Wadau wa Mazingira Mkoani Ruvuma wametakiwa kulinda Mazingira ili kuweza kuepukana na
Janga la kukosa mvua na kushindwa kukabiliana na uharibifu wa
Hewa Ukaa.
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith
Satano Mahenge amewataka
wafanya kazi wa TFS kuacha kujadiliana
na waharibifu wa Mazingira badala yake Mali zinazokamatwa zitaifishwe baada
ya kukidhi masuala yote ya kisheria.
Kaimu meneja wa Wakala wa
Huduma za Mazao ya Misitu (TFS) wilaya ya Songea Juma Omary Mbwambo amesema sasa hivi Mazao ya misitu
hupelekwa Nchi jirani ya Msumbiji baada
ya kuona udhibiti wa usafirishaji mkaa nje ya Mkoa wa Ruvuma umedhibitiwa.
Mkoa wa Ruvuma umekuwa
ukikabiliana na waharibifu wa Mazingira baad ya kuona eneo lililobaki kuchoma
mkaa ni Ruvuma na Mbao zenye ubora zinapatikana mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment