Kaimu Mkurugenzi wa uzuiaji wa Ujangiri dhidi ya wanyama
Pori Robert Mande amewaasa wananchi kuachana na ujangiri kwa
sababu sasa hivi biashara ya pembe za ndovu hazina soko kwa kuwa wafanya biashara
wakubwa wa biashara hiyo wamesha kamatwa kudhihirisha hilo hata mizoga ya tembo walio
kuwa wana uwawa imepungua kutoka 184 hadi kufikia mizoga 84
Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Tunduru amewataka watu wanaomiliki Silaha za
kijeshi kuzisalimisha kwenye Vituo vya Polisi
Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Tunduru ameyasema hayo baada ya Tembo wawili
kuuwawa na mmoja kung`olewa meno yake katika Kijiji cha Wenje Tarafa ya Nalasi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tunduru
Juma Homera amesema imebainika kuwa wananchi wanaoishi karibu na miapaka ya
Nchi jirani wanapata silaha za kijeshi kwa kubadilishana silaha hizo na chakula
amesema wale wote wenye silaha hizo wazisalimishe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Juma Homera
amesema watuhumiwa waliokamatwa kuhusika na tukio hili la ujangiri wako 8 nane ambao walikutwa na silaha zilizotumika kuuwa wanyama na baadhi ya pembe za ndovu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wilaya ya Tunduru akiwataja watuhumiwa hao amesema wa kwanza ni Juma saidi Ally(36) , Mwinyi Omary (24), Salumu Charamanda Aski (46), Kalengo Mkenda( 45), Fadhili Mohamed( 43), Abduli Shaibu (37), Ahamad Yasini( 30), Rashid Hausi (46)
Naye Afisa Upelelezi kutoka Kitengo cha Ujangiri Makao Makuu Dar es Salaam amesema wahalifu wamekuwa wakifanya vitendo vya Ujangiri kwa kujidanganya watakuwa salama kwa kuwa wanatumia dawa za kienyeji zinazowaaminisha kutokamatwa pindi wanapofanya ujangiri huo.
Majangiri wamekuwa wakitumia silaha za risasi wakati wa kutekeleza dhima yao ya kuangamiza wanyama ambao ni rasilimali za Taifa jambo ambalo haliwezi kuungwa mkono na Serikali.
Kaimu Mkurugenzi wa Oparesheni za kuzuia Ujangiri Taifa
amesema mpaka sasa kuna watu 320 ambao wamekamatwa kwa makosa ya Ujangiri na
watuhumiwa 284 wamefikishwa mahakamani
pia kuna Taarifa ya watu 1006 kuwa
ni Majangiri amewataka watu wanaojihusisha na Ujangiri wajisalimishe.
Kaimu Mkurugenzi wa Kikosi cha Kupambana na Ujangiri Taifa akitoa Elimu kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru juu ya Madhara ya kuangamiza waanyama pori na kutumia kitoeo pasipo kuzingatia taratibu za kiafya.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru amesema wananchi waliohusika na tukio la ujangiri na kukimbia watasakwa popote walipo ili kuhakikisha wanachukuliwa hatua stahiki na vyombo vya dola.
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika Tarafa ya Nalasi eneo la Tukio ambako Tembo wawili waliuwawa na wananchi.
Afisa Upelelezi akionyesha dawa ambazo zimekuwa zikitumiwa na wanaojihusisha na Ujangiri na kuamini wakifunga dawa hiyo serikali haiwezi kuwakamata inawalinda.
Mratibu Maximillan
Janes wa Shirika la PAMS Foundation
linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ujangiri amesema shirika lime toa ndege mbili ambazo
zita husika na kulinda wanya wasiingie katika makazi ya watu pia kufuatilia
mienendo ya watu wanao jihusisha na ujangili
Aidha Mratibu amesema wananchi wakiona wanyama wameingia
katika makazi watoe taarifa ofisi ya mtendaji ili kuweza kusaidia mara moja kuwafukuza wanyama hao, pia katika
kuepukana na uvamizi wa tembo wananchi katika mashamba yao wajaribu kupanda
pilipili kwa kuwa adui mkubwa wa Tembo ni pilipili
Shirika la kimataifa la PAMS Fondation lina fadhili njia
mbalimbali za kupambana na ujangiri na kulinda usalama wa wanyama na mali za
raia katika maeneo jirani na hifadhi kwa kuhakikisha wanyama wana kuwa salama muda
wote, Wananchi kuanzia watambue kuwa Wanyama walioko katika mbuga zao ni mali yao
kwani fedha za utalii zinazo patikana zinasaidia Nyanja mbalimbali katika jamii
ikiwemo Elimu,Afya,na mindombinu mbalimbali.
Nao wananchi wa wilaya ya Tunduru wameomba Serikali kuwadhibiti wanyama waharibifu kabla ya kuleta madhara kwa binadamu kwa kuharibu mashamba ama kuvamia makazi ili kuepukana na migongano inayojitokeza kati ya Wananchi na Viongozi wa Serikali.
Wananchi hao wakiwa katika Mkutano wa pamoja na viongozi wanaohusika na kupaambana na Ujangiri wamesema wao wapo tayari kufuata taratibu kwa kulinda wanyama wa asili lakini wanaomba Maafisa wanyamapori wanapotembele doria katika Hifadhi kutumia busara badala ya kutoa vitisho kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment