Zaidi ya Shilingi Milioni 300 zimepatikana baada ya
Kampuni ya KAPONDOGORO AUCTION MARK kuwadai wadaiwa sugu waliokopa katika vyama
vya ushirika kati ya shilingi bilioni 4 zinazodaiwa kwa vyama vya ushirika
Mkoani Ruvuma.
Meneja wa Kampuni ya Kapondogoro Auction Mart Julius
Aron Mashauri ameyasema hayo wakati akipiga Mnada wa vitu vya Wana ushirika
ambao walikopa na kushindwa kurejesha Madeni.
Mnada Uliofanywa na Kampuni
ya KAPONDOGORO AUCTION MARK katika mkoa wa Ruvuma ulijumuisha uuzaji wa Magari, Pikipiki Fenicha
za ndani pamoja na madeni ya nyuma vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 300,000,000 katika kutekeleza
agizo la Waziri Mkuu la kukusanya madeni
yote na kuweza kufufua vyama vya
Ushirika.
Kwa Mujibu wa Meneja wa Kampuni
ya KAPONDOGORO AUCTION MART amesema
uzoefu unaonyesha wananchi wakikopa hudhani Serikali inasahau lakini siku ya
siku wanajikuta Mali zao zikiuzwa na kuziacha familia katika changamoto. Mkoa
wa Ruvuma una wadaiwa sugu wanaodaiwa na
Vyama vyama vya ushirika zaidi ya shilingi
bilioni 4
No comments:
Post a Comment