KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, December 31, 2011

VIONGOZI WA MKOA WA RUVUMA WALIFANYA NINI MKOANI RUVUMA ?

Kiongozi wa kitaifa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha upendo kwa mkoa wa Ruvuma Kwakuweza kutoa Genereta ili wananchi wapate Umeme Rais hakuweza kuishia hapo aliongeza kiwango cha Pembejeo mkoa wa Ruvuma,Hapo juu ni pale alipo tembelea Mkoa wa Ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu Ameupokea Mkoa wa Ruvuma kwa kuwa mwazi na Mchapakazi kitu tulicho jifunza kwake kwa mwaka 2011 hataki Majungu, wala Kumsengenya Mtu sasa Swali lina kuja jee mwaka 2012 gia yake nini Wanaruvuma tuna takiwa kumunga mkono

Waziri mkuu wa zamani mh. Edward Luwasa alikuwa imara katika uongozi lakini kama isemavyo bibilia Yesu lazima afe ili aikomboe ulimwengu ndivyo alivyo kuwa shujaa huyu watanzania lazima wa shukuru kwa kile alicho fanya


Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda katika mwaka 2011 ameweza kupunguza maswala ya uhalifu kwa asilimia 89 %pia ameimarisha ulinzi shirikishi kwa asilimia 50% jee mwaka 2012 ataweza kutokomeza majambazi na kuweza kuzuia uhalifu

Waziri wa Habari Utamaduni Michezo na Vijana Emanueli John Nchimbi toka achaguluwe kuwa mbunge ameweza kuimarisha barabara za mji wa songea pia kuongeza idadi ya secondari , mbunge wa Jimbo la Songea amejitolea kujenga secondari ya Mkuzo kwautoa fedha zake mwenyewe zaidi ya shilingi milioni 100

Mkuu wa Veta Gidioni ambaye toka afike ameweza kupunguza ajali mbalimbali kwa kutoa elimu kwa madereva kwa mwaka 2011 jee jyhudi zake mwaka 2012 zitakuwaje

Mkurugenzi wa The Foundation John Ulanga amekuwa kiongozi imara kwa kuweza kuimarisha Azaki Nchini Tanzania kwa kuweza kuziwezesha kifedha kukabiliana na Umasikini Tulionao Nchini Tanzania kwa kuziwezesha Azaki kutoa elimu ya Utawala Bora,Jinsi ya Kujiondoa na Umasikini jee juhudi zake mwaka 2012 zita kuwaje ?

Kamanda wa kikosi cha FFU Maile ambaye aliweza kuhimili maswala ya Uchaguzi mkuu

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliye pita Saidi Saidi Kalembokatika uongozi wake aliweza kuinua kiwango cha Elimu hadi mkoa wa Ruvuma Kuchukua Nafasi ya Nne Kitaifa


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliye pita Crisitina Ishengoma katika uongozi wake ameweza kuinua kilimo mkoa wa Ruvuma kwa Asilimia 100 hadi serekari kuelemewa na ununuzi wa mahindi

Thursday, December 29, 2011

SONNGO WAENDESHA MCHAKATO WA KATIBA SONGEA

Washiriki wa Mdahalo wa mchakato wa Katiba Mpya wakisikiliza maelezo ya jinsi ya kushiriki kupata Katiba Mpya

Waandishi wa Habari wakiwa katika Mdahalo wa Mchakato wa katiba ulio fadhiliwa na The Foundation na kuendeshwa na Shilika lisilo la Kiserekari SONNGO Kutoka kulia ni Juma Nyumayo wa Uhuru FM ,anaye fuatia na Gidioni Mwakanosya wa Gazeti la Nipashe anaye Fuatia ni Catherin Nyoni wa TBC

Washiriki wa Mdahalo wa mchakato wa katiba manspaa ya Songea ulioendeshwa na SONNGO Katika ukumbi wa Romani Catholic Bombambili wakiwa makini kusikiliza mada

Washiriki wa mdahalo wa mchakato wa katiba wakibadilishana mawazo kutoka kulia ni Jongo Jongo na kushoto kwake ni Adam NindiHakimu mkaazi wa Makama ya Songea Elithabet Sinzika akitoa mada katika mdahalo wa mchakato wa katiba akielezea haki za waandishi wa Habari katika mahakama


matibu wa SONNGO Mathew Ngalimanayo akirabibu maswala ya Mchakato wa Katiba Mpya katika Ukumbi wa Roman Catholic Bombambili

Mwana sheria akitoa maada kuhusu ubora wa Katiba ya Zamani na kuwa Taka wananchi wajisomee kwa makini katiba ili wanapo changia wajue kitu wanacho changia

Wednesday, December 28, 2011

MAMA AUWAWA KIKATILI ATUPWA PORINI SONGEA NDUGU HAWAJAPATIKANA

Mama aliye uwawa kikatili na maiti yake kutupwa Porini eneo la Luwiko Songea mpaka sasa haja patikana ndugu yake ,mama ni mnne mweusi ana kadiriwa kuwa na miaka kati 30 na 35 maiti ipo Hospitali ya Mkoa Songea yeyote aliye potelewa na Ndugu atoe Tarifa Police Songea

MTOTO ATUPWA PORINI NA MTOTO MWINGINE ATELEKEZWA NA MAMA YAKE SONGEA

Naomba niulize kwa watanzania wenzangu Tabia ya Kutupwa watoto ovyo ina sababishwa na nani Jamii inayo tuzunguka au Tabia mbaya ya kizazi kipya tulicho nacho ? Ndugu zangu unaweza kusema hizi ni hadithi lakini ni ukweli usio pingika mtoto unaye mwona hapo juu ni mtoto Bakari Haule ambaye alitupwa na mama yake porini na kuanza kutafunwa na wadudu kama unavyo ona kichwa kilivyo liwa

Mama mzazi wa mtoto Baraka Haule mwenye umri wa miezi miwili akiwa mpakata mtoto Baraka Haule mara baada ya kukamatwa na polisi mkoani Ruvuma

Mama Salini Salumu akiwa amemshika mtoto a,mbaye alimtelekeza mlangoni kwa nyumba ya baba watoto wake baada ya kukosa huduma ,


Mtoto aliye telekezwa na mama yake Naimu Baraka akiwa kituo cha Police baba ya Baba yake kujisalimisha Police kutoa maelezo ya mtoto

Tuesday, December 27, 2011

MANSPAA YA SONGEA YA GUBIKWA NA UCHAFU

Wanawake wanalazimika kufanya kazi za hatari kiafya katika kujikwamua na hali ngumu ya uchumi pichani mama akisafisha mji bila vifaa bora vya kujilinda kiafya, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeshindwa kumsadia mwajiri wao kwa kumpa vitendea kazi vinavyoendana na mazingira mazuri jee TGNP kama wanaharakati wanaotetea haki za wanawake mnatoa ushauri gani kwa akina mama wanaofanya kazi ktk mazingira hayo.

Pichani hapo juu ni hali halisi ya Mji wa Songea ambao maguba yake yameelemewa na shehena ya Uchafu tena ni Maguba ambayo yapo ukingoni mwa Barabara za Magari Uongozi wa Manispaa unachukua hatua gani.

Pichani ni halisi inavyoonekana Maji machafu yakiwa yamechanganyika na uchafu mbalimbali katikati ya Mji wa Songea pembeni kukiwa na wafanya biashara wakiendelea na biashara huku wakivuta harufu kali ya uchafu. jee katika hali ya kawaida wananchi wanaokuja kupata huduma kwa wafanya biashara hao watakosa kupata magonjwa ya milipuko? nani alaumiwe Halmashauri ya Manispaa, Wananchi Serikali ya Mkoa.

Wafanya biashara wa Mabucha ya Nyama na wauza Viungo wakiendelea na biashara huku pembeni kukiwa na hali ya uchafu uliokithiri wasiwe na wasiwasi.

Hiyo ni hali ya Usafi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo haieleweki kama hali hiyo inatokana na uhaba wa vitendea kazi vya kuzolea uchafu huo, uhaba wa vibarua ama ni uwajibikaji wa wahusika wanaotakiwa kusimamia usafi wa Mji.

Pichani ni wafanyabiashara wa Soko Kuu la Songea likionekana kugubikwa na uchafu aliyevaa nguo nyeupe ni muuza nyama jee kama hali ndiyo hiyo vyakula vinavyotoka hapo vitakuwa salama kwa watu? na hili ni soko kuu Masoko mengine hali ikoje, toa maoni yako.

Mama huyu anaonekana akiwa anfanya usafi sehemu zenye uchafu wa hatari pasipo kuvaa gloves wala buti au viatu unafikiri akifanya kazi hiyo kwa muda wa miezi 6 hali yake ya kiafya itakuwa salama? Nini kifanyike na yeye anafanya hayo katika kujikwamua na maisha ili apate ridhiki ya kuwasaidia wanae na kujikimu mwenyewe halmashauri ya Manispaa inawasaidiaje vibarua hawa katika kuwalinda na maradhi kazini.

Sunday, December 25, 2011

MATUKIO KATIKA SIKUKUU YA CRISMAS RUVUMA

Waumini wa Dhehebu la Lutherani wakiwa katika Ibada ya Krismas Mjini Songea

Wanakwaya wa Kanisa la Lutherani wakifurahia kuzaliwa kwa Mkombozi wao Yesu Kristo ikiwa ni ishara ya upendo na ukombozi kwao katika Ibada ya Sikukuu ya Krismas.


Wachungaji wa Kanisa la Lutherani wakifurahia tunu zilizokuwa zikitolewa na waumini wao ikiwa ni ishara ya Upendo kwa kujiwa na Mkombozi wao Yesu Kristo


Watoto wa Kipapa wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Songea wakiwa katika Ibada ya Krismas kanisa la mtakatifu Matias Mlumba Kalemba

Padri na wahudumu wakiwa katika Misa Takatifu ya Krismas katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Matias Mlumba Kalemba Jimbo la Songea


Mchungaji John Msyani wa Kanisa la Moraviani akisisitiza kuendeleza Upendo kwa waumini wa Kanisa la Moraviani katika kusherekea Sikuu ya kuzaliwa kwa Yesu.


Waumini wa Kanisa la Moraviani wakisikiliza kwa makini mahubiri mazuri ya Mchungaji John Msyani katika Ibada ya Sikukuu ya Krismas katika kanisa la Moraviani Songea Manispaa.



Waumini wanafunzi wa Sekondari ya wasichana Songea wakifuatilia kwa usikivu mkubwa Ibada ya Krismas katika Kanisa la Moraviani Songea Manispaa.

Sunday, December 18, 2011

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID THABITH MWAMBUNGU AWA TAKA WANACHI KUTUMIA VIZURI BARABARA ILI KUEPUKANA NA VIFO VINAVYO TOKANA NA VYOMBO VYA MOTO

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa vyeti kwa wahimu 105 walio hitimu mafunzo ya Udereva Katika chuo cha Veta Mkoani Ruvuma kulia ni Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Veta Gidion Lairumbe

Mkuu wa Chuo cha Veta Gidion Lairumbe akisikiliza kwa makini wakati akibadilishana mawazo jinsi ya kuongeza nguvu kukifanya chuo hicho kiwe chanzo cha kupunguza ajali barabarani kwa kutoa Elimu Bora na siyo Bora Elimu

Wahitimu 105 walio hitimu mafunzo ya Udereva katika chuo cha Veta Mkoani Ruvuma waliaswa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma kuwa makini wawapo barabarani Uhai wa watu unawategemea wao, pia nao wawe na Huruma na Roho zao wanapo Endesha Gariili kunusuru vifo kwa watu

Saturday, December 17, 2011

AZAKI ZISIZO ZA KISEREKARI ZA KUTANA DODOMA

Ufikapo Dodoma jambo la kwanza ni jinsi mji huo unavyo tunzwa katika hali ya usafi jambo hili ni jambo la kuigwa hata azaki zinapo fanya mikutano yake Dodoma ni juu ya Azaki kwenda kuhamasisha usafi katika sehemu zao Mtandao waRuvuma ujulikanao kwa jina la RUNECISO umeshuhudia usafi katika mji wa Dodoma hapo juu ni sehemu ya mgawanyo wa mpishano wa magari

Mtalamu kutoka Foundation Dar - es -salaam Omary Jecha akitoa mafunzo kuhusu mafanikio na changamoto zilizo ikabili Azaki nini kifanyike nani chakuongeza katika ukumbi wa Dodoma hotel

Washiriki kutoka Tanzania bara na visiwani walio hudhulia washa ya kutasimini kazi zilizo fanywa na kufadhiliwa na The Foundation Tasimini iliyo fanyika jijini Dodoma .

Mjumbe kutoka Mbinga Benedict Lwena akimsikiliza kwa makini mwezeshaji Omary Jecha kutoka Foundation .kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao RUNECISO ndugu Adam Nindi kutoka mkoa wa Ruvuma wakiwa katika ukumbi Dodoma Hotel

Wednesday, December 14, 2011

MEJA AHEMED MGUMBA AKIWA KAZINI MKOANI RUVUMA

Meja Ahemed Mgumba akiwa mkoani Ruvuma huku akiwa ana Peruzi kila kitu ambacho ana weza kumshauri Mh.Emanuel John Nchimbi katika kuwasaidia wananchi waliko pembezoni,



Dr Daniel Malekela akiwa sambambamba na Mh.Emanuel John Nchimbi wakiwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma nyuma ni meja Ahemed Mgumba

Tuesday, December 13, 2011

WAZIRI WA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEA HOSIPITARI SONGEA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dokta Emmanuel John Nchimbi akitoa Taarifa kwa waandishi wa Habari jinsi serekari ilivyo jipanga kuimarisha Hospitali ya Mkoa Songea kuwa Hospitari ya Rufaa


Wajawazito wakiwa nje ya wodi baada ya wagonjwa kufurika katika wodi ya wazazi ambayo ina uwezo wa kuchukua wajawazito 50 tu hivi sasa wapo zaidi ya 200


Mheshimiwa Waziriri Emanuel John Nchimbi akiwa na mganga mkuu Dr Daniel Malechela wakiweka mikakati endelevu ili kukabiliana na wagonjwa wanao toka nje ya wilaya hasa Namtumbo ili wapate huduma bora baada ya kufika hospitali ya mkoa kwa ajili ya kujifungua[picha ya chini].