh Jafo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Shafi Mpenda amesema halmashauri inakabiliwa na changamoto ya kukosa vitendea kazi kama magari kuweza kuvifikia vyanzo vyote vya mapato vilivyopo kwenye halmashauri hiyo ingawa anasema pamoja na kukosa vitendea kazi
katika kipindi cha miezi 6 wameweza kuvuka lengo walilojiwekea katika kukusanya
mapato kwa kukusanya shilingi Milioni 15 badala ya shilingi milioni 7
walizopanga kukusanya kwa miezi sita, jambo lililoungwa mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo Vastus Mfikwa
Watumishi wa halmashauri ya madaba wametakiwa kufanya kazi kwa bidii kutojiona wanyonge kutokana na uchanga wa halmashauri hiyo na uchache wao wameombwa kuwa mfano kiasi cha kuvutia watumishi wengine kwenda kufanya kazi Madaba.
Sehemu ya Mradi wa vibanda vya stend ya Mabasi vilivyopo Halmashauri ya Madaba.
Vibanda vya Stend ya madaba mradi ambao unatarajiwa kufunguliwa mapema mwezi january 2017 kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba.
Naibu waziri Jafo akikagua mradi wa Stend Madaba amesema ameridhishwa na hali inayoendelea na fedha zilizotumika ameagiza wakuu wa watendaji kusimamia miradi ya halmashauri kwa makini na kumuomba Mweka hazina kuwa makini katika matumizi.
Jengo la choo cha stend ya Madaba
Majengo ya Mradi wa Vibanda vya biashara eneo la Stend ya Madaba
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Vastus Mfikwa amesema Baraza la Madiwani liko imara kushirikiana na wataalamu katika kuhakikisha halmashauri ya Madaba inasonga mbele kwa kasi katika maendeleo.
Watumishi wa Halmashauri ya Madaba wakiwa nje ya Jengo la Halmashauri hiyo mara baada ya kuongea na Naibu Waziri wa Nchi Tamisemi.
Naibu Waziri
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Selemani Jafo katika ziara hiyo aliweza kukagua
miradi mbalimbali ya halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma ikiwemo mradi wa Maji na mradi wa MESS wa Ukarabati
vyumba 4 vya madarasa na matundu 10 ya vyoo kwenye halmashauri ya Songea na
Mradi wa vibanda 221 vya Stend ya Mabasi Halmashauri ya madaba, ambapo
hakuridhishwa na mradi wa MESS wa ukarabati wa madarasa na matundu 10 ya vyoo
uliogharimu shilingi milioni 188 kwa
kuwa ulionekana kuwa chini ya kiwango ukilinganisha na thamani ya fedha iliyotumika.
Watumishi wa Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Vastus Mfikwa akimshukuru naibu waziri kwa nasaha zake kwa watumishi wa halmashauri hiyo amemuomba kutoisahau madaba katika mipango mbalimbali kwa maendeleo ya halmashauri hiyo.
Watumishi Halmashauri ya Madaba
Mh Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh Seleman Jafo.
No comments:
Post a Comment