KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, August 3, 2017

MNADA WA HADHARA WA FANYIKA SONGEA KUNUSURU MALI ZA USHIRIKA



Zaidi ya Shilingi Milioni 300 zimepatikana baada ya Kampuni ya KAPONDOGORO AUCTION MARK kuwadai wadaiwa sugu waliokopa katika vyama vya ushirika kati ya shilingi bilioni 4 zinazodaiwa kwa vyama vya ushirika Mkoani Ruvuma.
Meneja wa Kampuni ya Kapondogoro Auction Mart Julius Aron Mashauri ameyasema hayo wakati akipiga Mnada wa vitu vya Wana ushirika ambao walikopa na kushindwa kurejesha Madeni.
  
Mnada Uliofanywa na Kampuni ya KAPONDOGORO AUCTION MARK katika mkoa wa Ruvuma  ulijumuisha uuzaji wa Magari, Pikipiki Fenicha za ndani pamoja na madeni ya nyuma vyote vikiwa na thamani ya zaidi  ya shilingi 300,000,000 katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la  kukusanya madeni yote na kuweza kufufua  vyama vya Ushirika.

Kwa Mujibu wa Meneja wa Kampuni ya KAPONDOGORO AUCTION MART amesema uzoefu unaonyesha wananchi wakikopa hudhani Serikali inasahau lakini siku ya siku wanajikuta Mali zao zikiuzwa na kuziacha familia katika changamoto. Mkoa wa Ruvuma una wadaiwa sugu wanaodaiwa na
 Vyama vyama vya ushirika zaidi ya shilingi bilioni 4

TFS SONGEA WAKAMATA MBAO NA KUWA FIKISHWa MAHAKAMANI



Wadau wa Mazingira Mkoani Ruvuma wametakiwa  kulinda Mazingira ili kuweza kuepukana na Janga la  kukosa  mvua na kushindwa kukabiliana na uharibifu wa Hewa Ukaa.

Hayo yamebainika baada ya Wakala wa Huduma za Mazao ya Misitu (TFS) kukamata Gari lenye namba za usajili T. 194 ABL Aina ya SCANIA likiwa n mbao 400 pamojana Mkaa  ukiwa na thamani ya shilingi 24,871,944

Mkuu wa Mkoa  wa  Ruvuma  Mhandisi  Dr. Binilith  Satano Mahenge  amewataka wafanya  kazi wa TFS kuacha kujadiliana na waharibifu wa Mazingira badala yake Mali zinazokamatwa zitaifishwe baada ya  kukidhi masuala yote ya kisheria.

Kaimu meneja wa Wakala wa Huduma za Mazao ya Misitu (TFS) wilaya ya Songea Juma Omary  Mbwambo amesema sasa hivi Mazao ya misitu hupelekwa Nchi  jirani ya Msumbiji baada ya kuona udhibiti wa usafirishaji mkaa nje ya Mkoa wa Ruvuma umedhibitiwa. 
 Mkoa wa Ruvuma umekuwa ukikabiliana na waharibifu wa Mazingira baad ya kuona eneo lililobaki kuchoma mkaa ni Ruvuma na Mbao zenye ubora zinapatikana mkoa wa Ruvuma.