KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, December 27, 2011

MANSPAA YA SONGEA YA GUBIKWA NA UCHAFU

Wanawake wanalazimika kufanya kazi za hatari kiafya katika kujikwamua na hali ngumu ya uchumi pichani mama akisafisha mji bila vifaa bora vya kujilinda kiafya, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeshindwa kumsadia mwajiri wao kwa kumpa vitendea kazi vinavyoendana na mazingira mazuri jee TGNP kama wanaharakati wanaotetea haki za wanawake mnatoa ushauri gani kwa akina mama wanaofanya kazi ktk mazingira hayo.

Pichani hapo juu ni hali halisi ya Mji wa Songea ambao maguba yake yameelemewa na shehena ya Uchafu tena ni Maguba ambayo yapo ukingoni mwa Barabara za Magari Uongozi wa Manispaa unachukua hatua gani.

Pichani ni halisi inavyoonekana Maji machafu yakiwa yamechanganyika na uchafu mbalimbali katikati ya Mji wa Songea pembeni kukiwa na wafanya biashara wakiendelea na biashara huku wakivuta harufu kali ya uchafu. jee katika hali ya kawaida wananchi wanaokuja kupata huduma kwa wafanya biashara hao watakosa kupata magonjwa ya milipuko? nani alaumiwe Halmashauri ya Manispaa, Wananchi Serikali ya Mkoa.

Wafanya biashara wa Mabucha ya Nyama na wauza Viungo wakiendelea na biashara huku pembeni kukiwa na hali ya uchafu uliokithiri wasiwe na wasiwasi.

Hiyo ni hali ya Usafi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo haieleweki kama hali hiyo inatokana na uhaba wa vitendea kazi vya kuzolea uchafu huo, uhaba wa vibarua ama ni uwajibikaji wa wahusika wanaotakiwa kusimamia usafi wa Mji.

Pichani ni wafanyabiashara wa Soko Kuu la Songea likionekana kugubikwa na uchafu aliyevaa nguo nyeupe ni muuza nyama jee kama hali ndiyo hiyo vyakula vinavyotoka hapo vitakuwa salama kwa watu? na hili ni soko kuu Masoko mengine hali ikoje, toa maoni yako.

Mama huyu anaonekana akiwa anfanya usafi sehemu zenye uchafu wa hatari pasipo kuvaa gloves wala buti au viatu unafikiri akifanya kazi hiyo kwa muda wa miezi 6 hali yake ya kiafya itakuwa salama? Nini kifanyike na yeye anafanya hayo katika kujikwamua na maisha ili apate ridhiki ya kuwasaidia wanae na kujikimu mwenyewe halmashauri ya Manispaa inawasaidiaje vibarua hawa katika kuwalinda na maradhi kazini.

No comments:

Post a Comment