Katika Ziara hiyo Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipata fursa ya kuzindua Mradi wa maji katika Kijiji cha Magingo Halmashauri ya madaba wilayani Songea mkoa wa Ruvuma mradi uliogharimu
kiasi cha shilingi 1,92,439,812.
Waziri Mkuu mara baada ya kukata utepe wa kuashirikia uzinduzi rasmi wa Mradi wa maji kwa wananchi wa Halmashauri ya Madaba aliweza kufungua maji na kujaza katika plastiki yenye ujazo wa lita 2o kama anavyoonekana pichani akifungulia maji. Amewataka wakaazi wa kijiji cha magingo na vijiji jirani kuutunza mradi huo kwa kuhakikisha miundo mbinu yake hairibiwi ili uwanufaishe kwa muda mrefu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiinua ndoo ya maji kumtwika mama kama sehemu ya kuzindua matumizi ya maji hayo kwa wananchi wa eneo la mradi. Amesisitiza kuundwa kwa kamati za maji zitakazoshirikiana katika ulinzi wa mradi huo.
Viongozi wa halmashauri na mbunge wa Jimbo la madaba Joseph Kizito Mwagama wakifurahia kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji ambao utawaondolea hadha ya kufuata maji umbali mrefu wakaazi wa eneo la mradi.
Wananchi wa Kijiji cha Magingo wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa maji uliozinduliwa na mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet kamando Mgema akitoa taarifa ya mradi wa Maji Madaba mbele ya waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu katika Ziara hiyo halmashauri ya Madaba pia alikagua Mradi wa Kituo cha kupooza Umeme kilichopo Mtepa Madaba Wilaya ya Songea. Aidha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amewataka Wananchi wa mkoa wa Ruvuma kulinda vyanzo vya Maji, ili kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanayoendelea..
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr binilith Satano Mahenge akieleza shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mh Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa
Kassim amesema hali ya Mvua kwa sasa ni mbaya sana kiasi watu
wameshindwa kupanda mbegu kwa wakati katika mashamba yao hali hiyo imetokana na uharibifu
wa Mazingira.
Waziri Mkuu amesema mtu atakayepatikana akiwa na lengo la kuharibu Mazingira kwa makusudi mtu huyo ashughulikiwe hukohuko anakoharibu mazingira.
Waziri Mkuu akiendelea amesema ni Marufuku mtu yeyote kulima au kufanya shughuli zozote za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji atakayebaini hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Waziri Mkuu akizungumza kuhusu suala la Elimu upande wa
Mtoto wa kike, amesema yeyote
atakayehusika kukatisha masomo ya moto wake kwa kumuoza au namna nyingine, Baba aliyeoza na
walioowa adhabu yao miaka 30 jela.
Katika ziara hiyo pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea kituo cha Afya cha madaba kuona utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kuongea na watumishi wa kituo hicho kuwataka kufanya kazi kwa makini katika sekta yao ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu.
Watumishi wa halmashauri ya Madaba wilayani Songea wakisikiliza maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipoongea na watumishi hao.
Waziri Mkuu ameendelea kuwasisitiza watumishi kufanya kazi za wananchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea waendane na serikali ya awamu ya tano
Amesema wananchi wanahitaji huduma na siyo masemango wameajiriwa ili kuwatumikia ni vema wakawaheshimu kwa kuwahudumia ipasavyo.
Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa tanzania Mh Kassim Majaliwa ameonya watumishi wanaofanya kazi kwa lengo la kujipatia mshahara bila kutimiza wajibu wao waache mara moja.
Waziri Mkuu katika Ziara yake aliweza kukabidhi Pikipiki kwa vijana 11 wa Madaba ili ziwasaidie katika kujikwamua kiuchumi kupitia biashara ya bodaboda
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mwagama akikakibidhi pikipiki
Waziri Mkuu katika ziara hiyo pia alitembelea Mradi
wa upandaji miti Wino Madaba kuona shughuli za kilimo cha miti katika kukabiliana na uhifadhi wa misitu unaofanywa chini ya wakala wa huduma za misitu (TFS)
Ziara ya Waziri Mkuu katika kijiji cha Wino Eneo la Mradi wa Mashamba ya Miti Halmashauri ya madabaWaziri Mkuu akipokea maelezo ya mradi wa Miti wino kutoka kwa Meneja wa Wakala wa huduma za Misitu
Waziri Mkuu na Viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika Ziara yake aliyoifanya januari mwanzoni 2017 katika kutembelea miradi mbalimbali ya Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Waziri Mkuu akipata ufafanuzi jinsi wakala wa Huduma za Misitu wanavyoendesha shughuli za mradi huo na faida wanazozipata wananchi wanaoishi jirani na mradi huo ikiwemo na ajira za muda mfupi na mrefu.
Meneja wa Mradi wa Shamba la Miti Wino kutoka wakala wa Huduma za Mazao ya Misitu akimueleza waziri Mkuu malengo ya mradi huo.
Waziri Mkuu akiwa Ikulu ndogo Songea katika Mkutano wa Majumuisho ya Ziara yake ya Siku tano Mkoani Ruvuma. Kulia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Kilian Mwisho
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tananzia kushoto sambamba na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani wakifuatilia maelezo ya mradi wa Miti na kuomba ufafanuzi.
Eneo la Majengo ya TFS kijiji cha wino ambako mradi wa miti unatekelezwa kwa jitihada kubwa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani akitolea ufafanuzi juu ya uhifadhi wa misitu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ziara ya Waziri Mkuu Wino Halmashauri ya madaba
Shamba la miti inayolimwa katika Kijiji cha wino kilimo cha biashara ya Miti
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika Kikao cha Majumuisho ya Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu ndogo Songea.
Kikao cha majumuisho ya Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu aliagiza kukamatwa kwa watu wanne wilayani Masasi waliosababisha
wakulima wa korosho wilayani humo kutolipwa fedha zao baada ya kuuza
korosho tani 2,138 na kulipwa fedha pungufu bila maelezo na kusababisha hasara
ya shilingi biloioni 23
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema wakulima wanatakiwa kusaidiwa na viongozi, Wakulima wa Masasi baada ya kuuza korosho zao Tani 2138 walilipwa fedha pungufu kwa madai kuwa korosho zao zilikuwa nyaufu jambo ambalo siyo la ukweli
Waziri Mkuu alipokuwa akizungumza
juu ya Campuni ya TNCOAL inayochimba Makaa ya mawe katika Kijiji cha Ngaka Kata
ya Rwanda wilayani Mbinga amesema kampuni hiyo imedai kuwa tangu mwaka 2011
hadi sasa inafanya kazi kwa hasara jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuagiza uchunguzi zaidi ufanyike juu ya uendeshaji wa mgodi wao.
Waziri Mkuu ameagiza SAG kufuatilia kwa karibu mwenendo wa uendeshaji wa Mgodi wa Makaa ya Mawe Rwanda na ripoti aipate mapema ili kuona mustakabali wa wananchi wanaoishi katika eneo la Mgodi huo namna wanavyonufaika nao.
Waziri mkuu ametaka watendaji wa serekari viongozi wa siasa
na viongozi wa dini kuwa na umoja ili kulinda amani na utulivu tulionao
.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema pamoja na mambo yote anawashukuru wasanii wa ngoma mbali mbali kwa kutunga nyimbo mbalimbali ambazo zina hamasisha amani.
Waziri Mkuu wa hamhuri ya Muungano wa Tanzania akiagana na viongozi katika uwanja wa ndege wa ruhuwiko Songea baada ya kuhitimisha ziara yake.
Waziri Mkuu akiagana na viongozi wa Chama na Serikali katika uwanja wa Ndege wa Songea
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama akimshukuru waziri Mkuu kwa ziara yake ambayo imetoa mtazamo chanya wa mwelekeo wa Serikali katika kuwahudumia wananchi kwa dhamira ya kuwaletea maendeleo
Viongozi wa kamati ya Ulinzi na usalama wakiagana na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa ruvuma ACP Zuberi Mwombeji akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimuhakikishia Mkoa wa Ruvuma unakuwa na amani ulinzi upo imara.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akifurahi wakati alipokuwa akiagana na Mh Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri Mkuu kusalimiana na Kamati ya Ulinzi na usalama Ruhuwiko muda mfupi kabla ya kuondoka
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akimuhakikishia Waziri Mkuu usalama wa chaklula katika wilaya ya Songea na jitihada za wakulima katika kilimo hali ya hewa haiwezi kuwakatisha tamaa ya kuendelea kulima.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaji Shaweji akiagana na Waziri Mkuu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko katika uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko Songea wakati wa kuagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani akiagana na Waziri Mkuu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma Uwanja wa ndege Ruhuwiko Songea
Viongozi mbalimbali waliojitokeza kumsindikiza waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Uwanja wa Ndege wa Songea.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Majaliwa Kassim Majaliwa akiwaaga Viongozi mbalimbali baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tato mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge, Mkiti wa CCM Mkoa Odo Mwisho na Mama Helen Mwambungu wakiagana na Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
picha ya uzinduzi wa mradi wa maji madaba
Watumishi wa Kituo cha Afya Madaba Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI RUVUMA
Wakuu wa Wilaya
No comments:
Post a Comment